Wednesday, March 9, 2022

Wanawake Endeleeni Kufanya Kazi Kwa Bidii na Kuonyesha Mfano, Mafanikio Yenu Yasiwapelekee Kujisahau Kwamba Baba ndie Kichwa Cha Familia- RC KAFULILA

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila ameyasema hayo wakati wa sherehe ya siku ya wanawake Duniani, ambayo kimkoa imefanyika katika wilaya ya Itilima.

Mhe. Kafulila ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi ametembelea na kukagua mabanda ya wajasiriamali na kuwaagiza wakuu wa wilaya na wakungugenzi kutoa kipaumbele cha mikopo kwa wamama wajasiliamali  ambao bado hawajapata mikopo hiyo.


Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ,Mhe. Kafulilamesema “ sisi sote tumetoka kwa mama, binadamu pekee ambaye hakutoka kwa mama ni Adam pamoja na Hawa ambaye alitoka kwenye ubavu wa Adam, ambaye ni baba.Hivyo hii ni siku pekee ambayo inatupa fursa ya kutafakari safari ya mwanamke katika kutoa mchango wake kwenye taifa lake na dunia hii. 


Kwa uzoefu niliokuwa nao moja ya sifa kubwa ya mwananamke ni kuwa,Wanawake hawapendi kukosea, hivyo atafanya kila kinachowezekana ili asikosee, kwa hiyo leo tunasherehekea siku ya wanawake,mama ambaye ni nguzo ya familia na viumbe wenye uvimilivu kuliko kiumbel kingine chochote duniani.

 

“Wanawake ni waaminifu sana na tafiti zinaonyesha kwamba kati ya wanaume na wanawake, wanaorejesha mikopo kwa wakati ni wanawake. Hivyo Wakurugenzi na wakuu wa Wilaya katika mikopo yote mnayotoa kwa makundi ya wanawake, vijana na wenye ulemavu, mikopo kwa wanawake ipewe kipaumbelekwani hawa wamama/dada zetu endapo wanapewa mikopo ambayo ni mikubwa kidogo wana historia ya  kulipa kwa wakati. Tafiti  za kimataifa zinaonyesha Mwanamke anapofanya kazi na kupata kipato anarudisha nyumbani 90% ya kipato chakelakini mwanaume anapeleka 35% ”.Ameeleza Kafulila.

 

Aidha, akizungumzia mataifa mengine, Mhe. Kafulila ameitaja nchi ya Marekani ambayo iliwachukua  miaka 100 kuruhusu mwanamke kupiga kura,wakati kwa nchi ya Tanzania mifumo yetu ya kisheria haijawahi kumzuia mwanamke kupiga kura. Sanjari na hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Rais mwanamama Mhe.Samia Suluhu Hassan amefanikiwa kuituliza nchi na kuikusanya pamoja.Anaendesha nchi kwa viwango vya juu kabisa na nchi imetulia.Mhe. Samia Suluhu Hassan amewezesha upatikanaji wa fedha za miradi kila mahali. Kwa upande wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Samia Suluhu Hassan,ametoa fedha ambazo zimewezesha miradi 26 ya maji,miradi 58 ya barabara-TARURA, Miradi 37 ya TANROADS kufanyika.Amewezesha miradi 60 ya umeme kufanyika ilikuhakikisha kuwa umeme unapatikana katika vijiji 220 kwa kipindi cha miezi 18, ili ifikapo mwanzoni mwa 2023, mkoa mzima wa Simiyu uwe na umeme.

 

Vilivile fedha za Mama Samia zimewezesha mkataba mkubwa wa maji wenye thamani ya Tsh. 400 bln kufanyika mradi ambao utawezesha vijiji 240 vya mkoa wa Simiyu kupata maji.Mhe.Rais amewezesha upatikanaji wa Tsh. 5.1bln, ambazo zinatumika katika ujenzi wa majengo 25 kwa mpigo ya Chuo cha ufundi VETA.


Mama Samia ndio mfano wa kuigwa kwani amechukua mkopo mfuko wa fedha za kimataifa, mkopo wa UVIKO-19, na kuzitumia kujenga madarasa, kununua vifaa tiba, magari ya kubeba wagonjwa, mapinduzi sekta ya maji, umeme na elimu.

 

“Hivyo wanawake ninyi ni jeshi kubwa na mnaweza kufanya mambo makubwa zaidi.Natamani mfanye kitu kikubwa zaidi, Kamati ya Usalama nusu ya wajumbe ni wanawake. Wabunge wengi ni wanawake, Viongozi wa Taasisi nyingi mkoa wa Simiyu ni wanawake na wanasaidia sana sababu wengi ni wachapa kazi na wanafanya kazi vizuri Sana. Mimi kama kiongozi wenu nitawapa kila aina ya ushirikiano,natamani nione jambo kubwa kuliko mikoa mingine litakaloanzishwa na kufanywa na wanawake wa Simiyu, ili  watu wengine waje kujifunza, endeleni kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha mfano, mafanikio yenu yasiwapelekeekujisahau kwamba baba ndie kichwa cha familia.Amesisitiza Kafulila

 

Aidha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoani Simiyu yaliendana sambamba na matendo ya hiruma,ambazo zilitia ndani utoaji wa  madaftari 5000, ambayo yatasambazwa katika shule mbalimbali za mkoa wa Simiyu pamoja na mashuka na sabuni katika kituo cha afya cha ikindilo, wilayani Itilima.

 

Akizungumza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo amesema “wakina mama hawa kwa upendo wao wamechanga fedha ambazo zimetumika kununua madaftari 5000 ambayo yatagawiwa katika shule za wilaya zote za mkoa wa Simiyu”.Bi. Prisca Kayombo, amewaeleza washirki wa halfa hiyo kuwa, pamoja na 08/03/2022 kuwa kilele cha siku wa Wanawake Duniani kuanzia 01/03/2022 hadi 08/03/2022, shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanywa na kina mama, hii ikiwa ni pamoja na kutoa misaada mbalimbali, kutoa elimu kwa umma, pia baadhi ya kina mama wamepewa fursa ya kupata mikopo.Kawaida “Wakina mama hawakubali kushindwa, hivyo tukiwa kama Malkia tunapaswa kungara na kuwa na umoja’’.Amesisitiza Bi. Kayombo.

 

Nae Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Faidha Salum, amemshukuru Mkuu wa Mkoa pamoja na Katibu Tawala kwa kuiheshimisha Wilaya ya Itilima kwa kitendo cha kuipa fursa Itilima kuwa Wilaya Mwenyeji wa Maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, kimkoa. Aidha Mhe. Faidha amemshukuru sana ,Mam a
























Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapatia fedha ambazo zimesaidia katika miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtua mama ndoo kichwani. Mhe. Faidha na Wanaitilima wameahidi kushiriki kikamilifu katika suala la sensa“Tutahakikisha tunatoa watu wote ili wahesabiwe’’. Amesema Faidha.

 

Aidha pamoja na wanawake wa Mkoa wa Simiyu kushiriki kwa wingi katika siku ya wanawake dunia, siku hiyo ilihudhuriwa namwenyekiti wa  Umoja wa Wanawake (UWT-CCMMkoa wa Simiyu, Mama Manyangu,Madiwani na Wabunge wanawake wa mkoa wa Simiyu.

 

Akizungumza Mbunge anayewakilisha Vijana Mkoa wa Simiyu Mhe. Lucy Sabu aliwakumbusha wanawake kuwa “Mwanamke ni nuru iangazayo, mwanamke popote hakikisha kuwa unaangaza, jiheshimu, fanya kazi kwa bidii”amesisitiza Mhe.Lucy.Mwisho.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!