Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
amewakabidhi pikipiki Maafisa Tarafa 15 wa Mkoa huo ambazo ni utekelezaji wa
ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
aliyoitoa mwezi Mei 2019 wakati alipokutana na Maafisa tarafa wote nchini katika
kikao kazi jijini Dar es Salaam.
Akiwakabidhi
pikipiki hizo Mei 08, 2020 Mjini Bariadi Sagini amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa
pikipiki hizo zitakazorahisisha utekelezaji wa majukumu ya Maafisa tarafa huku
akiwaagiza kuzitunza na kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa; ikiwa ni pamoja
na kufuatilia mkakati wa elimu wa Mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kusoma wakiwa
katika likizo ya dharura ya tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Tumeandaa
mkakati wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi
kusoma kipindi ambacho wako likizo ikiwa ni tahadhari ya maambukizi ya Virusi
vya Corona; moja ya majukumu yenu katika kipindi hiki ni kuhakikisha mkakati
unatekelezwa kwenye maeneo yenu ya utawala; walimu, maafisa elimu watatimiza
wajibu wao nanyi pia mna sehemu yenu,”alisema Sagini.
Aidha, Sagini amewataka maafisa tarafa hao kuzitumia pikipiki
hizi kwa kuwafikia wananchi wote wakiwemo wakulima hasa kipindi hiki cha mavuno
na lengo kuu likiwa ni kuwaasa kutunza chakula.
Awali akisoma taarifa katibu tawala msaidizi utawalana
rasilimaliwatu katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu amewataka
maafisa tarafa hao kuzitumia pikipiki hizo kwa madhumuni yaliyokusudiwa ikiwa
ni pamoja na kusukuma shughuli za maendeleo ya jamii ikiwemo kusimamia
miradi ya elimu ,afya kilimo na hifadhi ya mazingira.
Wakati huo huo Mujungu ametoa maelekezo kwa makatibu tawala wa
wilaya mkoani Simiyu kutenga fedha kwa ajili ya mafuta na matengenezo ya
pikipiki hizo kwa kila tarafa ili pikipiki hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Akiongea kwa niaba ya maafisa tarafa mara baada ya kukabidhiwa
pikipiki hizo afisa tarafa ya Dutwa , Isabela Nyaulingo
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kuwawezesha kupata usafiri huo ambao utarahisisha utendaji kazi
wao huku akiahidi kuwa watazitunza na kufuata maelekezo yote waliyopewa na
viongozi.
Jumla ya pikipiki 15 zimekabidhiwa kwa maafisa tarafa mkoani hapa
zikiwa na thamani ya shilingi milioni 33,285,000/=, ambapo pikipiki moja inagharimu kiasi cha shilingi
milioni 2,219,000.
Tarafa zilizonufaika mkoani Simiyu ni Dutwa, Nkololo na Muhango(BARIADI),
Kivukoni na Busega(BUSEGA), Itilima, Kanadi, Bumela na Kinang'weli (ITILIMA) Mwagala,Sengerema,na
Nung'hu( MASWA), Kisesa Nyalanja na Kimali (MEATU).
MWISHO
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimkabidhi kofia Afisa Tarafa wa
Dutwa, wilayani Bariadi Bi. Isabela Nyaulingo ikiwa ni ishara ya kumkabidhi
pikipiki katika tukio la makabidhiano ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa
Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimkabidhi ufunguo Afisa Tarafa wa Tarafa ya Busega, Bw. David Pallangyo wilayani Busega ikiwa ni ishara ya kumkabidhi pikipiki katika tukio la makabidhiano ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Bw. Ekwabi Mujungu akiwasilisha taarifa ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kwa maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mwenye suti nyeusi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Tarafa wa mkoa huo mara baada ya kuwakabidhi pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kwa maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu(kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mwenye suti kulia) akizungumza na Maafisa Tarafa wa mkoa huo kabla ya kuwakabidhi pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kwa maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu.
Afisa Tarafa wa tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi, Bw. Rashid Zongo akimuonesha kitu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) mara baada ya Katibu Tawala wa Mkoa kuwakabidhi maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo zimekabidhiwa rasmi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Mei 08, 2020 Mjini Bariadi kwa maafisa tarafa wa mkoa wa Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (mwenye suti nyeusi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na Maafisa Tarafa wa mkoa huo mara baada ya kuwakabidhi maafisa tarafa pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo alizikabidhi Mei 08, 2020 Mjini Bariadi kwa maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimkabidhi ufunguo Afisa Tarafa wa Tarafa ya Busega, Bw. David Pallangyo wilayani Busega ikiwa ni ishara ya kumkabidhi pikipiki katika tukio la makabidhiano ya pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.
Afisa Tarafa wa tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi, Bw. Rashid Zongo akimuonesha kitu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) mara baada ya Katibu Tawala wa Mkoa kuwakabidhi maafisa tarafa wote wa mkoa wa Simiyu pikipiki zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa nchini ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.
Afisa Tarafa wa Tarafa ya Busega, Bw. David Pallangyo wilayani Busega (kulia) akishukuru mara baada ya kukabidhiwa pikipiki na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ambazo zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Maafisa Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimkabidhi kofia Afisa
Tarafa wa Dutwa, wilayani Bariadi Bi. Isabela Nyaulingo ikiwa ni ishara ya
kumkabidhi pikipiki katika tukio la makabidhiano ya pikipiki zilizotolewa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa
Maafisa Tarafa ambazo zimekabidhiwa Mei 08, 2020 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment