Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika
la viwanda vidogo nchini SIDO kuweka
mikakati ya kupanua wigo wa shughuli zake kwa kuanzisha vituo katika ngazi ya halmashauri
za wilaya ili kuwafikia wajasiliamali wengi zaidi, kuwajengea uwezo, kuwapa
miongozo bora ya namna ya kuendesha shughuli zao kwa tija na kuwaunganisha na
taasisi za fedha waweze kupata mikopo.
Waziri mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo
katika ufunguzi wa maonesho ya SIDO Kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi
Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu ambapo amesema umefika wakati kwa SIDO kutilia
mkazo sekta ya viwanda na hivyo kuifanya jukwaa la kuwakutanisha wabunifu pia
kuwapa fursa ya kuonyesha uwezo wao katika matumizi ya teknolojia rafiki na
rahisi zitakazoharakisha maendeleo ya viwanda nchini.
Pia
Waziri Mkuu Majaliwa amesema SIDO inapaswa kujielekeza katika kubuni mashine ,
mitambo na teknolojia rahisi zitakazotumika kuongeza thamani ya bidhaa na
kusisitiza kuwa kutokana na umuhimu wa
sekta ya viwanda nchini katika kukuza ajira na kuongeza pato la taifa serikali
itaendelea kuweka miundombinu wezeshi itakayoharakisha kasi ya ukuaji wa
viwanda.
“
Bila shaka nyote mnafahamu tumedhamiria kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka
2025, ninaamini tunao uwezo wa kulifikia lengo hili, sasa tunachotakiwa kufanya
kuhakikisha halmashauri zetu zote zinatenga maeneo maalumu kwa ajili shughuli
za viwanda kama mlivyofanya hapa Simiyu, lakini pia lazima mhakikishe
mnawajengea uwezo wajasiliamali ili waweze kuingia katika soko la ushindani,
alisisitiza Waziri Mkuu Majaliwa”
.
Waziri
Mkuu Majaliwa amewasisitiza SIDO
waendelee kubuni mikakati itakayoleta mabadiliko katika sekta ya viwanda huku
akiwataka wananchi kuthamini bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini ambazo tayari
zimeonyesha kukidhi mahitaji ya soko.
Halikadhalika
waziri Mkuu Majaliwa ameziagiza halmashauri za wilaya nchini kuendelea
kutekeleza agizo la kutenga 10% ya
mapato yake ya ndani kwa ajili ya mikopo ya wanaweke, vijana na walemavu
huku akiwasisitiza madiwani katika
halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa agizo hilo.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa ameupongeza uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa
kujenga mahusiano mema na wananchi, viongozi
wa kisiasa pamoja na taasisi mbalimbali jambo ambalo amesema ni chachu
ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii mkoani Simiyu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo(SIDO), Prof.
Sylvester Mpanduji amesema Shirika hilo litaendelea kutoa mafunzo kwa
wajasriamali ili kuwajengea uwezo zaidi, ambapo amebainisha kuwa katika mwaka
wa fedha 2017/2018 SIDO imetoa mafunzo kwa wajasiriamali 16,900.
Aidha,
Prof. Mpanduji ameishukuru Serikali kwa kutenga shilingi bilioni 29 katika
mwaka wa fedha 2018/2019 ambazo zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali za
wajasiriamali ikiwemo upatikanaji wa mashine mpya zitakazotumika katika vituo
vya SIDO vya kuendeleza viwanda, kukopesha wajasiriamali mitaji na kujenga
miuondombinu mingi ya viwanda katika sehemu hapa nchini.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amemhakikishia Waziri mkuu
kuwa Mkoa huo utahakikisha
unaendelea kutekeleza maagizo ya serikali ikiwemo agenda ya kitaifa ya Uchumi
wa Viwanda kupitia Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa Moja.
“Simiyu
ni Mkoa wenye ajenda na kazi yetu ni kutekeleza maelekezo na miongozo yote ya
Serikali, tunatekeleza Sera ya Viwanda chini ya Falsafa ya Wilaya Moja Bidhaa
Moja na sasa tunaenda kwenye utekelezaji wa Kijiji Kimoja Bidhaa Moja na sisi
tunaamini Mapinduzi ya Viwanda yanaanza na SIDO” alisema Mtaka.
Maonesho
hayo ya SIDO ambayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mkoani Simiyu yamehudhuriwa
na wajasiliamali zaidi ya 500 kutoka mikoa
mbalimbali hapa nchini ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
MWISHO
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonesho
ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi
Mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Simiyu,
katika Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23,
2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani
Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO)
Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
(katikati) akiangalia moja ya mashine zitumikazo kutengeneza bidhaa mbalimbali
zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda Vidogo(SIDO) Kitaifa, yatakayofanyika
kuanzia Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya
Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
akiangalia sabuni zinazotengenezwa katika Kiwanda kidogo cha Itilima mkoani
Simiyu, wakati wa Ufunguzi wa wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa,
uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiangalia
teknolojia rahisi ya utengenezaji wa chaki
kabla ya Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa (SIDO),
uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(wa tatu
kulia) akiangalia baadhi ya mashine zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda
Vidogo Kitaifa(SIDO) yanayofanyika Mkoani Simiyu, Oktoba 23-28, 2018 katika
Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mjasiriamali
kutoka mkoa wa Kagera(kushoto) akiwasilisha changamoto zake kwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati wa
Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23,
2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani
Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipata
maelezo ya mbegu bora za alizeti kutoka kwa Mjasiriamali kutoka Mkoa wa
Singida, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho
ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja
vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Kikundi
cha Ngoma cha BASEKI kutoka Mjini Bariadi kikitoa burudani wakati wa Ufunguzi
wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018
katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani
Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa
(katikati) akiangalia moja ya mashine zitumikazo kutengeneza bidhaa mbalimbali
zilizoletwa katika Maonesho ya Viwanda Vidogo(SIDO) Kitaifa, yatakayofanyika
kuanzia Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya
Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiwasalimia wananchi kabla ya
kuwasilisha salamu za Mkoa, wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO)
Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akipanda
mti mara baada ya kufungua Maonesho ya
Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya
Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kufungua Maonesho ya Viwanda
Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi
Mkoani Simiyu.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiagana
na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini mara baada ya kufungua Maonesho
ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja
vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye shati la kitenge)akiwaongoza
wakuu wa mikoa jirani Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela(mwenye kofia) na
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi. Robert Gabriel katika kupanda mti , mara baada
ya Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda
Vidogo (SIDO) Kitaifa, uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi
Mkoani Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) na Viongozi wa wengine
wa SIDO na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakimuongoza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kueleka kwenye mabanda ya maonesho wakati Ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,
uliofanyika Oktoba 23, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment