Balozi
wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan
Kazungu amefanya ziara mkoani Simiyu Oktoba 03, 2018 na kuzungumza na viongozi
wa mkoa huo, ambapo ameeleza kuwa moja ya malengo ya ziara yake ni kufahamu Mipango
na Fursa za Uwekezaji zilizopo mkoani Simiyu, ili aweze kuzungumza na
wawekezaji nchini Kenya kuwekeza mkoani humo.
Balozi Kazungu
amesema nchi ya Kenya ndiyo inaongoza kuwekeza nchini Tanzania ukilinganishwa
na nchi nyingine za Afrika ambapo hadi
sasa imewekeza takribani dola za Kimarekani bilioni 1.6 hapa nchini.
“
Nimekuja hapa ili tufahamiane vizuri,
nijue mipangilio yenu, fursa za uwekezaji ziko wapi ili tuweze kuzungumzana
wenzetu wakaja kuwekeza, Kenya ni nchi inayoongoza kwa kuwekeza nchini
Tanzania, hadi sasa imewekeza takribani dola bilioni 1.6 ” alisema Balozi
Kazungu.
Aidha,
ameomba ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya uendelee kuimarishwa kwa lengo la
kuzifanya nchi hizi kuwa shina la
viwanda na uwekezaji na kuwa wanufaika wa soko la pamoja la Afrika hali
itakayochangia kuimarisha uchumi wa nchi hizo.
Pamoja na
ushirikiano katika masuala ya uwekezaji na viwanda Balozi Kazungu amesisitiza
masuala ya ujirani mwema, upendo na ushirikiano wa kindugu baina ya nchi hizo
mbili.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa
Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo inakaribisha sekta
binafsi na iko tayari kutoa ardhi bure
kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza Simiyu katika maeneo yanayojibu mahitaji ya mkoa na nchi kupitia malighafi
zinazolishwa ndani ya mkoa na ndani ya nchi.
“Kwa mtu aliye tayari kujenga
kiwanda kinachojibu mahitaji yetu kama mkoa hasa kitakachutumia malighafi
tulizonazo mfano atakayewekeza kwenye viwanda vya kusindika nyama, viwanda vya
kutengeneza bidhaa za ngozi, pamba na yeyote atakayewekeza kwenye viwanda
vyenye malighafi inayozalishwa hapa nchini, tutampa ardhi bure” alisema
Mtaka amemweleza Balozi Kazungu
kuwa mkoa huo pia uko tayari kutoa ardhi
bure kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa vyuo ikiwemo vya
ufundi na utalii ili kuwajengea vijana ujuzi .
Naye Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema mafanikio ya Mkoa huo yanayopelekea
kufanya vitu vikaonekana ikiwa ni pamoja
na kuwa na Mwongozo wa Uwekezaji ni ushirikiano uliopo kati ya viongozi,
watendaji, wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwepo Taasisi za Serikali na binafsi,
sekta binafsi, madhehebu ya dini pamoja na wananchi
.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha
kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery kilicjopo Bariadi, Bw. Boaz Ogola ambaye
ni Mwekezaji kutoka nchini Kenya amemweleza Balozi kuwa Tanzania ni nchi yenye
amani na mahali sahihi kwa uwekezaji,
hivyo akatoa wito kwa Mhe. Balozi kuwaalika Wafanyabiashara kutoka
Kenya kuja kuwekeza Simiyu na Tanzania kwa ujumla
MWISHO
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akisaini kitabu cha katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mara
baada ya kuwasili Mjini Bariadi wakati
wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018(kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(katikati) Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akisalimiana na Mkuu wa mkoa
wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(kulia) ,
mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi
wakati wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akisalimiana na Mkuu wa mkoa
wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(kulia) , mara
baada ya kuwasili Mjini Bariadi wakati
wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.
Balozi wa Kenya nchini
Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, akisalimiana
na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini mara baada ya kuwasili
Mjini Bariadi wakati wa ziara yake
mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akisaini kitabu cha katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mara
baada ya kuwasili Mjini Bariadi wakati
wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018(kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(katikati) Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akitoa maelezo ya Mkoa kwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu(kulia), ambaye alifika
mkoani humo kwa ziara ya kikazi Oktoba 03, 2018
Kutoka kulia Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony
Mtaka, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu na Mkurugenzi wa Kiwanda cha
kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery kilichopo
Bariadi, Bw. Boaz Ogola wakiteta jambo, wakati wa ziara ya Balozi huyo mkoani Simiyu,
Oktoba 03, 2018.
Kutoka kushoto Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne
Sagini, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, wakimuonesha jambo Balozi wa
Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu katika Mwongozo wa Uwekezaji
wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya Balozi huyo mkoani Simiyu, Oktoba 03,
2018.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akisalimiana na Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi ,
mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi
wakati wa ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.
Mkuu wa mkoa wa
Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu, mara baada ya kuwasili
Mjini Bariadi wakati wa ziara yake
mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.
Kutoka
kulia Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu na Mkurugenzi wa Kiwanda cha
kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery kilichopo
Bariadi, Bw. Boaz Ogola wakiteta jambo, wakati wa ziara ya Balozi huyo mkoani Simiyu,
Oktoba 03, 2018.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu akizungumza na viongozi wa
Mkoa wa Simiyu , Mjini Bariadi wakati wa
ziara yake mkoani humo, Oktoba 03, 2018.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu ( wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani Simiyu, Oktoba 03,
2018.
Mkurugenzi wa Kiwanda
cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu wakati wa ziara ya Balozi
huyo mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.
Baadhi ya viongozi na waandishi wa habari mkoani Simiyu wakisikiliza Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu Mjini Bariadi, wakati wa ziara ya Balozi huyo mkoani Simiyu, Oktoba 03, 2018.
0 comments:
Post a Comment