Monday, April 6, 2020

KAMATI YA USHAURI YA MKOA SIMIYU YARIDHIA KUHAMISHWA KWA KATA, VIJIJI BARIADI, ITILIMA

Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu imeridhia kata za Itubukilo na Sakwe kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kuhamishiwa Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Kijiji cha Giriku kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuhamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma karibu na makao makuu ya Halmashauri hizo.

Maamuzi haya ni utekelezaji wa maagizo ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo yalitolewa kwa Halmashauri zote nchini kuhamisha Kata na vijiji ambavyo wananchi wake wanavuka makao makuu ya Halmashauri moja kwenda kupata huduma katika makao makuu ya Halmashauri zao ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.
Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema RCC imefikia maamuzi haya baada ya kupokea mapendekezo ambayo yamefikiwa katika vikao halali vya Halmashauri na kamati za ushauri za wilaya (DCC).
Aidha, katika kikao hicho mwakilishi wa Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021 wakala huo umetenga fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Barabara zinazounganisha Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na makao makuu ya Halmashauri hiyo yaliyopo kata ya Dutwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao maalum cha Kamati hiyo kilichofanyika April 01, 2020 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao maalum cha Kamati hiyo kilichofanyika April 01, 2020 Mjini Bariadi. 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akiwasilisha taarifa katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Aprili 01, 2020.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg. Enock Yakobo akichangia hoja  katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Aprili 01, 2020.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao maalum cha Kamati hiyo kilichofanyika April 01, 2020 Mjini Bariadi. 

 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao maalum cha Kamati hiyo kilichofanyika April 01, 2020 Mjini Bariadi. 

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akifungua kikao maalum cha Kamati hiyo kilichofanyika April 01, 2020 Mjini Bariadi. 

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!