Balozi
wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu amesema angependa kuona katika kipindi chake atakachokuwepo hapa
nchini akiiwakilisha nchi ya Kenya ushirikiano wa kiabishara katika Kenya na
Tanzania na unaimarika na takwimu za biashara, viwanda na uwekezaji kati ya
nchi hizo zikiongezeka mara dufu.
Balozi
Kazungu ameyasema hayo wakati alipotembelea Kiwanda cha Kuchambua pamba cha
Alliance (Alliance Ginnery LTD), kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi
Oktoba 05, 2018 katika ziara yake mkoani Simiyu.
Balozi Kazungu
amesema ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hususani katika viwanda, kati ya
Tanzania na Kenya ukiendelea kuimarika zaidi utachangia kuongeza ajira, kuwatoa
wananchi katika umaskini pamoja na kuimarika kwa uchumi wa nchi hizo pia.
“Baada
ya miaka minne kazi yangu kama ikiisha hapa, naomba nione takwimu za viwanda,
biashara, uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya zinaongezeka mara dufu, nafasi za
kazi kwa watu wetu zinapatikana na watu wetu wanaondokana na umasikini; kukua
kwa Tanzania kuwe ndiyo kukua kwa Kenya hilo ndiyo ombi letu” alisema Mhe.
Balozi Kazungu.
Aidha,
Mhe. Kazungu ametoa wito kwa wananchi wa
Tanzania na Kenya kuepuka migogoro ya kibiashara ambayo kwa namna moja au
nyingine inaweza kuchangia katika kushuka kwa biashara kati ya nchi hizo, huku
akiwataka waandishi wa habari kuwa makini na kijiridhisha kabla kuandika habari
za kibiashara kwani zisipoandikwa kwa usahihi zinaweza kuchochea migogoro ya
kibiashara.
Aidha,
Balozi Kazungu amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuwa
atakuwa mstari wa mbele kuzungumza na wawekezaji nchini Kenya ili waje
kuwekeza, ambapo amebainisha kuwa Sekta binafsi na Shirikisho la watu wenye
viwanda hapa nchini wameshaanza kuzungumzia masuala hayo na wenzao wa Sekta
binafsi Kenya.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka amemwomba Balozi
Kazungu kuwaalika wawekezaji kutoka nchini Kenya na kubainisha kuwa mkoa uko
tayari kutoa ardhi bure kwa wawekezaji watakaojenga viwanda vinavyojibu
mahitaji ya mkoa, hususani katika kuongeza thamani ya zao la pamba, mazao
yatokanayo na mifugo kama ngozi na nyama.
Mtaka
amesema Mkoa wa Simiyu una uwezo wa kuzalisha pamba zaidi ya kilo milioni 400
na hadi sasa umezalisha kilo milioni112 ambazo ni zaidi ya asilimia 50 ya pamba
yote nchini; hivyo katika kuiongezea thamani pamba hiyo kiwanda kikubwa cha
kuzalisha bidhaa zaidi ya 20 za afya zitokanazo na pamba
“Simiyu tunao uwezo wa kuzalisha zaidi ya kilo
milioni 400 za pamba, mpaka sasa tumezalisha kilo milioni 112 ambazo ni zaidi
ya asilimia 50 ya pamba yote inayozalishwa hapa nchini; katika kuongeza thamani
ya zao la pamba, mwaka huu tutaanza ujenzi wa kiwanda kikubwa kitakachozalisha
zaidi ya bidhaa 20 za afya zitokanazo na pamba, kitakachojengwa na Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kwa
kushirikiana na wadau wengine na Mkoa wa Simiyu tumetoa ardhi bure” alisema Mtaka.
Ameongeza kuwa kipaumbele cha
pili cha mkoa baada ya kujenga kiwanda hicho ni kuwa na uwekezaji katika
viwanda vya nguo(textile industries) ili kupata bidhaa ya mwisho katika zao la
pamba, hivyo akaendelea kutoa wito kwa wawekezaji ndani na nje ya nchi kuwekeza
katika eneo hili.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya
Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni Mwekezaji kutoka Nchini Kenya
amesema lengo la Kampuni hiyo yenye Kiwanda cha kuchambua pamba ni kwenda
katika kuongeza thamani ya zao la pamba, ili faida itakayopatikana irudi kwa
wakulima kwa kuifanya pamba yao ikanunuliwa kwa bei nzuri itakayowapa motisha
ya kuendelea kuzalisha zaidi.
MWISHO
Balozi wa Kenya
nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kushoto) akiangalia mbegu za zao la
pamba zinazozalishwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance
Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati
alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018.
Mkurugenzi wa Kampuni
ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni mwekezaji kutoka Nchini kenya(wa
kwanza kulia), akimuongoza Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu
(wa pili kulia) na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu, kuelekea katika moja ya
majengo ya Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli
wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani hapo, Oktoba 05, 2018.
Mfanyakazi wa katika
Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata
ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, akitoa maelezo ya namna mbegu za
pamba zinavyoandaliwa kwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu
(aliyeshika mbegu katikati), wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05,
2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akiangalia akiangalia mbegu za zao la pamba zinazozalishwa
katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd),
kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani humo, wakati ziara ya Balozi
wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa nne kulia) kiwandani hapo, Oktoba 05, 2018.
Balozi wa Kenya nchini
Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa tatu kushoto) akiangalia pamba iliyochambuliwa
katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd),
kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati alipotembelea
kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018 (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka na (wa pili kushoto) Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance Ginnery Ltd, Bw.
Boaz Ogola akitoa maelezo kwa Balozi huyo.
Balozi wa Kenya nchini
Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (aliyetanguliza mikono kushoto) akiwaeleza jambo
viongozi wa mkoa wa Simiyu na viongozi wa Kiwanda ca kuchambua pamba cha Alliance Ginnery Ltd, wakati alipotembelea
kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018.
Mfanyakazi wa katika
Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata
ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, akitoa maelezo ya namna mbegu za
pamba zinavyoandaliwa kwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa
tatu kulia), wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018.
Balozi wa Kenya nchini
Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kulia) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) wakiwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha
Alliance kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa
ziara ya Balozi huyo kiwandani hapo,
Oktoba 05, 2018.
Mkurugenzi wa Kampuni
ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni mwekezaji kutoka Nchini
Kenya(wa pili kulia), akitoa maelezo kwa
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (katikati) katika moja
ya majengo ya Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli
wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani hapo, Oktoba 05, 2018.
Mkurugenzi wa Kampuni
ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni mwekezaji kutoka Nchini
Kenya(wa pili kulia), akitoa maelezo kwa
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (katikati) katika moja
ya majengo ya Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli
wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani hapo, Oktoba 05, 2018.
Mkurugenzi wa Kampuni
ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni mwekezaji kutoka Nchini
kenya(kulia), akimuongoza Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa
pili kulia) na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu, kuelekea katika moja ya
majengo ya Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli
wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani hapo, Oktoba 05, 2018.
Balozi wa Kenya nchini
Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (kushoto) akiwaeleza jambo baadhi ya viongozi wa
Mkoa wa Simiyu na Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance katika moja ya
majengo hicho kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati
wa ziara ya Balozi huyo kiwandani hapo,
Oktoba 05, 2018.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance(Alliance Ginnery
Ltd) wakiendelea na kazi katika sehemu ya uzalishaji wa mbegu katika kiwanda
hicho kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara
ya Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu(hayupo pichani) kiwandani
hapo, Oktoba 05, 2018
0 comments:
Post a Comment