Friday, February 11, 2022

Mkoa wa Simiyu Waongoza- Utoaji Chanjo Covid -19 Kwa wiki mbili mfululizo.

Kwa wiki mbili mfululizo Mkoa wa Simiyu umechanja wananchi wengi zaidi kuliko Mikoa mingine yote Nchini ( Tanzania Bara na Visiwani). 

Hii ni kutokana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ( Covid Vaccination National Score Card ya 07/02/2022) ambapo kwa siku utoaji chanjo umekuwa ukifanyika kwa wastani wa asilimia 131 na kupelekea Mkoa wa Simiyu kutajwa kuwa Mkoa unaofanya vizuri sana ( High Performance region) kati ya mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Zanzibar. 

“Niwashukuru viongozi wote kwa ushirikiano. Changamoto iko katika dose  ya pili ambapo tupo chini ya 50%.Lakini tumeweka mikakati ya kuhakikisha wananchi wote wanaotakiwa kufikiwa na watoa huduma ili kupata dose ya pili wanafikiwa.Tukisimamia hili ni dhahiri tutakuwa katika kiwango kizuri sana cha uchanjaji”. Amesema Kafulila.

Mkoa wa Simiyu umekuwa ukitoa chanjo kati ya  3500 hadi 7000 kwa siku. Hizi takwimu ni kuanzia tarehe 01.02.2022 hadi 09.02.2022.

Hongera sana Viongozi ngazi za Wilaya, wataalam, wa afya  na wadau wa maendeleo kwa ushirikiano na kwa kazi nzuri






Wananchi wa Simiyu wakisubiri na kupata Chanjo ya Uviko -19

Kazi iendelee.👏👏👏

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!