Shirika
lisilo la kiserikali la Doctor with Africa CUAMM linalofanya kazi na Mkoa wa
Simiyu kama mdau wa Afya katika masuala ya UKIMWI na Huduma za Afya ya Mama na mtoto
limetoa msaada wa vifaa kinga (viambukuzi) kwa ajili ya kuunga mkono Serikali
katika kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akikabidhi msaada huo Mei 06, 2020 mjini Bariadi kiongozi kutoka
CUAMM Bi. Barbara Andreuzizi amesema Vifaa
kinga hivyo vina thamani ya shilingi milioni
nne ambapo amebainisha kuwa Shirika hilo pia limetoa msaada mafuta na gari
litakalotumiwa na wataalam wa afya kutoa elimu ya tahadhari ya maambukizi ya Virusi
vya Corona katika mkoa wa Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ameshukuru CUAMM kwa kutoa msaada huo ambao ni
sehemu ya makubaliano ya wadau wa afya na serikali mkoani humo katika
kukabiliana na Corona na kuiagiza Timu ya mkoa ya usimamizi wa huduma za afya
kuhakikisha vifaa hivyo vinapelekwa haraka katika vituo vya kutolea huduma za
afya kwa wakati.
“Tatizo la COVID 19
liliporipotiwa kama mkoa tulikutana na wadau tukakubaliana kujiandaa namna ya kukabiliana nalo katika
maeneo ya utoaji elimu, vifaa kinga na vifaa tiba, tunawashukuru sana CUAMM kwa
vifaa kinga hivi ambavyo naamini vitasaidia timu zetu za usimamizi wa Afya(CMT)
za Wilaya na vituo vya kutolea huduma za afya,” alisema Sagini.
Aidha, Sagini amewataka
wataalam wa afya ngazi ya Mkoa wakiongozwa
na Mganga Mkuu wa Mkoa kusimamia mafuta na gari lililotolewa na CUAMM kwa ajili
ya kutoa elimu kwa wananchi na kuhakikisha linafanya kazi iliyokusudiwa na
elimu inawafikia wananchi inavyostahili mpaka maeneo ya vijijini.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo
Dugange Simiyu inaendelea na jitihada mbalimbali kukabiliana na maambukizi ya
virusi vya Corona ambapo amewashukuru CUAMM kutoa msaada wa vifaa kinga vitakavyosaidia
katika utoaji wa huduma kwenye vituo vya
kutolea huduma za afya na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuunga mkono
na wananchi kuendelea kuchukua tahadhari.
Naye
Mratibu wa Mpango wa kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Corona Dkt. Khamis
Kulemba amesema msaada wa vifaa kinga, mafuta na gari kwa ajili ya kutoa elimu
ni muhimu sana kwa kipindi hiki, ambapo amebainisha kuwa wataalam wa afya
watashirikiana na Shirika hilo kuhakikisha elimu ya tahadhari ya Corona
inawafikia wananchi na vifaa kutumika ipasavyo.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto)akipokea msaada wa vifaa kinga(viambukuzi) kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona, kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Doctors with Africa CUAMM uliowasilishwa na Bi. Bi.Barbara Andreuzizi, Mei 06, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaada wa vifaa kinga(viambukuzi) kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona, kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Doctors with Africa CUAMM uliowasilishwa na Bi. Bi.Barbara Andreuzizi, Mei 06, 2020 Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange akizungumza kabla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa kinga( viambukuzi) kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona vilivyotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la Doctors with Africa CUAMM kwa mkoa wa Simiyu na kukabidhiwa kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na Bi.Barbara Andreuzizi, Mei 06, 2020 Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mpango wa kukabiliana na Corona Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba akizungumza kabla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa kinga( viambukuzi) kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya Virusi vya Corona, vilivyotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la Doctors with Africa CUAMM; kati ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na Bi. Barbara Andreuzizi, Mei 06, 2020 Mjini Bariadi.
Vifaa
kinga(viambukuzi) vilivyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la CUAMM kwa
mkoa wa Simiyu katika kukabiliana na
maambukizi ya Virusi vya Corona.
0 comments:
Post a Comment