Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga ameutaka uongozi wa Wilaya ya Maswa
kumsimamia Mkandarasi SUMA JKT anayejenga kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio wilayani humo ili
akamilishe ujenzi wa viwanda hivyo kwa wakati ili vianze uzalishaji.
Nyamhanga ameyasema
hayo wakati wa ziara yake alipotembelea kuona maendeleo ya ujenzi wa viwanda
hivyo eneo la Ng’hami ambapo ameutaka uongozi wa Wilaya ya Maswa kufuatilia
uagizaji wa mitambo ya kiwanda cha chaki huku akiahidi kuwa ofisi yake itafuatilia
kibali cha kuagiza Mitambo kwa ajili ya kiwanda cha vifungashio. katika Ofisi
ya HAZINA(Wizara ya Fedha)ili miradi yote iende sambamba.
0 comments:
Post a Comment