Monday, March 7, 2022

Katika Kusherehekea siku ya wanawake Duniani Malkia wa Taarabu Nchini Bi Khadija Kopa Azikonga Nyoyo za wanawake wa Simiyu





















 

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani Mkoa wa Simiyu umeendaa ‘Simiyu Women Gala’, ambayo imeanyika jana katika ukumbi wa Bariadi Confere Centre uliopo Bariadi ambayo pia ndio makao Makuu ya Mkoa wa Simiyu. 

 Akizungumzia kusudi la hafla hiyo Makamu mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya halfa hiyo  Bi.Mariam Mwanzamila, ambaye pia ni Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Simiyu, amesema kusudi la halfa hii ni Kufahamiana na kujenga  umoja baina ya wanawake wa Simiyu na Mikoa jirani. Aidha pamoja na hafla hiyo Kamishna Msaidizi Mwanzamila ameeleza kuwa mada mbalimbali zenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya biashara, uwekezaji na mahusiano zitawasilishwa na Manguli wenye uzoefu katika nyanja hizo. Watoa mada kutoka Benki ya TCB, Auntie Sadaka , Mbunge wa Viti maalum DSM Mhe.Janeth Elias Mahawanga pamoja na Malkia wa Taarabu Bi. Khadija Kopa walitoa mada ambazo ziliwanufaisha wanawake/ Wadada hao. 

Sanjali na halfa hiyo “wakina mama wa Mkoa wa Simiyu wamenunua madaftari na peni 1000,zenye thamani ya Tsh.2,500,000/-, ambazo watazigawa kwa wanafunzi kwenye shule zenye mahitaji maalum katika Wilaya zote Tano za Mkoa wa Simiyu”.Amesema Mhe.Faiza Salim,Mkuu wa Wilaya ya Itilima.

Aidha, Mgeni rasmi katika halfa hiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila, ambaye pamoja na kuwapongeza wanawake kwa kuandaa halfa hiyo ambayo mbali na kufurahi pamoja inawajengea uwezo wanawake katika masuala ya ujasiliamali. Mhe.Kafula alisisitiza umuhimu wa kuwa na malengo na kuvuka kutoka hatua moja kwenda hatua ingine.Mhe.Kafulila amewatia moyo Wanawake kuwa  wanaweza kwani tafiti za kimataifa zinaonyesha kuwa kuna tofauti kati ya matumizi ya kipato kati ya mwanaume na mwanamke,kwani 90% ya kipato cha Mwanamke hurudi nyumbani wakati kwa wanaume 35% tu ndio hurudi nyumbani. Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!