Mratibu wa Wakala
wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon
Msomba amesema Serikali imedhamiria kufungua barabara zote zilizoharibiwa na
mvua mkoani hapa na kuhakikisha zinapitika kwa mwaka mzima ili kuwarahisisha
wananchi mawasiliano na usafirishaji wa
bidhaa na mazao mbalimbali.
Dkt. Msomba
ameyasema hayo Mei 13, 2020 wakati wa ziara yake ya kukagau maendeleo ya ujenzi
wa madaraja katika wilaya ya Bariadi eneo la Mto Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na
Majahida litakalogharimu shilingi milioni 33 na daraja la Mto Nyambuli
linalounganisha kijiji cha Mwamondi na Lulai (Dutwa) litakalogharimu kiasi cha
shilingi milioni 25 yanayojengwa kwa mpango wa dharura.
“Azma
ya Serikali ni kuhakikisha barabara zote zinapitika kwa mwaka mzima,
tunaishukuru Serikali imetoa fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara mkoani
Simiyu, mwaka wa fedha 2019/2020 tulitenga bajeti ya shilingi bilioni tano, kufikia
Mei 13, 2020 tumepokea shilingi bilioni 4.23 sawa na asilimia 84; kwa hiyo barabara
zote zilizoathiriwa na mvua tuna uhakika wa kuzifungua,” alisema Mratibu wa
TARURA Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba.
Aidha,
Dkt. Msomba amesema TARURA itafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa
miradi yote ikiwemo ya dhararua
inatekelezwa kwa kiwango na kwa wakati ili barabara hizo ziweze kuwanufaisha
wananchi kiuchumi ambapo amebainisha kuwa TARURA Simiyu imeomba kiasi cha
shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kwa mpango wa
dharura.
Dkt.
Msomba amesema pamoja na ujenzi wa madaraja katika mwaka wa fedha 2019/2020 TARURA imejipanga kutengeneza mtandao wa
barabara wenye urefu wa kilometa 690 huku akiwataka Mameneja wa TARURA wa
wilaya kusimamia ubora wa kazi katika ujenzi huo na kuhakikisha kazi zote
zinakamilika kwa wakati.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru viongozi wa TARURA kwa namna
walivyochukua hatua madhubuti kuhakikisha madaraja yanatengenezwa na barabara
za vijijini zinapitika hususani kwenye kipindi cha mvua nyingi, huku akitoa rai
kwa viongozi hao kuwasimamia wakandarasi ili wafanye kazi kwa kuzingatia viwango
vya kitaalam na thamani ya fedha.
Naye
Diwani wa Kata ya Dutwa, Mhe.Mapolu Mkingwa amesema matengenezo ya daraja la Mto
Nyambuli linalounganisha kijiji cha Mwamondi na Lulai utaondoa adha iliyokuwa
ikiwapata wananchi kufika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Dutwa
na kurahisisha usafirishaji wa mazao kwa kuwa Mwamondi ndiyo ghala la chakula
kwa kata hiyo.
Wakizungumzia
ujenzi wa madaraja yaliyokuwa yamesombwa na maji kutokana na mvua wananchi wa
Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Kulwa
Nyanza, Lazaro Samwel na Magreth Magile wamesema baada ya daraja kukatika iliwalazimu
kutumia usafiri wa pikipiki na baiskeli
kutokana na eneo la mto Ndoba kutopitika kwa magari.
“Tulikuwa
tunapata shida kuvuka mto huu na mvua zinaponyesha tulikuwa tunalazimika
kutengeneza daraja la miti ili litusaidie kuvuka, tunaishukuru serikali
kuchukua hatua za kuanza kujenga daraja tunaomba likamilike mapema maana huku
kuna wananchi wengi na vile vile kuna chuo cha maendeleo ya jamii,” alisema
Lazaro Samwel.
Wakala wa Barabara
za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu unahudumia mtandao wa barabara
wenye urefu wa kilometa 4038.16 ambapo kati ya hizo asilimia 55 zinapitika na
ziko katika hali nzuri na wastani, huku asilimia 45 ya mtandao zinahitaji
matengenezo na jitihada zinafanyika ili zifanyiwe matengenezo kuhakikisha
zinapitika kwa mwaka mzima.
MWISHO
Ujenzi wa daraja katika eneo la Mto Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi ukiendelea ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020 kupitia fedha za mpango wa dharura.
Ujenzi wa daraja katika eneo la Mto Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi ukiendelea ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020 kupitia fedha za mpango wa dharura.
Ujenzi
wa daraja la Mto Nyambuli linalounganisha kijiji cha Mwamondi na Lulai katika
kata ya Dutwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ukiendelea ambao ambao
unatarajia kukamilika Mei 15, 2020 kupitia fedha za mpango wa dharura.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) Mei 13, 2020 mjini Bariadi juu ya kazi mbalimbali zilizofanywa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu.
Diwani wa Kata ya Dutwa, Mhe.Mapolu Mkingwa akizungumza akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) Mei 13, 2020 wakati wa zaira ya Matibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon Msomba.
Lazaro Samwel mkazi wa Mtaa wa Bunamhala katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi akizungumzia ujenzi wa daraja katika eneo la Mto Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida ukiendelea ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020.
Magreth Magile mkazi wa Mtaa wa Bunamhala katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi akizungumzia ujenzi wa daraja katika eneo la Mto Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na Majahida ukiendelea ambao unatarajia kukamilika Mei 15, 2020.
Mratibu
wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Eng. Philemon
Msomba akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja katika eneo la Mto Ndoba linalounganisha Mtaa wa Bunamhala na
Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mei 13, 2020 ambalo linajengwa
kupitia fedha za mpango wa dharura.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) Mei 13, 2020 mjini Bariadi juu ya kazi mbalimbali zilizofanywa na Wakala
wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Simiyu.
0 comments:
Post a Comment