Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani humo na maeneo mengine nchini kujitokeza
kwa wingi kushirikia katika Maonesho ya Kitaifa
ya Viwanda Vidogo (SIDO), yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23-28, mwaka huu
katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani humo na kubainisha kuwa Maandalizi
yote yamekamilika.
.Akizungumza na waandishi wa
habari Ofisini kwake Mtaka amesema Maonesho haya yatafunguliwa rasmi siku ya
Jumanne Oktoba 23, 2018 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Kassim Majaliwa.
Ameongeza kuwa katika maonesho
hayo wajasiriamali, waoneshaji wa teknolojia mbalimbali wamealikwa na
kusisitiza kuwa hii ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine
kuona ushindani katika uongezaji wa thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa
wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.
“ Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa
wa Simiyu kujitokeza kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa kwao ya kuweza kujielimisha
katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo,
lakini pia wajasiriamali watapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa
maeneo mengine nchini na nje ya nchi” alisema Mtaka.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji
wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO),
Shoma Kibende amesema tayari wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali wamethibitisha
kushiriki maonesho hayo na baadhi yao wameanza kuwasili.
“Wajasiriamali zaidi ya 1000 kutoka mikoa yote nchini
wanatarajia kushiriki maonesho haya na baadhi yao wameshaanza kuwasili, lakini
pia kuna taasisi mbalimbali ambazo ni taasisi shirikishi na SIDO, huduma za
kupata ubora hii ni fursa pekee kwa Watanzania” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif
Shekalaghe amesema zaidi ya wajasiriamali 51 kutoka wilayani humo watashiriki
katika kuonesha bidhaa mbalimbali ambazo wametengeneza na kuzalisha kupitia
viwanda vidogo.
Naye
Meneja wa SIDO Mkoa wa Kagera,Richard Mahela amesema maonesho ya SIDO ambayo ni
ya kwanza kufanyika Kitaifa yatawasaidia
wajasiriamali kote nchini kupanua masoko ya bidhaa zao kwa kuwa wameandaa
vipeperushi vya bidhaa zao ambavyo vitasambazwa
kwa lengo la kusaidia kuwaunganisha na wanunuzi.
Maonesho
ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa ambayo ni ya kwanza kufanyika ngazi ya Kitaifa
yatafunguliwa rasmi Jumanne Oktoba 23, 2018 na kuhitimishwa siku ya Jumapili
Oktoba 28, 2018 yakiwa na Kauli Mbiu: PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA
KATI”.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe, Anthony Mtaka akizungumza na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) , juu ya
ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28,
2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Kaimu Mkurugenzi
wa Masoko na Uwekezaji wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Shoma Kibende
akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka na
Waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya ufunguzi wa
Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika
Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya Waandishi wa
Habari na Maafisa na Mameneja wa SIDO wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe, Anthony Mtaka katika mkutano wake na Waandishi wa Habari, juu ya ufunguzi
wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018
katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi ya Mameneja wa
SIDO wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka katika mkutano
wake na Waandishi wa Habari, juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo
Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi
Bariadi Simiyu.
Mkuu wa
Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka na Waandishi wa habari(hawapo pichani)
juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba
23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Meneja wa
SIDO Mkoa wa Kagera Richard Mahela akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka na Waandishi wa habari(hawapo pichani)
juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba
23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
Baadhi
ya mabanda ya maonesho yakiendelea kuandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Viwanda
Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi Simiyu
0 comments:
Post a Comment