Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ametoa wito
kwa Taasisi, mashirika ya Umma na binafsi na wadau wote wa kilimo, mifugo na
uvuvi wanaotarajia kushiriki maonesho ya Kitaifa ya Nanenane mwaka huu kuanza
maandalizi ya maonesho hayo.
Sagini ameyasema hayo jana mara baada ya kukagua na kuona hali ya maandalizi ya maonesho hayo katika
Viwanja vya Nyakabindi katika maeneo ya wadau mbalimbali wa maonesho
hayo.ambayo yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika Kanda ya Ziwa Mashariki Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
“Halmashauri za mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambayo ndiyo inaunda Kanda ya Ziwa Mashariki
zimeanza vizuri, taasisi zilizo chini ya
Wizara ya kilimo nazo zimefanya vizuri lakini baadhi ya wadau wa sekta ya
kilimo hawajajitokeza; nitoe wito kwa wadau wote watakaoshiriki katika maonesho
ya Nanenane Kitaifa mwaka huu mkoani Simiyu waweze kuja kuanza maandalizi,”
alisema Sagini.
Amesema maandalizi ya vipando vya mazao, mashamba darasa,
mabanda ya mifugo na mabwawa ya samaki yanahitaji muda hivyo ni vema wakaanza
mapema ili kupata vitu vizuri vitakavyotumika kuelimisha wakulima, wafugaji na
wavuvi kuhusu teknolojia rahisi zinazotumika katika uzalishaji wenye tija.
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo,
Bw. Nyasebwa Chimagu amesema
ameridhishwa na maandalizi ya maonesho ya nane nane huku akiwataka wadau
kuyatumia kama kichecheo kikubwa cha ueneaji wa technolojia za kisasa katika
sekta ya kilimo, mifugo na uvivu ili mazao yao yaweze kuwa na tija.
Pamoja na kukiri kuwa hamasa ya maandalizi ya maonesho ya
Nanenane mwaka 2020 ilishuka baada ya kuibuka kwa homa kali ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya corona, Chimagu amesema kuwa kwa sasa maandalizi
yanaendelea katika viwanja vyote nane vya kanda za maonesho hayo nchi nzima.
Aidha Chimagu amewatoa hofu wananchi wote juu ya
sintofahamu ya maonesho ya nane nane na kusema kuwa yatakuwepo na kuwasisitiza
wadau ambao hawajajitokeza kujitokeza kwenye viwanja vya maonesho kwa ajili ya
kuanza shughuli za maandalizi kwani tayari wengine wameanza na maendeleo ni
mazuri.
"Niwatoe hofu wananchi wote nchini kuwa maonesho ya
nanenane yatakuwepo kwenye viwanja vyote vya kanda, kitaifa yatafanyika mkoani Simiyu kwa mara ya
tatu mfululizo, hivyo wadau binafsi, taasisi za umma na binafsi pamoja na
halmashauri ambazo bado hazijaanza maandalizi kuanza shughuli za maandalizi ya maonesho, "alisema Chimagu.
Kwa upande wake Bwana shamba kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Ishengoma Julius amesema maandalizi ya vipando kwa ajili ya
maonesho ya nane nane yamefikia 75% na vipando vya muda mfupi vimebaki
kwa 25% na kusema kuwa mpaka kufikia maonesho hayo vitakuwa tayari.
Naye mkuu wa kambi ya jeshi la magereza kwenye maonesho ya nane
nane Nyakabindi, Bw. Patrick Matiku amesema wanafanya ukaguzi kila siku kwenye
vipando vyao ili waweza kubaini kama kuna tatizo na kulitatua mapema.
Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 yanaongozwa na Kauli Mbiu
inayosema “KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”.
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mbele)
akiwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa waSimiyu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa
Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto)
akiwa na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo, Bw.
Nyasebwa Chimagu na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya
Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda
ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) na
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo, Bw. Nyasebwa
Chimagu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo
mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa
Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mbele) akiwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mbele) akiwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akiwa na baadhi ya viongozi na watendaji wa Wizara ya kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa waSimiyu wakiangalia mche wa mkorosho ulipandwa viwanja vya nanenane Simiyu wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia)
akiwa na Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo, Bw.
Nyasebwa Chimagu wakikagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane
Kitaifa ambayo mwaka 2020 yatafanyika kwa mara ya tatu mfululizo katika kanda
ya ziwa Mashariki Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu.
:-Mapapai yaliyopandwa katika
vibando vya mazao ya kilimo katika viwanja vya nanenane Nyakabindi
Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo,
Bw. Nyasebwa Chimagu akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara
baada ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka
2020 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mkurugenzi wa maendeleo ya mazao kutoka wizara ya kilimo,
Bw. Nyasebwa Chimagu akiangalia mazao yaliyopandwa katika vipando kwenye uwanja
wa maoenesho ya nanenane wakati wa kukagua
maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020 katika
Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Mkuu wa kambi ya jeshi la magereza kwenye maonesho ya nane nane
Nyakabindi, Bw. Patrick Matiku(kulia) akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini zawadi ya papai ambayo yamepandwa katika vipando vya
jeshi hilo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2020 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
0 comments:
Post a Comment