Thursday, February 17, 2022

Tumieni Wakandarasi na Watoa Huduma Kutoka Simiyu- RC Kafulilla

Mhe. Kafulila ameyasema hayo hivi karibuni akiwa ameambatana na kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na mkuu wa Wilaya ya Bariadi, wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA mkoani Simiyu. Mhe. Kafulila ametoa maelekezo hayo mara badaa ya kupokea taarifa kutoka kwa  Meneja mradi ambaye pia ni Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya jamii Buhnamala-Bariadi, Bw.Bazil Ngoloka, kuwa matofali ya ujenzi wa mradi huo yanasambazwa na mtoa huduma kutoka Mwanza anayejulikana kama Arm Strong Company Limited.

Akizungumzia mradi huo Bw.Ngoloka ameleza, mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA Mkoani Simiyu ulianza tarehe 26.01.2022 kwa kazi ya awali na kazi rasmi ilianza 07/02/2022 kazi ambayo inatarajiwa kukamilika mara ifikapo 30/6/2022. Mradi huu unasimamiwa na chuo cha ufundi Arusha.

Ujenzi wa chuo cha VETA Simiyu,utagharimu kiasi cha Tsh.5,150,731,187.10,ambazo zitatumika kujenja, mabweni manne , mawili yakiwa ya kike na mawili ya kiume, majengo ya idara tisa,majengo ya utawala na huduma zinginezo 7 pamoja  na nyumba za waalimu 4. “Kwa ujumla hatua ya utekelezaji hadi sasa zimefikia hatua ya uchimbaji wa Msingi majengo kwenye kila lot na umwagaji zege kwenye baadhi ya majengo. Kiasi cha fedha zilizotumika hadi sasa  ni Tsh. 7.89 ml.’’Amesema Ngoloka.

Pamoja na mafaniko hayo Bw. Ngoloka, ametaja kukabialina na changamoto za ubovu wa barabara hasa kipindi hiki cha mvua na ongezeko la  bei za vifaa vya ujenzi kama nondo na hivyo kupelela kurudia mchakato wa manunuzi ili kupata bei halisi ya soko. 

Aidha, Mhe Kafulila aliwataka wajumbe wa kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na mkuu wa Wilaya ya Bariadi kutoa maoni yao kuhusiana na mradi wa ujenzi huo, ambapo  Mkuu wa wilaya ya Bariadi Mhe.Lupakisyo Kapange alisisitiza umuhimu wa kutumia vijana wa Bariadi kufanya kazi za ujenzi katika mradi huo,badala ya kutumia vijana kutoka maeneo mengine na hasa mje ya mkoa wa Simiyu,labda iwe  tu kwa fani ambazo zinahitaji utaalamu maaluum,kwani mradi huo unategemewa kuongeza ajira kwa wakazi wa Baridi.

Aidha Mhe.Kapange aliahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali  kwa Meneja wa mradi huo na kuhakikisha anapata rasilimali watu katika kamati mbalimbali za ujenzi, wanakamati ambao watatokana na uwezo wao kama ilivyoelekezwa na mkuu wa Mkoa.

Wajumbe wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walisistiza, suala la  Usalama wa Vifaa vya ujenzi katika eneo la ujenzi na mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.Aidha wajumbe walikumbusha suala laupatikanaji wa Umeme ili kazi ziweze kufanyika kwa masaa 24 (usiku na Mchana) pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.

Ili kuhakikisha kuwa ujenzi huo unafanyika kwa viwango na kwa wakati Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe. David Kafulila alitoa maelekezo kwa Mamlaka ya Bonde kuja kufanya uchunguzi ili kujua maji yanapatikana wapi katika eneo husika na hatimaye Meneja mradi kuhakikisha kuwa wanachimba kisima,ambacho kitatumika wakati wa mradi wa ujenzi na baada ya mradi. Vilevile Mkuu wa Mkoa aliwaagiza TANESCO kuhakikisha kuwa kufikia ijumaa umeme uwe unapatikana katika eneo husika.

Aidha Mhe. Kafulila aliagiza kamati za ujenzi ziangaliwe upya na Mkuu wa Wilaya  pamoja na Mkurugenzi wasaidie upatikanaji wa rasilimali watu ambao watafanya kazi katika kamati mbaliambali. Mhe. Kafulila alisistiza kuwa upatikanaji wa rasilimali watu hao uwe kulingana na uwezo na si kwa majina.

Katika hatua hiyo hiyo Mhe. Kafulila alitoa maelekezo ya kuwasimamisha kazi  watoa huduma wote wanaotoka nje ya mkoa wa Simyu, labda iwe kwa maelekezo maalum au kwa watoa huduma wanatoa huduma za moja kwa moja kutoka kiwandani kama vile kiwanda cha nondo au Sementi, kwani kwa kufanya hivyo kutaokoa muda, kutapunguza gharama, kutaongeza mauzo, kupato na ajira kwa wananchi wa Simiyu.Mwisho.























 

 

 

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!