Mkoa wa Simiyu umezindua mpango
mkakati wa kuwawezesha wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kusoma katika
kipindi hiki cha likizo ya dharula ya tahadhari ya ugonjwa wa
homa ya mapafu ( COVID 19) inayosababishwa na Virusi vya Corona.
Akizindua mkakati huo, Mei 04, 2020
katika Shule ya Sekondari Simiyu Mjini Bariadi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa mkakati huo
utawasaidia wanafunzi kupata masomo wakiwa nyumbani kutoka kwa walimu wao huku
ukiwa na malengo makuu manne yatakayoifanya Simiyu iendelee kufanya vizuri katika
mitihani ya Taifa.
" Malengo makuu ya mkakati huu
ni kumwezesha mwanafunzi kuendelea kujifunza,walimu kuwa na mawasiliano ya
kitaaluma na wanafunzi wao, wazazi kufanya ufuatiliaji wa taaluma kwa
watoto wao pamoja na watoto(wanafunzi) kutulia nyumbani wakijisomea kipindi
hiki cha likizo ambayo wako nyumbani, tahadhari zote za maambukizi ya Virusi
vya Corona zitazingatiwa,"alisema Mtaka
Aidha, Mtaka amewataka wazazi na walezi
kuwahimiza wanafunzi kutulia nyumba kujisomea na kufuatilia vipindi vya
masomo mbalimbali vinavyorushwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini,
huku akisisitiza maelekezo yote yanayotolewa na wataalam wa afya na viongozi
juu ya tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona yazingatiwe wakati wa
kujisomea.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl
Ernest Hinju amesema Mkoa utaendelea kufanya mawasiliano na wazazi ili siku
tatu baada ya shule kufunguliwa wanafunzi wapewe mitihani ili kuwapima.
Katika hatua nyingine mbunge wa
jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge ametoa msaada wa kompyuta tano na printa
kwa Shule ya sekondari Simiyu kutoka mamlaka ya mawasiliano kwa wote ambazo
zimekabidhiwa na Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa, Christina Chenge (mke wa mbunge
huyo) kwa niaba ya mbunge.
Akikabidhi kompyuta hizo, Mama
Christina Chenge amesema mbunge ametoa
msaada huo na ametoa wito kuwa kompyuta hizo zitumike kwa kazi na malengo
yaliyokusudiwa ili mkoa wa Simiyu uendelee kufanya vizuri katika sekta ya
elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amemshukuru Mhe. Chenge kwa msaada huo na misaada mingine ambayo amekuwa
akiitoa kwa shule ya Sekondari Simiyu na shule nyingine ikiwemo saruji na
mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni na kusisitiza msaada huo
kutumika kama ulivyokusudiwa.
Akiongea mara baada ya makabidhiano
ya msaada huo, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema kuwa
hategemei kuona shule hiyo (Simiyu sekondari) iliyokabidhiwa vifaa hivyo kupata
wanafunzi wenye daraja sifuri kwani tayari wana walimu na vifaa vya
kutosha sambamba na madarasa ya kutosha.
Naye mkuu wa shule ya sekondari Simiyu,
Paul Susu amemshukuru Mhe. Chenge kwa kutambua uhitaji walionao kwani
utawasaidia katika kutekeleza shughuli zao za ufundishaji huku akiongeza kuwa
pamoja na kuwa shule ya Simiyu ndio imekabidhiwa shule nyingine zitanufaika pia
kwa kuwa wanafanya kazi kwa ushirikiano na shule nyingine.
Nao baadhi ya walimu wa shule hiyo
akiwemo Dorine Bella na John Mogela wamesema kuwa ujio wa kompyuta hizo
utakuwa chachu ya kurahisisha ufundishaji na kutekeleza mkakati wa mkoa wa wanafunzi
kusoma katika kipindi hiki cha ugonjwa wa homa ya mapafu na baada ya ugonjwa
huo.
MWISHO.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji wa idara ya
elimu katika uzinduzi wa mkakati maalum wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea
wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya
Corona, ambao umezinduliwa Mei 04, 2020 katika shule ya Sekondari Simiyu Mjini
Bariadi sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge. Mke wa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge, Mama Christina Chenge (wa pili kulia) akikabidhi moja ya kompyuta tano na printa zilizotolewa na Mbunge huyo kwa Shule ya Sekondari Simiyu, kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwl Paul Susu akipokea msaada huo Mei 04, 2020; kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Juliana Mahongo.
Mke wa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge, Mama Christina Chenge (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mara baada ya kukabidhi msaada wa kompyuta tano na printa moja kwaShule ya sekondari Simiyu kwa niaba ya Mbunge huyo, Mei 04, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akimkabidhi Afisa Elimu Halmashauri ya Mji wa Bariadi nakala ya mkakati wa maalum wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, ambao umezinduliwa Mei 04, 2020 katika shule ya Sekondari Simiyu Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu,Mwl. Ernest Hinju akitoa maelezo juu ya mkakati maalum wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, ambao umezinduliwa Mei 04, 2020 katika shule ya Sekondari Simiyu Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mbele) akiwaongoza baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali katika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mabweni katika Shule ya Sekodari Simiyu mjini Bariadi mara baada ya uzinduzi wa mkakati maalum wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, Mei 04, 2020 Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Mke wa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge, Mama Christina Chenge (kulia) akizungumza na viongozi na baadhi ya walimu mara baada ya kukabidhi kompyuta tano na printa zilizotolewa na Mbunge huyo kwa Shule ya Sekondari Simiyu, msaada huo ulikabidhiwa Mei 04, 2020 wakati wa uzinduzi wa mkakati maalum wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkakati maalum wa mkoa wa Simiyu wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, Mei 04, 2020 Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Diwani wa Kata ya Malambo, Mhe. Kitebo Kitebo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkakati maalum wa mkoa wa Simiyu wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, Mei 04, 2020 Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Juliana Mahongo akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari Simiyu Mjiini Bariadi moja ya kompyuta zilizotolewa na Mbunge wa Bariadi Mhe. Andrew Chenge kwa Shue hiyo, Mei 04, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mbele) akiwaongoza baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali katika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekodari Simiyu mjini Bariadi mara baada ya uzinduzi wa mkakati maalum wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, Mei 04, 2020 Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Shule ya sekondari Simiyu, Mwl.
Paul Susu na Afisa Elimu wa Mkoa, Mwl. Ernest Hinju wakiteta jambo mara baada
ya uzinduzi wa mkakati maalum wa mkoa wa
Simiyu wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari
dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, Mei 04, 2020 Mjini Bariadi uzinduzi
huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka
kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Baadhi ya madarasa
katika shule ya sekondari SimiyuMkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mbele) akiwaongoza baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali katika ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa mabweni katika Shule ya Sekodari Simiyu mjini Bariadi mara baada ya uzinduzi wa mkakati maalum wa mkoa wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, Mei 04, 2020 Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji wa idara ya
elimu katika uzinduzi wa mkakati maalum wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea
wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya
Corona, ambao umezinduliwa Mei 04, 2020 katika shule ya Sekondari Simiyu Mjini
Bariadi sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.
0 comments:
Post a Comment