Naibu waziri wa
ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.Angelina Mabula ametoa wito kwa wakazi
wa mkoa wa SIMIYU kutumia fursa za nyumba za makazi zinazotarajiwa kujengwa
katika eneo la Isanga Mjini Bariadi na Shirika la Nyumba la Taifa
Wito huo ameutoa
mkoani Simiyu alipokutana na wadau mbalimbali katika kongamano la ujenzi wa
nyumba za makazi mkoani Simiyu lililohudhuriwa na viongozi wa serikali
mkoani humo wakiongozwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa mkoa wa Simiyu,wakuu
wa wilaya wakurugenzi, makatibu tawala wilaya, wakuu wa idara na watumishi wa
kada mbalimbali kutoka halmashauri zote, wafanyabiashara na viongozi wa vyama
vya wafanyakazi lengo likiwa ni kuangalia aina ya nyumba zitakazojengwa na
Wateja watarajiwa.
Mabula amesema azma ya wizara ya ardhi
,nyumba na maendeleo ya makazi ni kumwezesha kila mtanzania kunufaika na nyumba
zinazojengwa na shirika hilo, huku akisisitiza Taasisi nyingine zinazohusika na
uwekaji wa miundombinu muhimu kuanza utaratibu wa kuweka miundombinu hiyo ili
kuwapunguzia gharama wanunuzi.
“ Tunatarajia taasisi zinazohusika ziwe
zimeshaanza kupeleka huduma huko, wakati NHC wanaanza kujenga nyumba zao pale
gharama itakuwa iko chini kwa sababu hivi vitu vingine vitakuwa vimewekwa na
taasisi nyingine na kazi yao itakuwa ni kurudiisha fedha zao kupitia bili za
umeme, maji”
“Awali nyumba za NHC zilikuwa
zikilalamikiwa kuwa ni za gharama kubwa kutokana na wao kufanya kazi zote wao
wenyewe, ujenzi wa nyumba na uwekaji wa miundombinu ya maji , umeme, barabara,
viwanja vya michezo na huduma nyingine, lakini tunamshukuru Mhe. Rais alishatoa
maelekezo kwa wizara na mamlaka husika kuhakikisha wanaweka miundombinu ya
huduma zote muhimu mahali ambapo NHC wanajenga nyumba zao” alisema.
Wakitoa maoni yao baadhi ya wadau
wametoa ushauri kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuona namna ya kujenga
nyumba zenye gharama nafuu zaidi ili wananchi wengi hususani wale wenye kipato
cha chini waweze kunufaika na mradi huu.
“Ninaiomba
Serikali kuangalia upya gharama za nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la
Nyumba la Taifa(NHC) ili kuwawezesha watumishi na wananchi wengi kumudu gharama
za kununua nyumba hizo kwa kuwa wengi ni wenye vipato vya chini, pia benki
zinazowakopesha wananchi wanaonunua nyumba hizo zitoe mikopo kwa masharti
ambayo hayatawaumiza wakopaji” alisema Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga.
“Ninashauri Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) kuona haja ya kuwa na mpango mkakati wa kuboresha makazi ya wakulima
ambao wamejiunga na Vyama vya Ushirika vya Msingi(AMCOS) ili vyama hivyo, benki
pamoja na NHC waje namna kujenga nyumba
zenye bei nafuu zaidi na kundi kubwa zaidi liweze kunufaika” alisema Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amelipongeza Shirika la Nyumba la
Taifa kwa kuwa chachu ya Maendeleo ya makazi bora nchini, huku akibainisha kuwa
Shirika hilo linaweza kuona namna ya kufanya kazi na Halmashauri mkoani humo
katika kukabiliana na changamoto ya makazi kwa watumishi.
Wakizungumza
katika Kongamano hilo Wawakilishi wa taasisi za fedha zikiwemo Benki za NMB,
CRDB na Azania Bank wamesema wamejipanga
katika utoaji wa mikopo ya nyumba kwa wale walio tayari na wenye vigezo
vinavyotakiwa.
MWISHO
Naibu waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula akizungumza na wadau mbalimbali katika Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wadau mbalimbali katika Kongamano lililohusu
ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi.
Naibu waziri wa Ardhi,
nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(kulia) akiteta jambo na
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka katika Kongamano lililohusu ujenzi wa
nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na
kushirikisha wadau mbalimbali.
Kutoka kushoto Kaimu
Mkurugenzi Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Itandula Gambalagi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka na Naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi,
Mhe. Angelina Mabula wakiteta jambo katika Kongamano lililohusu ujenzi wa
nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na
kushirikisha wadau mbalimbali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt. Sagamiko akichangia hoja
katika Kongamano lililohusu ujenzi wa
nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha
wadau mbalimbali.
Mshauri wa Jeshi la
Akiba Mkoani Simiyu, akichangia hoja katika kongamano lililohusu ujenzi wa
nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na
kushirikisha wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika semina kuhusu ujenzi
wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
katika Mji wa Bariadi, ambayo imefanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na
kushirikisha wadau mbalimbali.
Baadhi ya viongozi na
wadau mbalimmbali mkoani Simiyu wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa
katika kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi mkoani Simiyu, lililofanyika
Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia
hoja katika Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa
kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika
Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mmoja wa Wafanyakazi wa
Benki ya NMB akichangia hoja katika kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba
Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji
wa Bariadi, lililofanyika Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau
mbalimbali.
Meneja wa
Benki ya NMB Bariadi akichangia
hoja katika kongamano lilohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa
na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba
26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mmoja wa Watumishi wa
Benki ya CRDB akiwasilisha mada katika Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa
kujengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika
Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Naibu waziri wa Ardhi,
nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(katikati walioketi) akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mkoa
wa Simiyu baada ya kufungua kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi
zinazotarajiwa kujengwa na Shirika hilo katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba
26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe. Tano Mwera akichangia hoja
katika kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi zinazotarajiwa kujengwa na
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Mji wa Bariadi, lililofanyika Oktoba
26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Naibu waziri wa Ardhi,
nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(katikati walioketi) akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Wakuu
wa Idara Mkoa wa Simiyu baada ya kufungua kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba
Makazi zinazotarajiwa kujengwa na Shirika hilo katika Mji wa Bariadi, lililofanyika
Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
Naibu waziri wa Ardhi,
nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. Angelina Mabula(katikati walioketi) akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na
Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Wilaya na Makatibu Tawala Wasaidizi Mkoa wa
Simiyu, baada ya kufungua Kongamano lililohusu ujenzi wa nyumba Makazi
zinazotarajiwa kujengwa na Shirika hilo katika Mji wa Bariadi, lililofanyika
Oktoba 26, 2018 Mjini Bariadi na kushirikisha wadau mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment