Wafugaji Mkoani Simiyu wanatarajia kuboresha ufugaji
wao kupitia Mpango Mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia ya uhimilishaji kwa lengo la kuongeza tija katika
uzalishaji wa mazao ya mifugo, mpango unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi
Desemba, 2018.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha Wadau wa Mifugo
mkoani Simiyu, kilichofanyika Oktoba 10, 2018 mjini Bariadi, kwa lengo la
kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha mifugo kwa njia ya Uhimilishaji (Artificial Insermination),chini
ya Uenyekiti wa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka.
Akizungumza katika kikao hicho Mratibu wa Mpango wa
Uhimilishaji kutoka Shirika la Land O’
Lakes, Bw. Joachim Balakana amesema shirika
hilo kwa kushirikiana na mkoa wa Simiyu limelenga kuhakikisha wafugaji wa ng’ombe
wa kienyeji na kisasa wanafanya uhimilishaji ili kuboresha mbari za ng’ombe wao
na kuongeza tija katika uzalishaji wa maziwa na nyama.
“Uhimilishaji
utafanyika kwa kutumia mbegu bora zilizozalishwa hapa nchini katika kituo cha
Uhimilishaji Arusha, baada ya ng’ombe wa kienyeji kuhimilishwa tunategemea
kupata ng’ombe chotara wa waziwa ambao watakuwa wakitoa maziwa mengi na wa nyama
watakaofikia uzito mkubwa ndani ya muda mfupi”alisema Balakana.
Ameongeza
kuwa kupitia mpango huu ng’ombe zaidi ya 12,000 wanatarajiwa kuhimilishwa
mkoani Simiyu kuanzia Desemba, 2018, huku akibanisha kuwa kutokana na mwitikio
mkubwa wa wafugaji na viongozi mkoani humo, ng’ombe zaidi ya hao waliolengwa
wanaweza kuhimilishwa na ndani ya muda mfupi matokeo makubwa yakaonekana.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi,Mhe. Festo Kiswaga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa huo una ng’ombe wengi hivyo,
uhimilishaji utasaidia kuongeza thamani ya mifugo kwa upatikanaji wa mbegu
bora, ambapo ng’ombe wa nyama watakuwa na uzito mkubwa wakiwa na umri mdogo,
ngombe wa maziwa kutoa maziwa mengi na ngozi bora pia itapatikana.
Ameongeza
kuwa mkoa huo umejipanga kuboresha ufugaji na kuwasaidia wafugaji kuona thamani
ya ufugaji, huku akibainisha kuwa upo uhakika wa kuyaongezea thamani mazao ya
mifugo hususani maziwa, kutokana na uwepo wa kiwanda cha maziwa wilayani Meatu ambacho
kiko katika mpango wa kupanuliwa ili
kukiongezea uwezo katika uzalishaji.
Akiwasilisha
taarifa ya hali ya uboreshaji mifugo ya
mkoa wa Simiyu, Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.
Gamitwe Mahaza amesema jumla ya ng’ombe 348 waliozaliwa kwa njia ya
uhimilishaji kati ya ng’ombe 1,598,935 waliopo, hivyo mkoa unaendelea kufanya
jitihada mbalimbali kuhimiza uhimilishaji katika halmashauri zote mkoani humo.
Dkt.
Gamitwe ametaja moja ya juhudi hizo kuwa ni pamoja na kuzielekeza Halmashauri
kutenga asilimia 15 ya mapato ya ndani yatokanayo na mifugo kwa lengo la
kuanzisha mfuko wa maendeleo wa mifugo, kuzihamasisha halmashauri kununua vifaa
vya uhimilishaji na kununua madume bora.
Kwa
upande wao baadhi ya viongozi wa wafugaji na wafugaji wamesema wameupongeza
uongozi wa mkoa kwa kufikiri namna ya kuboresha ufugaji kupitia na mpango wa
uhimilishaji na wakaeleza kuwa wameupokea mpango huo na kuomba uanze
kutekelezwa mara moja ili waweze kuona tija katika ufugaji wao.
“Naishukuru
Serikali kuleta mpango huu wa kuhimilisha ng’ombe wetu nimeupokea kwa furaha
sana na ninaomba wataalam waje haraka kutuelimisha wafugaji, ili uanze
kutekelezwa haraka tupate kuona faida ya
ufugaji, tupate maziwa mengi na ng’ombe wa nyama wenye uzito mkuwa kama mtaalam
alivyotueleza” alisema Bw. Mathias Gabriel
Mfugaji kutoka Kijiji cha Mwanegele wilayani Maswa.
“
Nimeupenda mpango wa uhimilishaji ambao utasaidia kuboresha ng’ombe wa kienyeji
tulionao sasa, na mimi kama Katibu wa Wafugaji Itilima napendekeza mpango huu utakapoanza
uanzie kwangu, ili wafugaji wengine waje wajifunze kutoka kwangu” Katibu wa Wafugaji Wilaya ya Itilima, Samson
Kingi Guma alieleza.
Mpango mkakati wa uboreshaji wa mifugo kwa njia ya
Uhimilishaji Mkoani Simiyu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya
Mifugo, Shirika la Land O’ Lakes chini
ya Mradi wa Ushirikishwaji wa Sekta ya Umma na binafsi katika utoaji wa huduma
za Uhimilishaji (PAID), kwa ufadhili wa Mfuko wa wakfu wa Bill na Melinda
Gates.
MWISHO
Mkuu
wa Wilayaya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha wadau wa mifugo
mkoani Simiyu, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018
kwa lengo la kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa
asili kwa njia ya uhimilishaji.
Mratibu wa Mpango wa
Uhimilishaji kutoka Shirika la Land O’
Lakes, Bw. Joachim Balakana akizungumza na wadau wa mifugo Mkoani Simiyu katika
kikao cha wadau wa mifugo kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa
lengo la kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia ya uhimilishaji.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Simiyu, Mhe Enock Yakobo katika kikao cha wadau wa mifugo kilichofanyika Mjini
Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa lengo la kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa
kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia ya uhimilishaji.
Katibu wa Wafugaji
Wilaya ya Itilima, Samson Kingi Guma akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mifugo kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa lengo la
kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia ya uhimilishaji.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Maswa, Mhe. Paul Jidayi akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mifugo kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa lengo la
kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia ya uhimilishaji.
Katibu Tawala Msaidizi
Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.
Gamitwe Mahaza taarifa ya hali ya uboreshaji wa mifugo mkoani humo, katika kikao cha wadau wa mifugo kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa lengo la
kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia ya uhimilishaji.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mifugo kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa lengo la
kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia
ya uhimilishaji.
Mfugaji kutoka Kijiji
cha Mwanegele wilayani Maswa, Bw. Mathias Gabriel akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mifugo kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa lengo la
kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa
njia ya uhimilishaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mifugo, kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa lengo la
kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia
ya uhimilishaji.
Baadhi ya wadau wa mifugo mkoani Simiyu, uwasilishaji
wa mada mbalimbali katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi Oktoba 10, 2018 kwa lengo la
kujadili Utekelezaji wa Mpango mkakati wa kuboresha ng’ombe wa asili kwa njia ya uhimilishaji.
0 comments:
Post a Comment