Mhe. David Kafulila ameyasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa Pamba kilicholenga kujadili juu utekelezaji wa Mkakati wa Pamba ili kuongeza tija ya zao hilo kwa Kipindi cha Miaka miwili 2019-2022.
Akijibu hoja ya changamoto ya maafisa Ugani, Mhe.Kafulila ameelekeza, Halmshauri za Wilaya pamoja nahalmashauri za Pamba, zianze mara moja kuwatumia Wakulima wawezashaji ambao wapo wengi sana katika maeneo yao, kuwaelimisha Wakulima wa Kawaida, kanuni za kilimo bora cha Pamba.
“Kikubwa sisi Viongozi wote kuanzia ngazi za chini ni kuwa na nia ya kufanya makubwa, Kamati za Wilaya za Pamba endeleeni kutoa elimu kuhusu masuala ya Pamba hasa wakati huu ambao tunatumia hizi sumu za kukabaliana na wadudu wa Pamba . Nikweli kwamba kuna changamoto kubwa ya Maafisa Ugani, lakini pamoja na hayo tuna jeshi kubwa la Wakulima Wawezeshaji, hivyo tunaweza watumia Wakulima wawezeshaji ambao wanaweza kusaidia kutoa elimu kwa wakulima wakawaida, mara nyingi hawa wako tayari kujitolea na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa”. Amesema Kafulila.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila,ameishukuru kampuni ya GATSBY AFRICA kwa kazi nzuri ambayo wameifanya nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka 15 ,na kufanya kazi pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu kwa Kipindi cha Miaka 2 (2019-2022).“
“Yale yote mliyoyaanzisha tutayaendeleza na hasa makakati wa Pamba,kama kuna nyaraka ya kujivunia ni Mkakati wa Pamba,sisi kama mkoa tutayaishi na kuhakikisha kwamba tutafikia lengo la kuazalisha Pamba tani laki tano. Mwaka huu tunategemea kupata kilo 350 kwa heka, hii inaonyesha mwaka ujao katika eneo hilo hilo tunaweza pata hata mara tatu zaidi”. Amesisitiza Kafulila.
Wakizungumzia mafanikio ya Mkakati wa Pamba, Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe. Aswege Kaminyoge pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Faiza Salum, wameeleza kuwa elimu iliyotolewa na Balozi wa Pamba imewasaida sana wakulima, cha muhimu ni kuzingatia palizi na upuliziaji wa viua wadudu kwani Pamba inahitaji palizi za mara kwa mara.Pongezi sana kwa benki ya Azania, na tunategemea msimu ujao watakopesha hata zaidi.
“Niwashauri benki zingine kama CRDB, NMB na NBC, kama ambavyo wanawakopesha wakulima wa mazao mengine katika mikoa mingine, basi wawakopeshe pia wakulima wa pamba. Pongezi kwa wakulima wote kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na balozi wa Pamba” Amesema Kaminyoge.
Msimu ujao tutaendelea kutoa elimu ili wakulima wote wafuate kanuni za kilimo cha Pamba. Union na AMCOS, wabadilike maana wananchihawana imani nao. Kuna uhaba mkubwa wa maafisa ugani hivyo tunaomba, tupate maafisa ugani katika kila kijiji ili angalau kila kijiji kiwe na Afisa Ugani. Mhe.Faiza Salum,aliwapongeza wakulima wa Pamba wa Wilaya ya Itilima na amesisitiza kuwa ni vyema kukawa na ushirikiano mzuri kati ya SIMCU, Wanunuzi wa Pamba/Ginners, Halmashauri na bodi ya Pamba, kutakuwa hakuna haja kwa wakulima kukopa benki hivyo ni vyema taasisi hizo zikafanya kazi kwa ukaribu na kumsaidia Mkulima.
Akizungumza, Mkurugenzi wa GATSBY AFRICA Samweli Kilua, ameshukuru kwa ushirikiano mkubwa ambao wameupata mkoani Simiyu.Mkoani Simiyu, tumefika hatua ya mbali sana, maana si rahisi kwa wakulima wadogo kupata mikopo ya moja kwa moja kutoka Benki, lakini kwa Simiyu imewezekana. ChaMuhimu ni kuendelea kutoa elimu ili wakulima wengi zaidi waweze kunufaika na mikopo hiyo. Kukiwa na ushirikiano mzuri na wa karibu kati ya Mkulima na Wanunuzi wa Pamba/Ginnery, hii itasaida benki kuwa na uhakika wa kuwa Pamba itanunuliwa, na hivyo kuweka utaratibu wa kuwakopesha wakulima hao na kufanya malipo yote yafanyike kupitia benki, kwenye akaunti ambayo ilimkopesha mkulima na hivyo kuiwezesha benki hiyo kumkata mkulima deni moja kwa moja. “Tumetoa elimu juu ya kulipizia dawa kwa vijana 1500 ambao wamefundishwa kupiliza dawa na kujikinga. Hivyo tunapaswa kuwatumia, kwani sekta ya Pamba imetengeneza ajira.Tutumie wataalamu ili kudhibiti pembejeo na wadudu.Biashara za siku hizi zinahitaji ushirikiano, tumeshafanikiwa sana katika masuala ya mbegu”Amesisitiza Kilua.
Nae Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa Pamba Bwana Boaz Ogola ameeleza kuwa njia yenye mafanikio na matokeo chanya katika kuwaelimisha Wakulima wa Pamba ni kupitia Redio. “ Kwa Kutumia redio iliyopo Mkoani Simiyu, Baraidi FM umeweza kutoa elimu kwa wakulima wengi na mafanikio tunayaona kupitia upandaji Pamba unaozingatia kanuni za Pamba , kama matokeo tunatarajia kuvuna pamba nyingi sana msimu huu.
Akizungumzia faida za uwepo wa GATSBY AFRICA mkoani Simiyu,mshauri mwelekezi wa masuala ya Pamba Bw. Mirumbe Chacha, ameeleza kuwa wakati Gatbsy inaanza kazi Mkoani Simiyu, changamoto kubwa ilikuwa tija, mashamba ya Simiyu yalikuwa yakizalisha kilo 175 kwa hekari ila kwa sasa uzalishaji huo umepanda na kufikia kilo 350 kwa hekari. Wakulima wa Pambawameacha kuchangaya mazao kwenye mashamba yao ya pamba, kwa sasa zaidi ya 80% ya mashamba ya pamba tunaona Pamba tu. Akizungumzia Changamoto Bw.Mirumbe ameeleza kuwa changamoto kubwa ni Taasisi za Kifedha kushindwa kuwasaidia wakulima moja kwa moja. Kwa mara ya kwanza msimu huu benki imeweza kuwapatia wakuklima fedha ya kulima na kupalilia pamba.
“Ujenzi wa maghala nao ni jambo la muhimu sana kwani maghala mengi yalijengwa wakati wa utawala wa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Zamani,ujenzi wa maghala uligharimu kiasi cha Tsh.200ml, lakini kwa sasa ujenzi huo umepungua na kufikia Tsh. 50ml hii imetokana na utawala bora na usimamizi madhubuti” Amesisitiza Mirumbe.
Changamoto ya pembejeo za viua wadudu na pampu za kupulizia pamba,ni changamoto inayowaadili wakulima kwa kiasi kikubwa,ilikukabiliana na changamoto hiyo ni vyema, tukajenga owezo na uelewa mzuri kwa vyama vya ushirika ambavyo ni AMCOS na UNION ambazo zina uwezo wa kukopa kwenye Taasisi za fedha na kununua mbegu mahali sahihi mfano shinyanga na kuzipeleka vijijini. Inabidi kujenga uwezo wa ushirika wa msingi pamoja na Union ili waweze kununua pembejeo wenyewe na hii itasaidia sana kuepuka udanganyifu.Tuendelee kutumia ushirika, na vyama vya ushirika vya msingi viwatambue wakulima wake.Tuendelee kuutumia ushirika na tuupende ushirika’’ Amesema Mirumbe.
Mkulima Vetus Katebe kutoka Meatu, ameeleza kuwa kutokana na mradi wa kuwakopesha wakulima tumefaidika na fedha hizo kutoka Azania Bank japo zimekuja kwa kuchelewa sana, fedha hizo zimewasaida sana wakulima katika upandaji wa Pamba na kilimo cha kisasa. Kilimo cha kisasa kinaleta tija na matumaini mazuri,tunaomba mabwana shamba, wahudumu wetu walete huduma kwa wakati, ili tuanze kilimo mapema nahatimaye kumtoa mkulima katika hali ya chini. Bwana Katebe ameomba suala la utoaji wa elimu liwe endelevu.
Sanjali na hayo, Bw.Igelele Yakobo, Katibu wa Amcos ya Tusekelege Matongo, amemshukuru mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila kwa kazi ambayo amefanya, kwani imemuinua mkulima, na mategemeo ni kuongezekakwa ufanisi toka kg 175-350 kg kwa hekari. “Changamoto kubwa inayowakabili wakulima ni kwamba wakulima wetu hawana mitaji wakipatiwa mitaji wataweza kulima na kufikia kilo 1000, kwa heka. Tunaomba wasambazaji wa pembejeo, walete pembejeo kama mbegu mapema, ili mkulima ajiandae mapema.Wakulima wamekosa iman kwa AMCOS hivyo,AMCOS ambazo zina matatizo na wasio waadilifu wajirekebishe. Baadhi ya maeneo AMCOS zimewasaidia wakulima wao kupata mikopo. Elimu iendelee kutolewa kwa AMCOS na wakulima ili kuongeza tija na ufanisi”.Amesema Igelele.Mwisho.
0 comments:
Post a Comment