Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo ametembelea wilaya za mkoa wa Simiyu ambazo ni Wilaya ya Itilima na Wilaya ya Bariadi.
Akiwa Wilaya ya Itilima Jenerali Mabeyo alikabidhi madarasa 2, Ofisi Moja na vyoo matundu nane, yaliyojengwa na Meja Jenerali Paulo Kisesa kwa ushirikiano na Wanajeshi wenzake.Akiwa kwenye hafla hiyo Jenerali Mabeyo aliahidi kutoa kiasi cha Tsh. 30m ambazo zitatumika kukamilisha ujenzi wa baadhi ya Miundo mbinu pamoja na Ofisi ya waalimu.
Aidha Jenerali Mabeyo akiwa Wilaya ya Bariadi alitembelea Kata ya Matongo, Kijiji cha Matongo, na kuahidi kuchangia kiasi Tsh. 50m ambazo zitatumika kukamilisha ujenzi wa shule ya wasichana Matongo-Bariadi ambayo majengo yake yaliachwa tangu mwaka 2010 wakati Simiyu ikiwa sehemu ya Shinyanga.Mwisho.
0 comments:
Post a Comment