Mkurugenzi wa
Kampuni ya JBS Fuel Company Limited ya Mjini Bariadi, Bi. Lucy Sabu ametoa
msaada chakula na vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona,
katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Bikira Maria
kilichopo Lamadi wilayani Busega.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo Bi. Sabu amevitaja vifaa hivyo kuwa ni pamoja na
Vitakasa mikono, sabuni za maji, ndoo kwa ajili ya maji ya kunawia mikono, mahindi
na sukari vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mbili (2,000,000/=).
Amesema wito
uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli wa maombi ya siku ya tatu umemsukuma kutoa msaada huo kwani ameona ipo
haja ya kuwasaidia wahitaji katika kipindi hiki cha Janga la Corona na kutoa
wito kwa Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya
wataalam wa afya.
"Namshukuru
sana Mhe. Rais kwa maono yake kwa Watanzania kufanya maombi ya siku tatu kumuomba
Mungu atuepushe na Janga la Corona, maombi haya yamenikumbusha kuwakirimu
wahitaji na ndiyo maana nimeguswa kufika katika kituo hiki; nitoe wito kwa
Watanzania wote kuwakumbuka wahitaji katika kipindi hiki cha Janga la
Corona," alisema Bi Lucy Sabu.
Akipokea
msaada huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa
Wilaya ya Busega Mhe. Tano Mwera amemshukuru Bi. Lucy Sabu kwa namna
alivyoguswa kusaidia kituo hicho huku akiendelea kusisitiza wananchi kuchukua
tahadhari na kumwelekeza Mkurugenzi wa kituo kuwa makini kudhibiti watu wanaoingia
kituoni hapo ili kuwalinda watoto.
Naye Mratibu
wa mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona Mkoani Simiyu, Dkt.
Khamis Kulemba ameutaka Uongozi wa kituo hicho kuongeza maeneo ya watoto kunawa
mikono pamoja na kuwasisitiza kunawa mara kwa mara.
Mkurugenzi
wa kituo cha Bikira Maria, Sister Helena Ntambulwa amemshukuru Bi. Lucy
Sabu kwa msaada aliotoa na kuwashukuru viongozi wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa
Simiyu kwa namna wanavyokisaidia kituo hicho chenye jumla ya watoto 71 ambao
wanatoka maeneo mbalimbali ya Tanzania
wakiwemo waliopoteza wazazi na waliotelekezwa.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya
wadhamini ya Kituo hicho, Bw. Belensi China amesema kituo hicho kinakabiliwa na
changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na upungufu wa fedha za kulipa matibabu
ya watoto na mishahara ya wafanyakazi; hivyo amewaomba Watanzania wenye mapenzi
mema kuendelea kuwasaidia watoto hao wenye mahitaji maalum.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera (kushoto) akipokea msaada vifaa wa chakula na vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona uliotolewa na Mkurugenzi wa JBS Fuel Company Limited, Bi. Lucy Sabu (wa pili kulia) kwa kituo cha kulelea watoto wenye ualbino na watoto wenye mahitaji maalumu kilichopo Kata ya Lamadi wilayani Busega, Aprili 22, 2020.
Mkurugenzi wa Kituo cha Bikira Maria kinacholea watoto wenye ulbino na watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Lamadi Busega, Sister Helena Ntabulwa (kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona uliotolewa na Mkurugenzi wa JBS Fuel Company Limited, Bi. Lucy Sabu (wa pili kulia) kwa kituo hicho Aprili 22, 2020.
Mkurugenzi wa JBS Fuel Company Limited, Bi. Lucy Sabu (katikati) akikabidhi msaada wa chakula na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto wenye ualbino na watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Kata ya Lamadi wilayani Busega, Sister Helena Ntabulwa(wa pili kushoto) Aprili 22, 2020 wakishuhudiwa na baaadhi ya watoto hao.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akizungumza kabla ya kupokea msaada wa chakula na vifaa vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona uliotolewa na Mkurugenzi wa JBS Fuel Company Limited, Bi. Lucy Sabu (hayupo pichani) kwa kituo cha kulelea watoto wenye ualbino na watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Kata ya Lamadi wilayani Busega, Aprili 22, 2020.
Mkurugenzi wa JBS Fuel Company Limited, Bi. Lucy Sabu (wa pili kulia) akiangalia mabweni ya watoto katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino na watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Kata ya Lamadi wilayani Busega, kabla ya kukabidhi msaada wa chakula na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona Aprili 22, 2020.
Mkurugenzi wa JBS Fuel Company Limited, Bi. Lucy Sabu (kulia) akionesha baadhi ya vitu alivyotoa msaada katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino na watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Kata ya Lamadi wilayani Busega, kabla ya kukabidhi msaada huo wa chakula na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona Aprili 22, 2020.
Mkurugenzi wa JBS Fuel Company Limited, Bi. Lucy Sabu (kulia) akionesha baadhi ya vitu alivyotoa msaada katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino na watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Kata ya Lamadi wilayani Busega, kabla ya kukabidhi msaada huo wa chakula na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona Aprili 22, 2020.
Mkurugenzi wa JBS Fuel Company Limited, Bi. Lucy Sabu (kulia) akionesha baadhi ya vitu alivyotoa msaada katika kituo cha kulelea watoto wenye ualbino na watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Kata ya Lamadi wilayani Busega, kabla ya kukabidhi msaada huo wa chakula na vifaa vya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona Aprili 22, 2020.
Mkurugenzi wa JBS Fuel
Company Limited, Bi. Lucy Sabu (wa tatu kulia) akiangalia mazingira katika katika kituo
cha kulelea watoto wenye ualbino na watoto wenye mahitaji maalum kilichopo Kata
ya Lamadi wilayani Busega, kabla ya kukabidhi msaada wa chakula na vifaa vya
kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya
Corona Aprili 22, 2020.
0 comments:
Post a Comment