Umoja
wa makanisa kata ya Lamadi Wilayani Busega umetoa mchango wa vifaa vya ujenzi
vikiwemo mchanga na saruji kwa awamu ya
kwanza kwa.ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika ujenzi wa vyumba vya
madarasa katika Shule ya Sekondari ya Anthony Mtaka iliyopo katika Kijiji cha
Lukungu kata ya Lamadi.
Akipokea
vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewashukuru viongozi
hao kwa kuona umuhimu wa kuchangia katika maendeleo
ya elimu na kuahidi kuendelea kushirikiana na madhehebu ya dini wakati wote.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Busega Tano Mwera aliushukuru Umoja wa Makanisa
ya Kikristo Lamadi kwa mchango wao walioutoa kwa kutambua umuhimu wa kuchangia
miundombinu ya elimu na huku akiyataka madhehebu mengine na jamii kwa ujumla
kuona umuhimu wa jambo hilo.
Naye
mwenyekiti wa makanisa ya kikristo Lamadi, Mchungaji Michael Zacharia
Kaburimoja amesema kuwa waliona umuhimu wa kuchangia miundombinu ya elimu
ambapo wamechangia mchanga tripu 10 na mifuko mitano ya saruji yenye thamani ya
shilingi laki saba.
"Umoja
wetu una jumla ya makanisa 30 ila yaliyoridhia kuchanga ni 21 na kila kanisa
linamchango wake na kila tunapopokea michango tunaiwasilisha na hatujaishia
hapa bado makanisa yanaendelea kuchanga," alisema Mchungaji kaburimoja
Awali
akisoma taarifa kwa niaba ya wachungaji wa makanisa hayo yaliyotoa mchango Mchungaji
Emmanuel Edward Fyita kutoka Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)
ameiomba serikali kuona uwezekano wa kuipandisha hadhi ya shule ya sekondari
Lamadi kutoka kidato cha nne hadi cha sita kutokana na ongezeko la wanafunzi wa
kidato kwanza hadi cha nne kwenye kata hiyo.
Aidha,
wameiomba serikali kuanzisha shule nyingine ya sekondari katika eneo la shule
ya msingi lamadi ambapo bado kuna eneo kubwa lengo likiwa kuwapunguzia wanafunzi
kutembea umbali mrefu.
"Kuna
wanafunzi wanaotoka vijiji vya mbali kama mwabasabi na Mwabulugu kwenda Lukungu
waishie hapa lamadi badala ya kutembea mwendo mrefu na ujenzi huu utasaidia
kukabiliana na ongezeko kubwa la wanafunzi katika shule zetu zilizo ndani ya
kata ya Lamadi kwa sasa" alisema mchungaji Fyita.
"Wachungaji
tulio katika umoja huu tunakuahidi kuonesha njia kwa kujenga angalau chumba
kimoja cha darasa," aliongeza mchungaji Fyita.
MWISHO
Mwenyekiti
wa makanisa Lamadi, Mchungaji Michael Zacharia Kaburimoja (kushoto) akitoa
maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kuwasili
katika Shule ya Sekondari Anthony Mtaka, wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika
shule hiyo uliotolewa na Umoja wa Makanisa Lamadi Machi 31, 2020.Mmoja wa Wachungaji akitoa sala wmara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Viongozi wa Wilaya ya Busega mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Anthony Mtaka wakati wa wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule hiyo uliotolewa na Umoja wa Makanisa Lamadi Machi 31, 2020.
Mwenyekiti wa makanisa Lamadi, Mchungaji Michael Zacharia Kaburimoja (kushoto) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Anthony Mtaka wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule hiyo uliotolewa na Umoja wa Makanisa Lamadi Machi 31, 2020.
Mwenyekiti wa makanisa Lamadi, Mchungaji Michael Zacharia Kaburimoja (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Anthony Mtaka wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule hiyo uliotolewa na Umoja wa Makanisa Lamadi Machi 31, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akieleza jambo mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Anthony Mtaka wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika shule hiyo uliotolewa na Umoja wa Makanisa Lamadi Machi 31, 2020.
Mwenyekiti
wa makanisa Lamadi, Mchungaji Michael Zacharia Kaburimoja (kushoto) akitoa
maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kuwasili
katika Shule ya Sekondari Anthony Mtaka, wakati wa makabidhiano ya msaada wa vifaa vya ujenzi wa madarasa katika
shule hiyo uliotolewa na Umoja wa Makanisa Lamadi Machi 31, 2020.
0 comments:
Post a Comment