Tuesday, February 22, 2022

Serikali kukifufua Kiwanda Cha Kuchambua Pamba cha Sola Wilayani Maswa

MKUU  wa Mkoa Simiyu, David Kafulila ametaka kujua hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi ya Askari,Nuru Mtafya anaetuhumiwa kumpa ujauzito Mwanafunzi anayejulikana kwa jina la Neema Mabula wa shule ya Sekondari iliyopo wilayani Maswa mkoani humo.

Uamuzi huo umefikiwa na RC Kafulila mara baada ya mzazi wa mtoto huyo Mabula Masanja Manyanda mkazi wa kijiji cha Njiapanda kulalamika mbele ya Mkuu huyo wa Mkoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana na wananchi kutoa malalamiko yao.

Akitoa malalamiko yake amesema baada ya askari huyo ambaye alikuwa ni Askari wa Usalama Barabarani katika kituo cha polisi Malampaka kumpatia ujauzito binti yake alihamishwa na kupelekwa kituo cha polisi Maswa.

Aliendelea kueleza kuwa aliendelea kufuatia suala hilo kwa ukaribu hadi kwa Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu lakini amekuwa akipigwa danadana.

Akijibu malalamiko hayo,Rc Kafulila pamoja na kumpatia pole Mzazi huyo alimwagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu ACP.B.Z. Chatanda, kupata taarifa ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya askari huyo katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kitakachofanyika juma lijalo huku akisisitiza hakuna mtu aliye juu ya sheria.




" Pole sana mzazi. Naagiza RPC suala hili ulilete kwenye kikao cha Kamati ya Usalama wiki ijayo ili nijue kama kweli mmefanyia kazi kikamilifu kwani hakuna aliyejuu ya sheria haijalishi ni Polisi, Mwalimu au Hakimu na hata nikiwa mimi RC"alisema.Mwisho

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!