Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu, Mhe. David Kafulila ameyasema hayo wakati wa kikao cha tathimini ya Matokeo ya Mitihani ya Taifa ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha Sita,2021 kilichofanyika hivi karibuni, Bariadi.
Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa amewapongeza viongozi wote, wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Elimu,Wathibiti ubora,walimu na wanataaluma wote kwa kuendelea kuchapa kazi licha ya changamoto na mabadiliko mbalimbali ambayo yametokea katika Idara ya elimu. “Pamoja na kwamba tuna changamoto kubwa ya mabweni, chakula kwa wanafunzi, suala la elimu ni agenda kubwa ndani ya nchi na hasa ndani ya mkoa wetu wa Simiyu .Mkiwa viongozi na wakuu wa Serikali kwenye maeneo yenu lazima kuweka nguvu na tumieni kila aina ya uwezo na maarifa ili kuhakikisha kwamba mnafanya vizuri. Pamoja na kushindana Halmashauri na Halmashauri hakikisheni kwamba mnashindana na kushinda kitaifa. Wakurugenzi, licha ya kufanya vizuri kwenye mapato na kutumia muda wenu kuhakikisha kuwa makusanyo yanaongezeka, jicho katika sekta ya elimu linapaswa kuwa la kipekee,hakikisheni kwamba waalimu na mazingira yao yanazingatiwa kwenye mipango yetu”.Amesisitiza Kafulila.
Nae, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bi. Prisca Kayombo, amewapongeza Walimu kwa kazi nzuri na kuahidi kuwatembelea huko waliko ili aweze kujua kwa undani kiini cha changamoto ambazo wanakabiliana nazo.“Ninaelewa kwamba kuna changamoto kubwa ya nyumba za Walimu, matundu ya vyoo na mazingira magumu ya kazi, ambayo naahidi kuyafanyia kazi”.Amesema Bi. Kayombo.
Akizungumza, Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu Bw. Majuto Njanga, ameeleza kuwa kikao cha Tathmini ya matokeo ya mitihani ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita , kimelenga katika kuangalia jinsi ya kufanikiwa zaidi Kielimu, kujadili changomoto ambazo tunakabiliana nazo na kujadili mikakati gani iwekwe kwa mwaka ujao wa masomo.
Aidha Mkuu wa Mkoa aliwataka maafisa elimu, wathibiti ubora,wakurugenzi, wakuu wa Wilaya kueleza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika maeneo yao. Nyingi ya changamoto zilizoelezwa ni pamoja na utoro wa wanafunzi ,wanafunzi wengi hupewa kazi na wazazi wao, ambapo kati ya kazi hizo ni pamoja na kuuza vyakula mnadani au kuchunga ng'ombe,kuuzuza mifuko na kadhalila.Utoro wa baadhi ya walimu nao ulitajwa kama changomoto kwani baadhi ya walimu badala ya kufundisha madarasani hawaonekani shuleni na huku baadhi wakiendelea na shughuli zao binafsi. Aidha ,miundombinu baadhi ya maeneo yana changamoto za matundu ya vyoo kwa wanafunzi na waalimu,ukosefu wa nyumba za walimu, umbali wa maeneo ya shule kwa baadhi ya wanafunzi.Changamoto kubwa ya chakula mashuleni, kuna uhusiano wa karibu kati ya chakula na ufanisi wa wanafunzi shuleni.Ukosefu wa umakini kwa baadhi ya waalimu,Ukosefu wa motisha kwa walimu na baadhi ya shule kukosa madawati na hivyo wanafunzi kukaa chini.
Ili kukabiliana na changamoto hizo, viongozi hao kwa kushirikiana na Afisa elimu mkoa wamejipanga na kutaja mikakati mbalimbali,kwa mfano ili kukabiliana na changamoto ya utoro, viongozi hao wameona ni vyema kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto wao,kujenga mabweni kwa maeneo ambayo ni mbali na shule,kuboresha miundombinu.Afisa elimu kuhakikisha maoni na maelekezo yanayotolewa na mdhibiti ubora yanafanyiwa kazi kikamilifu. Mthibiti ubora kuboresha ripoti zake, ripoti ziusishe taarifa za utendaji kazi na si miundombinu tu. Wanafunzi ambao hawana uwezo wasiruhusiwe kwenda darasa la mbele zaidi.Kuwa na vikao vya mara kwa mara na wazazi na kufanya kazi kwa ukaribu zaidi na maafisa ngazi ya kata.
Akifunga kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, aliwahimiza wakurugenzi kuwa wabunifu zaidi na kutumia fursa mbalimbali zikiwemo kuwatumia wadau wa maendeleo kutatua changamoto mbalimbali kama matundu ya choo na nyumba za walimu, aidha Mhe. Kafulila aliwataka wakurugenzi hao kuwamotisha walimu wanaofanya vizuri.
“Kuna namna nyingi ambazo mnaweza kufanya kwa mfano mapato ya madini mnaweza kuangalia jinsi gani mapato hayo mnaweza kuyaelekeza kwenye elimu. Kama viongozi zipo njia mbalimbaai ambazo mnaweza kufanya na kubadilisha maisha ya watu wetu.Lazima tufikiri nje ya bajeti za Halmashauri. Leo tupo mwezi Februari ikifika Juni.Sitegemei kuona mtoto yeyote anakaa chini mkoa wa Simiyu”.Amesisitiza Kafulila.
Mwisho
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na wadau wa Elimu Mkoani Simiyu
|
Washiriki wa kikao cha tathmini |
|
Afisa elimuMkoa wa Simiyu Bw. Majuto Njanga akieleza madhumuni ya kikao cha Tathimini |
|
Mhe. David Kafulila akisisiyiza jambo |
|
Washiriki wa kikao cha Tathimini |
|
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Faidha Seleman akichangia hoja |
|
Wakuu wa baadhi ya Wilaya za mkoa wa Simiyu |
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza, aliyeketi Afisa Elimu mkoa wa Simiyu Bw. Majuto Ngaja |
|
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe. Fauzia Hamidu |
|
Kushoto Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila |
|
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe.Gabriel Zakaria akichangia hoja |
|
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge akichangia jambo |
|
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama |
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza pembeni yake aliyeketi ni Afisa Elimu Mkoawa Simiyu Bw. Majuto Njanga
|
0 comments:
Post a Comment