Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila hivi karibuni amezindua Bodi ya Parole, Mkoani Simiyu.Akizungumza na wajumbe wa Bodi wakati wa uzinduzi waBodi hiyo, Mhe. Kafulila amesema “ninyi mkiwa wajumbe wa Bodi mna wajibu wa kuamua kwa haki stahili zawafungwa.
Cha kukumbuka siku zote ni kuwa, Rais wetuMama Samia Suluhu Hassan, suala la haki lipo kwenyemoyo wake,mbali ya sheria ya nchi pamoja na katiba,suala la haki lipo kwenye moyo wa Mhe Rais. Hivyo nanyi mkiwa wasaidizi wake mnapaswa kuhakisi hiyo haki.Mpaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Hamad Masauni anawateua ninyi, mchakato mkubwaumepita,hivyo bila shaka mnauwezo na uzoefumkubwa,nanyi pia ni wenye haki’’.
Pitieni vizuri sheria zotezinazohusiana na kazi yenu ili mjue sheria na taratibuzinasema nini, ili mnapofanya maamuzi yawe maamuzi yahaki yanayozingatia, sheria, taratibu na kanuni.
Akizungumza Kamishna Msaidizi wa Magereza Simiyu,ACP.Huruma.E.Mwalyaje,ameeleza kuwa kuzinduliwa kwa Bodi ya Parole Mkoa wa Simiyu, ni mafanikio makubwa sana kwa mkoa, kwani hii ni bodi ya kwanza kuzinduliwa na kufanya kikao chake cha kwanza mkoani Simyu.Kabla ya hapo Mkoa wa Simiyu haukuwana Bodi yake ya Parole na hivyo kupelekea shughuli zote na maamuzi yote yanayohusu Magereza mkoa wa Simiyu, kufanywa na Bodi ya Parole ya Mkoa wa Shinyanga.
ACP.Mwalyaje ameeleza kuwa Bodi hiyo ina wajumbe watano ambapo kati yao wajumbe wanne ni wanaume na mmoja wa kike. Majina ya wajumbe hao ni Zongo Said ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi, Sheikh Mahmoud Salum Kalokola-mjumbe,Dkt. Phillips Mtiba-mjumbe, Bi.Margareth Magele-mjumbe na Mchungaji Marco Fabian Mringo- mjumbe.
Akizungumza mwenyekiti wa Bodi ya Parole Simiyu Bw. Zongo Said amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwazindulia Bodi na kwa ushauri aliowapatia wakusimamia haki nao wameahidi kuwa watazingatia hilo.Bw.Said amewataka wale wanaoanzisha masuala ya haki na stahili za wafungwa wawe makini na watende kwa haki ili wao kama watekelezaji,wasipotoshwe na hivyo kufanya maamuzi yanayozingatia haki,taratibu na sheria.Mwisho.
0 comments:
Post a Comment