Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa umetenga shule za Sekondari
za Bweni za Serikali kuwa maeneo ambayo yatatumika kuwahifadhi washukiwa wa
Virusi vya Corona endapo watapatikana mkoani hapa; baada ya serikali kufunga
shule na vyuo nchini kwa siku 30 lengo likiwa kukabiliana na ugonjwa huo.
Mhe.
Mtaka ameyasema hayo wakati akipokea mchango kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya
shule ya sekondari Anthony Mtaka uliotolewa na umoja
wa Makanisa Lamadi na kuongeza kuwa mbali na maeneo ya shule Mkoa pia umetenga
maeneo ya hoteli ambayo yatatumika endapo washukiwa/watu wanaohisiwa kuwa na
ugonjwa huo ambao hawatahitaji kukaa kwenye maeneo ya shule.
"Mkoa
hautatumia hoteli kwa ajili ya kuhifadhi mtu yeyote atakayeshukiwa kuwa na
maambukizi ya virusi vya corona badala yake tutatumia shule za zetu za
sekondari za bweni lakini ikitokea mtu anahitaji kukaa hotelini tayari
tumeandaa hoteli za kutosha,"alisema Mtaka.
"
Tumechukua uamuzi huu ili kuwapunguzia watakaoshukiwa kuwa na ugonjwa huo
gharama ila utaratibu huu hautawafunga watu wenye uwezo ambao watapenda kwenda
hotelini; kwa mara nyingine tena niwaombe wananchi kuendelea kuchukua tahadhari
na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na viongozi kuzuia maambukizi ya CORONA,"
aliongeza Mtaka
Hata
hivyo aliongeza kuwa tayari kila wilaya imetenga shule yenye vitanda vya
kutosha na mazingira mazuri kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa huo, huku
akiwataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kuchukua tahadhari.
Mbali
na hayo amewataka wazazi wa wanafunzi wa madarasa ya mitihani mkoani humo
kuhakikisha wanawasimamia watoto wao wanajisomea katika wa kipindi hiki ambacho
shule zimefungwa kutokana na ugonjwa huo.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na
wachungaji wa makanisa Lamadi mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya
ujenzi na umoja wa makanisa Kata ya Lamadi kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya
Sekondari Anthony Mtaka
0 comments:
Post a Comment