Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania kwa kuagiza ving’amuzi vyote vyenye leseni ya kutoa Huduma za Utangazaji
kwa kwa Maudhui yanayotazamwa bila kulipia kuonyesha chaneli za ndani bure.
Pongezi hizo amezitoa
wakati akifungua mkutano wa viongozi wa mkoa wa Simiyu. na baadhi ya viongozi wa Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kwa lengo la kujadili Huduma
za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA, kilichofanyika
Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi..
“Niwapongeze sana TCRA kwa kuhakikisha kwamba, watu wanakuwa na uhuru wa
kulipia kwenye chaneli wanazozihitaji lakini zile Televisheni zetu za ndani za
kuangalia mambo yetu kama Watanzania wanazipata bure” alisema Mtaka.
Amesema anaridhishwa na utendaji wa kazi wa TCRA kwa
kuleta mabadiliko makubwa na kutoa wito kwa TCRA kuangalia gharama ya kulipia
ving'amuzi kwa bei nafuu ili kuwafikia wananchi wengi.
“Ukitaka kushindana kwenye dunia wekeza kwenye
teknolojia, TCRA mtusaidie namna vyombo hivi vinavyofanya mawasiliano kwa Umma
ambayo ndio chakula chetu cha kila siku wananchi wapate kwa urahisi,
tusiwanyime watu fursa, kama
tunawapelekea umeme kwa elfu 27, mtu awe na uwezo wa kuuza kuku wake mmoja na
akalipia king’amuzi”alisema.
Naye Mhandisi.
Francis Mihayo TCRA
amesema Serikali kupitia TCRA amesema watu wamekuwa wakijuliza kwa nini chaneli
ambazo zinatakiwa kuonekana bure zilizokuwa zinabebwa kwenye kisimbuzi cha
kulipia, zimeamriwa zirudishwe kwenye visimbuzi vya watoa huduma wanaoruhusiwa
kuzibeba chaneli hizo, pasipo malipo ndiyo maana wamelazimika kufanya mkutano
huo.
Amesema Baada ya watoa huduma wenye visimbuzi vya kulipia
kuamriwa kutoa chaneli za ndani ambazo si za kulipia TCRA iliwatangazia
wananchi watoe taarifa zao binafsi na
kuziwasilisha TCRA, ambazo ni jina , eneo analoishi, aina ya kisimbuzi ,namba
ya kisimbuzi, namba ya kadi ya kisimbuzi, muda aliotumia kisimbuzi hicho na kiasi
cha fedha ambacho amekuwa akilipia kila mwezi na kutuma kwenye barua pepe ya
Mkurugezi Mkuu ambayo ni dg@tcra.go.tz.
Ameongeza kuwa hadi sasa Serikali kupitia TCRA
inaendelea kukusanya taarifa ili wale waliokuwa wakitumia visimbuzi vyenye
leseni ya kulipisha na vilikuwa vikibeba chaneli ambazo si za kulipisha baadaye
itatoa maamuzi.
Amesisitiza kuwa TCRA ilitoa muda mpaka kufikia
Septemba 05 2018 chaneli zote ambazo zilipaswa kuonekana bila kulipia zilitakiwa
ziwe zinaoneshwa kwenye visimbuzi visivyolipisha lakini kulitokea changamoto ya
tatizo la kiufundi ambalo lilipelekea chaneli hizo kuanza kurejeshwa taratibu.
Pamoja
na kujibu maswali na kutolea ufafanuzi changamoto mbalimbali zilizowasilishwa
na wajumbe wa Mkutano huo, Mhandisi Mihayo alitaja baadhi chaneli ambazo
hazipaswi kulipiwa kuwa ni (kwa mkoa wa
Simiyu ) ni pamoja na TBC 1, ITV, Star TV, Channel Ten, EATV, Clouds, UHAI na Bunge TV.
Akizungumza
mara baada ya mkutano huo, Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Bi. Mwanahamisi Kawega aliishukuru TCRA kwa kutoa elimu jambo
ambalo na namna ya kupata haki yao ya kupata taarifa.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akifungua mkutano wa
Viongozi wa Mkoa huo na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) kuhusu Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA, uliofanyika
Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Mhandisi. Francis Mihayo kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) akiwasilisha mada kuhusu Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA, kwa Viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika mkutano uliofanyika Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi katika mkutano wa Viongozi wa Mkoa huo na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA, Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani
akichangia hoja katika mkutano
wa Viongozi wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu na
baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika
kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA,
Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa
Simiyu, SSF. Crispin Rabiuzima akichangia hoja katika mkutano wa Viongozi wa Mkoa wa Mkoa wa
Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia
– FTA, Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi
wakifuatilia mjadala katika Mkutano wa Viongozi wa Mkoa wa Mkoa
wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila
Kulipia – FTA, Oktoba 02, 2018.
Mkku wa Wilaya ya
Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akichangia
hoja katika Mkutano wa Viongozi wa Mkoa
wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) uliofanyika kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila
Kulipia – FTA,Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, Dkt. Mabimbi akichangia hoja katika Mkutano wa Viongozi wa Mkoa wa Mkoa wa
Simiyu na baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika
kujadili Huduma za Utangazaji kwa Maudhui yanayotazamwa Bila Kulipia – FTA,
Oktoba 02, 2018 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment