Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amekemea
tabia ya baadhi ya viongozi kuwapa ndugu au jamaa zao zabuni za ujenzi wa
miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo miradi ya maji kwa kuwa ni kinyume cha
taratibu na hali hiyo haiwatendei haki wananchi na Serikali.
Mhe.Makamu
wa Rais aliyasema hayo jana katika kikao cha majumuisho alichokifanya mara
baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku nne mkoani humo ambayo aliianza tarehe
19/02/2018.
Amesema
miradi mingi hususani miradi ya maji katika maeneo mengi mkoani humo
haitekelezwi kwa wakati na katika kiwango cha ubora unaotakiwa kwa kuwa baadhi
ya viongozi wamekuwa wakipeana miradi hiyo kwa kuzingatia undugu/ ukaribu wao
badala ya kuangalia sifa zinazotakiwa.
“Miradi
mingi ya maji imeshindwa kwenye baadhi ya maeneo kwa sababu mmepeana kindugu
ndugu, mnashindwa kukemeana mnashindwa kusimamiana miradi haiendi, msiwadhulumu
wananchi haki yao; mlizoea huko nyuma mnachukua fedha za miradi na hamfanyi
lakini siyo sasa hivi” alisema.
Mhe.Makamu
wa Rais aliwaagiza Wakuu wa Wilaya kuwasilisha taarifa yenye orodha ya miradi inayotekelezwa katika maeneo yao, mtu
anayetekeleza, hatua iliyofikia, tarehe ya kumaliza mradi na ikiwa
haijamalizika ioneshwe sababu za kutokamilisha miradi hiyo kwa wakati, lengo
likiwa ni kutoa nafasi kwa vyombo vya dola kufanya kazi yake.
Aidha,
amevitaka vyombo vya dola ikiwemo
Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kufuatilia Miradi mbalimbali
ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri zote mkoani humo.
Sanjali
na hilo Mhe.Makamu wa Rais amewataka viongozi mkoani Simiyu kufanya kazi kwa
kushirikiana ili kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao.
Wakati
huo Mhe.Makamu wa Rais amewapongea viongozi na wananchi Mkoani Simiyu kwa kufanya
vizuri katika sekta ya Kilimo hususani Kilimo cha zao la pamba na akaahidi kuwa
Serikali itahakikisha wakulima wanapata dawa za kuuwa wadudu waharibifu ili
malengo ya kuongeza mavuno mwaka huu kufikia kilo milioni 300 yaweze kutimia.
Vile
vile amewapongeza kwa kutekeleza Sera ya Tanzania ya Viwanda kwa kuanzisha
viwanda katika maeneo mbalimbali kupitia Mkakati wa “Wilaya moja Bidhaa moja” ambapo
amesema Serikali inakusudia kujenga Kiwanda cha Bidhaa za Afya zitokanazo na
pamba (Bariadi) na Maji wanayotundikiwa wagonjwa(IV Fluid/Drip) katika wilaya
ya Busega.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehitimisha ziara yake jana Mkoani
Simiyu ambapo alikuwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya 34 ya Chuo kikuu Huria cha
Tanzania yaliyofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu katika kikao
cha majumuisho ya ziara yake ya siku nne aliyoianza tarehe 19/02/2018 hadi
22/02/2018 mkoani humo
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu(waliokaa mbele)
pamoja na viongzoi wengine wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani)katika kikao cha
majumuisho ya ziara yake ya siku nne aliyoianza tarehe 19/02/2018 hadi
22/02/2018 mkoani humo
Baadhi ya Viongozi wa Chama Tawala na Serikali mkoani
Simiyu wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Samia Suluhu Hassan(hayupo pichani) katika kikao cha majumuisho ya ziara
yake ya siku nne aliyoianza tarehe 19/02/2018 hadi 22/02/2018 mkoani humo
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Serikali Mkoani Simiyu
wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia
Suluhu Hassan(hayupo pichani) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku
nne aliyoianza tarehe 19/02/2018 hadi 22/02/2018 mkoani humo
Baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Serikali Mkoani Simiyu
wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia
Suluhu Hassan(hayupo pichani) katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku
nne aliyoianza tarehe 19/02/2018 hadi 22/02/2018 mkoani humo
0 comments:
Post a Comment