Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. Angelina Mabula ameshauri Wizara ya Viwand, Biashara na Uwekezaji kuona
namna ya kuwa na Kliniki za Biashara ngazi ya kanda ili kuwasaidia wafanyabiashara
hususani wale wanaoanza, wajasiriamali wadogo na wasiojua taratibu za
uendeshaji wa biashara zao kujua na kuwa wafanyabiashara wazuri.
Mhe.Mabula ameyasema hayo mara baada ya kutembelea banda
la Maonesho la Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TanTrade) katika Maonesho ya
Viwanda Vidogo (SIDO) yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi
Mkoani Simiyu.
Amesema
amepongeza Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji kubuni Kliniki ya biashara ambayo
inachangia kuwandaa wafanyabiashara kufahamu wafanye nini kabla na baada ya
kuanzisha biashara na kufanya biashara zao kwa kuzingata sheria, kanuni na
taratibu za nchi hii
“Ili
mtu awe huru kufanya biashara yake ni lazima zingatie sheria kanuni na taratibu
za nchi hii, mtu anapokuja kwenye kliniki hii anaambiwa kabla ya kuanza
anatakiwa apitie hatua zipi na aweke mazingira yapi, ili atambulike na TRA
anapaswa afanye nini na mambo mengine
mengi na wakizingatia wanachoambiwa hapa hawahitaji kukimbizana na mgambo wa
polisi”
“Ninashauri
Wizara ya Viwanda ione namna ya kuwa na kliniki za biashara kikanda ili
wafanyabiashara wanaoanza, wajasiriamali wadogo na wale wasiojua taratibu
waweze kujua taratibu na wawe wafanyabiashara wazuri” alisema Mhe. Mabula.
Afisa
Biashara Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara hapa nchini (TanTrade)
Bi. Magdalena Shirima amesema hadi kufikia Oktoba 26, 2018 wajasiriamali zaidi
ya 60 walioshiriki katika Maonesho ya SIDO Kitaifa wamehudhuria Kliniki hiyo
kupata huduma.
Baadhi
ya Wajasiriamali waliopata nafasi ya kushiriki na kupata huduma za ushauri wa
kibiashara kupitia Kliniki hiyo wamesema imewasaidia kubadili mitazamo dhidi ya
biashara zao na kufahamu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uanzishaji wa
biashara, namna ya kutangaza biashara zao na umuhimu wa kusajili biashara zao
ili ziweze kutambulika kisheria.
Maonesho
haya ya Viwanda Vidogo (SIDO) ni ya kwanza Kitaifa yakiwa na Kauli Mbiu “Pamoja
Tujenge Viwanda Kufikia Uchumi wa Kati” ambayo yalianza Oktoba 23, 2018
yatahitimishwa Oktoba 28, 2018.
MWISHO
Naibu Waziri waNyumba
na Maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula akizungumza na Watumishi wa
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) alipotembelea banda la Mamlaka hiyo
katika Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018
yanayoendelea katika Viwanja vya
Nyakabindi Simiyu, ambapo huduma za Kliniki ya Biashara zinatolewa.
Naibu Waziri wa Nyumba
na Maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(wa pili kushoto) akiongozwa na
viongozi wa Shirika la Kuhudumia viwanda Vidogo (SIDO) kuelekea katika
kutembelea mabanda ya maonesho ya Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018 yanayoendelea katika Viwanja vya Nyakabindi Simiyu.
Naibu Waziri waNyumba
na Maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kutembelea banda la maonesho la Kiwanda cha Chaki Maswa Oktoba 26,
2016 wakati alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika ya Maonesho ya
SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018
yanayoendelea katika Viwanja vya
Nyakabindi Simiyu.
Naibu Waziri wa Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akipewa maelezo kuhusu mashine
mbali za kuongeza thamani mazao mbalimbali wakati alipotembelea mabanda
mbalimbali ya maonesho katika ya Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018 yanayoendelea
katika Viwanja vya Nyakabindi
Simiyu.
Naibu Waziri wa Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula akiangalia baadhi ya bidhaa za
ngozi zilizotengenezwa a wajasiriamali wadogo , wakati alipotembelea mabanda
mbalimbali ya maonesho katika ya Maonesho ya SIDO Kitaifa Oktoba 26, 2018 yanayoendelea
katika Viwanja vya Nyakabindi
Simiyu.
0 comments:
Post a Comment