Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema kuwa
jumla ya watu 34 kati ya watu 120 waliokuwa kwenye uangalizi maalum (Karantini)
mkoani Simiyu wameruhusiwa mara baada ya kupimwa na kukutwa hawana maambukizi
ya Virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu (COVID-19).
Mtaka ameyasema hayo Aprili 18, 2020 wakati
akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Bariadi Mjini, ambao
wameitikia
wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
kwa Watanzania kuingia katika maombi ya siku tatu (Aprili 17-19, 2020) kuliombea
Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
“Tulikuwa na watu 120
waliokuwa chini ya uangalizi ambao pia wamekuwa wakipata elimu kuhusu maambukizi
ya virusi vya Corona ili wakitoka wakawe msaada kwa familia zao; mpaka sasa
watu 34 wameruhusiwa baada ya kupimwa na kuthibitika kwamba hawana maambukizi
ya Corona, sisi kama mkoa tunaendelea kuchukua tahadhari zote,”alisema Mtaka.
Ameongeza kuwa waliowekwa
karantini ni pamoja na wanaofanya biashara nchi jirani ambao waliomba wenyewe ili
wajitenge na familia zao; pia wapo baadhi ambao familia ziliomba Serikali
iwaweke kutokana na kujua kuwa wametoka nchi zenye maambukizi kwa hofu ya
kupeleka maambukizi kwa familia zao ikiwa itatokea wameambukizwa virusi vya
Corona.
Aidha, Mtaka amesema kuwa mpaka sasa mkoa wa
Simiyu hauna mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Corona na kutoa wito kwa
wananchi kuendelea kuchukua tahadhari huku wakimuomba Mungu bila kukoma ili aliponye
Taifa na janga la kidunia la ugonjwa wa COVID 19.
Katika hatua nyingine Mtaka
amewahimiza wazazi kuwasimamia watoto wao na kuhakikisha wanajisomea wakiwa
nyumbani huku akiwaasa kutunza chakula na kuepuka kuuza mazao pasipo na ulazima
wa kufanya hivyo.
Mchungaji wa Kanisa la SDA
Bariadi Mjini, Marco Mlingwa amesema Kanisa hilo limepokea maelekezo ya Serikali
na linaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli kuliombea Taifa Mungu aliponye na janga la Corona.
Kwa upande wao waumini
wa Kanisa la SDA Bariadi Mjini wamemshukuru Mhe. Rais kuruhusu ibada kufanyika
kwa kuzingatia maelekezo ya watalaam wa afya na kubainisha kuwa wataendelea
kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Corona wakiamini kuwa Mungu atasikia wakiomba
kwa imani na kwa bidii.
“Tunamshukuru Mhe. Rais
kuruhusu ibada kuendelea kufanyika huku tukichukua tahadhari, sisi Wakristo tunaamini watu tukiomba kwa
bidii Mungu anasikia maombi, hivyo tukikutana na kuomba kwa bidii Mungu
atasikia na kutuokoa na ugonjwa huu wa COVID 19,” alisema Paul Jidayi muumini
SDA na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa.
“Sisi kama Wasabato
tuna vipindi vyetu vya afya na kupitia vipindi hivyo tumeshajifunza na kuchukua
tahadhari dhidi ya Corona kanisani na majumbani; pia tunaungana na Rais
kuliombea Taifa tukiamini kuwa Mungu atatusikia maana hata zamani, nchi ya Ninawi
walipelekewa taarifa kuwa wataangamizwa lakini walipomlilia Mungu aliwasikia na
hawakuangamia,” alisema Mariam Manyangu.
MWISHO
Baadhi ya Wazee wa
Kanisa wa Kanisa la SDA Bariadi mjini wakiwaongoza waumini wa kanisa hilo
katika maombi maalum ya kuliombea Taifa, yaliyofanyika katika ibada Aprili 18,
2020 kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili
17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.(mwenye Tai
wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 ambapo ameshiriki katika ibada ambayo waumini
hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John
Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili
17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Baadhi ya waumini wa
Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambapo ameshiriki ibada ambayo
waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania
wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa
ili Mungu aliponye na janga la Corona.Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini wakiimba katika ibada ya Aprili 18, 2020 ambayo waumini wa kanisa hilo pia wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Marco Mlingwa akiwaongoza waumini wa kanisa hilo katika maombi maalum ya kuliombea Taifa, yaliyofanyika katika ibada Aprili 18, 2020 kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.(wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka).
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye tai katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Kanisa la waumini wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambapo ameshiriki ibada ambayo waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) na Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Marco Mlingwa wakiwa katika maombi kwenye ibada ambayo waumini wa Kanisa hilo wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Marco Mlingwa akihubiri katika ibada ya Aprili 18, 2020 ambayo waumini wa kanisa hilo pia wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Vijana wa Pathfinder katika Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini wakiimba katika ibada ya Aprili 18, 2020 ambayo waumini wa kanisa hilo pia wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambapo ameshiriki ibada ambayo waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Baadhi ya waumini wa
Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambapo ameshiriki ibada ambayo
waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania
wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa
ili Mungu aliponye na janga la Corona.
0 comments:
Post a Comment