Tuesday, March 1, 2022

Kilimo cha Pamba Kuvunja rekodi 2022, shukrani kwa Kuitangaza Pamba- RC Kafulila


Mhe.Kafulila ameyasema hayo na kutoa Shukrani hizo hivi karibuni wakati akiongea na Waandishi wa Habari."Hamasa  yeyote kuhusu zao la  Pamba Kwa wasukuma huwafanya waongeze uzalishaji".Amesema Kafulila.

Mkuu wa Mkoa huyo,aliwajuza wahariri hao kuwa, Katika Kilimo cha Pamba  tupo Katika hatua za upuliziaji   wa Dawa pamoja na palizi.

Mwaka huu tunategemea kuvunja rekodi, mwaka jana wakati tunaanza Kilimo cha Pamba,bei ya Pamba katika soko la Dunia ilianzia $ 0.78 na  kufikia $ 0.96. Mwaka huu mategemeo yetu bei hiyo katika soko la dunia itaanzia $ 1.00- $1.50 hivyo bei Pamba Katika soko la Dunia  itazidi ya mwaka Jana, tunategemea bei iende zaidi mara 3.

Vilevile tunategemea uzalishaji wa Pamba utaongezeka kuanzia  tani 81,000,mwaka jana na kufikia tani 250,000 mwaka huu na hivyo kuigiza takribani Tsh. 300 bln.

"Haya mafanikio yote kwa  sehemu kubwa ni sababu ya mchango wenu.Kwani kwa kuwahabarisha wananchi Kuhusu umuhimu wa zao la Pamba na kwa kutumia kalamu zenu wananchi  wamehamasika kulima Pamba zaidi ya ilivyokuwa awali. Niwashukuru sana kwa ushirikiano wenu".

Tunategemea Mavuno ya Pamba yataanza  mwezi wa nne na kuendelea.Njia nzuri zaidi ya  mauzo ya Pamba ni  kwa njia ya Benki. 

Mwaka huu tumelima hekari 1,364,000 za Pamba.Mategemeo yetu ni kuwa mara baada kuvuna Pamba tutaendelea na Kilimo cha  dengu.Kusudi ni kumsaidia Mkulima kutoka shamba lilelile apate kipato zaidi ya mara mbili.

Pamoja na Mkuu wa Mkoa   kusisitiza Kilimo cha Pamba,Waandishi hao walitaka kujua hali ya elimu Mkoani Simiyu, ambapo  Mhe.Kafulila aliwaeleza kuwa  "Tumefanya vizuri sana kielemu, matokea ya 2021, kidato cha nne tumekuwa wa tatu kitaifa.

Katika shule za Serikali tunafanya vizuri sana,kwani tumeongoza kitaifa Katika Mtihani wa Darasa la Saba Katika shule za Msingi za Serikali. Kati ya wasichana  kumi bora Kitaifa wasichana watano wametoka Mkoani Simiyu huku Msichana  wa kwanza akitokea Inonelwa Shule ya Msingi iliyopo Wilayani Meatu.

Aidha waandishi hao walitaka kujua mwitikio wa wanafunzi kuingia darasani ukoje baada ya ujenzi wa Madarasa ya UVIKO-19. Mhe.Kafulila aliwaeleza hali ya uingiaji madarasani katika Elimu ya awali ni 110%,Darasa la Kwaza ni 97% na  Kidato cha kwanza ni 93%.Kukiwa na baadhi ya maeneo yenye changamoto.

Aidha Mhe.Kafulila, aliwajuza waandishi  hao Kuhusu Maendeleo mazuri ambayo Serikali imepanga kufanya ili kufufua viwanda viwili vya Pamba ambavyo vitaanza kufanya Kazi Katika msimu huu wa Pamba.

“Tumeletewa chuo cha VETA kutokana  na fedha za UVIKO-19. Ukiangalaia Tanzania inafanya vizuri zaidi kuliko nchi zingine za EAC, ambazo zote zimepokea pesa za UVIKO-19”. Ameeleza Kafulila.

Waandishi hao walimshauri Mhe.Kafulila kufungua kiwanda cha nyama na mazao yake  kwani Mkoa  Wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa 3 nchini inayoongoza kwa ufugaji wa ng'ombe nchini.Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!