Mkoa wa Simiyu kwa kushirikiana na wadau wa afya umezindua
rasmi kampeni ya kupambana na Maambukizi ya Ugonjwa wa Homa Kali ya mapafu
unaosababishwa na virusi vya Corona kupitia utoaji wa elimu, ambapo Shirika la
Msalaba Mwekundu limeanza kutoka elimu ya tahadhari ya ugonjwa huo katika
Wilaya zote mkoani hapa hususani katika maeneo yenye muingiliano wa watu wengi
kama vile stendi na masoko.
Akizindua kampeni hiyo Aprili 03,2020 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka amelishukuru Shirika la msalaba mwekundu kwa kujitoa kutoa
elimu ya tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona na kuwataka wataalam
watakaotoa elimu hii kuendelea kuwahimiza wananchi kuzingatia maelekezo ya
viongozi na wataalam wa afya ikiwa ni pamoja na kuepuka kupeana mikono, kuzuia
mikusanyiko isiyo ya lazima, matumizi sahihi ya vitakasa mikono na kuhakikisha
wananawa mikono kwa sabuni na maji tiririka.
“Sisi kama mkoa tunawashukuru sana Red Cross(Shirika la
msalaba mwekundu) kwa kuanza kutoa elimu ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi
vya Corona kwa wananchi, elimu hii ni vema ikaenda sambamba na kuwakumbusha
wauzaji wa vitakasa mikono ili waweze kutengeneza vitakasa mikono kwa
kuzingatia taratibu zilizowekwa na wauze kwa bei rafiki ya soko kwa wananchi,”
alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka amehimiza kuwa zoezi la utoaji elimu liende pamoja
na kuwakumbusha wazazi na walezi kuwasimamia watoto wao kuhakikisha kuwa
wanajisomea wakiwa majumbani katika kipindi hiki ambacho shule na vyuo
vimefungwa ili wanafunzi hao waweze kufikia malengo yao hususani wanafunzi
wa madarasa ya mitihani.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa, Dkt. Festo Dugange amesema Mkoa wa
Simiyu umewashirikisha wadau wote wa afya katika kuiandaa jamii kupambana na
maambukizi ya Virusi vya Corona katika utoaji wa elimu ambayo ndiyo kinga, utoaji
wa mafunzo kwa watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya na utoaji
wa vifaa tiba na vifaa kinga lengo likiwa ni kuufanya mkoa wa Simiyu kutopata
maambukizi ya virusi vya Corona.
Kwa upande wake Mratibu wa Mapambano dhidi ya Corona Mkoani
Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba amesema Mkoa wa Simiyu utashirtikiana na wadau
katika kuhakikisha kuwa tahadhari na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi
vya Corona yanafanikiwa.
Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Msalaba Mwekundu
Mkoa wa Simiyu,, Bw. Dismas Kiwale amesema Shirika hilo kwa kushirikianana
watalam wa afya limekusudia kuwafikia wananchi hasa walio ndani zaidi(vijijini)
na kupitia gari lao la matangazo wanatarajia kuzifikia kata zote na halmashauri
zote sita za Mkoa wa Simiyu ambapo watakuwa wakitoa elimu katika maeneo yenye muingiliano wa watu
wengi na kugawa vipeperushi vyenye elimu juu ya tahadhari dhidi ya Corona.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Mhe. Anthony Mtaka
akikabidhi bendera ya Shirika la Msalaba mwekundu kama ishara ya uzinduzi wa
kampeni ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kupitia utoaji wa
elimu kwa wananchi, uzinduzi huo ulifanyika Aprili 03, 2020 katika Viwanja vya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akibandika kipeperushi chenye ujumbe na elimu ya tahadhari dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Corona katika Ubao wa Matangazo katika Ofisi yake mara baada ya kuzindua kampeni ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona uzinduzi huo ulifanyika Aprili 03, 2020 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange akifafanua jambo katika uzinduzi wa kampeni ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kupitia utoaji wa elimu kwa wananchi, uzinduzi huo ulifanyika Aprili 03, 2020 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Mwakilishi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Bw. Dismas Kiwale akifafanua jambo katika uzinduzi wa kampeni ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kupitia utoaji wa elimu kwa wananchi, uzinduzi huo ulifanyika Aprili 03, 2020 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Mratibu wa Mapambano dhidi ya Corona Mkoani Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba akifafanua jambo katika uzinduzi wa kampeni ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kupitia utoaji wa elimu kwa wananchi, uzinduzi huo ulifanyika Aprili 03, 2020 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akibandika kipeperushi chenye ujumbe na elimu ya tahadhari dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Corona katika Ubao wa Matangazo katika Ofisi yake mara baada ya kuzindua kampeni ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona uzinduzi huo ulifanyika Aprili 03, 2020 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu. Mhe. Anthony Mtaka akikabidhi bendera ya Shirika la Msalaba mwekundu kama ishara ya uzinduzi wa kampeni ya mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kupitia utoaji wa elimu kwa wananchi, uzinduzi huo ulifanyika Aprili 03, 2020 katika Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment