Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka leo ameshiriki ibada ya Pasaka katika
makanisa tofauti mjini Bariadi na kuwasisitiza waumini na wananchi wote wa Mkoa
wa Simiyu kutulia, kuepuka safari zisizo za lazima na kuendelea kuchukua
tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa
na Serikali.
Mtaka ameyasema hayo
kwa nyakati tofauti wakati akitoa salamu za Pasaka za Mkoa aliposhiriki ibada
katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu John, Parokia ya Mtakatifu Luka,
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Bariadi Mjini na Kanisa la
Africa Inland Church of Tanzania (AICT) leo Aprili 12, 2020.
“Nimeona watu wananawa mikono
utaratibu huu usiishie kwenye nyumba za ibada na maeneo ya kutolea huduma, uende
mpaka nyumbani,tunapokuwa kwenye nyumba za ibada pia tuzingatie umbali katika
ukaaji wetu na wakati wa kupokea huduma za kiroho: pasaka hii tutulie majumbani
tuepuke safari zisizo lazima na tufuate maelekezo ya Serikali.” alisema Mtaka.
Aidha, pamoja na
kuwasisitiza wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima Mtaka ametoa wito kwa
jamii kuona namna ya kuwasaidia zaidi wazee, watoto na watu wenye magonjwa yasiyoambukiza kama
kisukari na shinikizo la damu kuepuka zaidi mikusanyiko hiyo ili kuwaondolea
hatari ya kupata maambukizi kutokana na hali ya kinga zao za mwili.
Katika hatua nyingine
Mtaka amewataka wazazi kuwasimamia watoto wao kujisomea kwa bidii kipindi hiki
ambacho shule zimefungwa kutokana na tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya
Corona hususani wale wa madarasa ya Mitihani ya Kitaifa kwa kuwa mitihani hiyo
bado ipo na itafanyika.
Sambamba na hayo Mtaka
amewaasa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kutunza chakula ambacho kimepatikana mwaka
huu na kutokiuza kwa matumizi ambayo si ya lazima hususani katika kipindi hiki ambacho
chakula kinauzwa kwa bei ya chini huku akiwasisitiza kujiunga na Bima ya Afya
na Mfuko wa Afya ya Jamii ili waweze kupata unafuu katika huduma za matibabu.
Kwa upande wao viongozi
wa makanisa akiwemo Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu John, Peter Mkunya,
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Luka, Martine Jilala, Mchungaji wa KKKT Bariadi,
Greyson Kinyaha na Mchungaji wa AICT, Amosi Ndaki wamesema wametumia Maadhimisho
ya Kufufuka kwa Yesu Kristo(Pasaka) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na Janga
la Corona na kuendelea kuwakumbusha waumini kuzingatia maelekezo ya viongozi wa
Serikali na wataalam wa afya.
Koga
Mihama na George Lyimo ni miongoni mwa waumini waliohudhuria ibada ya pasaka
wameishukuru Serikali kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa kujikinga na
Maambukizi ya CORONA huku wakitoa wito kwa wananchi wote kufuata maelekezo
yanayotolewa na Serikali ili Maambukizi ya Virusi vya Corona yaishe nchini
Tanzania.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waumini
wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi Mjini (hawapo
pichani), wakati alipofika kanisani hapo kutoa salamu za Pasaka kwa waumini hao
leo Aprili 12, 2020 kushoto ni Mchungaji wa Kanisa hilo, Greyson Kinyaha na
kulia ni Mchungaji Sarah Kimaro.
Baadhi ya waumini wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi Mjini
wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati alipofika kanisani hapo kutoa salamu
za Pasaka kwa waumini hao leo Aprili 12, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akipokea ekaristi takatifu katika misa takatifu Kanisa
Katoliki Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Mjini, wakati aliposhiriki katika
misa hiyo na kutoa salamu za pasaka kwa waumini wa Kanisa hilo waumini hao leo
Aprili 12, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waumini
wa Kanisa la Africa Inland Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini wakati alipofika
kanisani hapo kutoa salamu za Pasaka kwa waumini hao leo Aprili 12, 2020.
Paroko
Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Mjini,Peter Mkunya akitoa
mahubisri ya neno la Mungu katika misa Takatifu leo Aprili 12, 2020.
Waimbaji wa Kwaya ya
Uinjilisti katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Usharika wa Bariadi
Mjini wakiimba wakati wa ibada ya kwanza
leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshiriki
katika ibada hiyo na kutoa salamu za pasaka kwa waumini na wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akinawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara baada ya
kuwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Bariadi Mjini
ambapo ameshiriki ibada ya Pasaka na kutoa salamu za Pasaka za Mkoa leo Aprili
12, 2020 kwa waumini wa Kanisa hilo. Waimbaji wa Kwaya kutoka Kanisa la Africa Inland Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini wakiimba wakati wa ibada leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshiriki katika ibada hiyo na kutoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa kanisa hilo.
Mchungaji wa Kanisa la Africa Inland Church of Tanzania(AICT) Bariadi Mjini, Amosi Ndaki akitoa mahubiri ya neno la Mungu wakati wa ibada leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshiriki katika ibada hiyo na kutoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa kanisa hilo.
Kwaya ya Mtakatifu Johh kutoka Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Mjini wakiimba wakati wa misa takatifu leo Aprili 12, 2020 kuadhimisha Siku ya Pasaka ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshiriki katika misa hiyo na kutoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa kanisa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye suti nyeusi katikati ) akiwa katika misa na waumini wengine wa Kanisa la Mtakatifu Luka Mjini Bariadi leo Aprili 12, 2020 ambapo ametoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini wa Kanisa hilo.
Baadhi ya wanakwaya na Waumini wa Kanisa la Mtakatifu Luka Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akitoa salamu za Pasaka za Mkoa kwa waumini wa kanisa hilo leo Aprili 12, 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akiagana na baadhi ya viongozi waandamizi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania,
Usharika wa Bariadi Mjini mara baada ya kushiriki katika ibada ya Pasaka
kanisani hapo na kutoa salamu za pasaka za mkoa kwa waumini leo Aprili 12, 2020.
0 comments:
Post a Comment