Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vidogo (SIDO)
ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi,
kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka katika kikao cha maandalizi ya maonesho hayo kilichowashirikisha baadhi ya viongozi
wa mkoa wa Simiyu na mameneja wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO) kutoka mikoa
ya Simiyu, Dodoma ,Mwanza, Kagera ,Mara, Shinyanga na Arusha.
Mtaka amewakaribisha wananchi wa
mkoa mwenyeji Simiyu Watanzania wote kwa ujumla kuja kushiriki maonesho ya SIDO
yatakayobebwa na Kauli Mbiu “Pamoja Tujenge Viwanda Kufikia Uchumi wa
Kati” na kubainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaamini kuwa maonesho hayo
yatakuwa ni maonesho darasa, mahali ambapo watu watajifunza na kufanya
biashara.
Ameongeza kuwa maonesho ya SIDO
yanabeba ajenda ya Serikali ya awamu ya tano na matamanio ya Mhe. Rais ya kuwa
na Tanzania ya Viwanda na kuifikisha nchi katika Uchumi wa Kati, hivyo akaawaalika
wadau wote wenye teknolojia mbalimbali kushiriki maonesho haya.
“Ninawaalika wadau wote wenye
teknolojia mbalimbali waweze kushiriki maonesho haya , nayaalika makampuni,
taasisi na mashirika yenye vitu vinavyoweza kuwafaa wajasiriamali na Watanzania
ambao wangehitaji kuwekeza kwenye viwanda, waweze kuleta teknolojia zao”
“Ninawaaalika Wajasiriamali wote
kushiriki maonesho haya maana yatatoa nafasi kila mjasiriamali kujifunza kwa
mwenzake, kupata elimu na kubadilisha ujuzi ili waweze kuzalisha bidhaa bora
zaidi” alisema Mtaka.
Aidha, ametumia mkutano huo
kuzialika taasisi za fedha ili ziweze kujitangaza kwa wajasiriamali nao wakaona
ni namna gani wanaweza kupata mitaji, huku akisisitiza na kuzialika taasisi za
kitaaluma na vitivo vya uhandisivya Vyuo vikuu pamoja na mashirika mbalimbali ya Kimatifa
yanayofanya kazi hapa nchini.
Akizungumzia ada ya ushiriki
Mtaka amesema wajasiriamali wenye mahitaji maalum watashiriki bure, wajasiriamali
wadogo watashiriki bila kulipia gharama yoyote isipokuwa watalipa shilingi elfu
kumi (10,000/=) kwa ajili ya sare, wajasiriamali
wa kati watachangia shilingi laki mbili (200,000/=) taasisi, makampuni na
mashirika ambayo hayapo katika makundi la wajasiriamali wadogo , wa kati na wadhamni
watatakiwa kuchangia shilingi milioni mbili (2000,000/=) kama ada ya ushiriki.
Kwa upande wa udhamini Mtaka
amesema kuwa kwa taasisi, mashirika au kampuni zilizo tayari kudhamini maonesho
hayo, kiwango cha juu kitakuwa shilingi
milioni thelethini (30,000,000/=), kiwango cha kati shilingi milioni kumi (10,000,000/= ) na kiwango cha chini kitakuwa
milioni tano (5,000,000/=) huku
akisisitiza kuwa wadhamini hawa
watambuliwa kwa vyeti na watapewa kipaumbele cha mgeni rasmi kutembelea mabanda
yao.
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari na
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya
Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja
vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 .
Baadhi
ya waandishi wa habari na Wajumbe wa
Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya
Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya
nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 , wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi
ya na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya
Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja
vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 , wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment