Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amemuagiza Mkandarasi
wa Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa yenye urefu wa Kilomita 49.7
kukamilisha mradi huo Juni 2019.
Waziri Mbarawa amesema hayo wakati alipotembelea Kambi ya Mkandarasi CHICCO
anayetekeleza Mradi huo iliyopo kata ya Luguru wilayani Itilima wakati wa Ziara yake Mkoani Simiyu .
Amesema barabara
hiyo iliyopangwa kujengwa kwa miezi 24 kuanzia Mwezi Oktoba 2017, itajengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 86.9
na tayari Serikali imeshamlipa Mkandarasi shilingi Bilioni 8.9.
Amemuelekeza
Mkandarasi CHICCO kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo na kuahidi kuwa Serikali itamsimamia na
kuhakikisha mradi huo unakamilika mwezi Juni 2019, jambo ambalo limekubaliwa na
Mkandarasi huyo.
“Tutahakikisha
tunamsimamia Mkandarasi masaa yote usiku
na mchana ili barabara hii imalizike kwa wakati na tutamlipa fedha kila
anapoleta ‘certicate’ kazi hii isisimame tena, nawaagiza TANROADS na Mkandarasi
Mshauri kusimamia barabara hii ili thamani ya fedha ionekane” alisema Mbarawa.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi aliyoitoa mwezi Januari 2017 katika
ziara yake Mkoani humo, ambapo amebainisha kuwa kukamilika kwa barabara hiyo
kutaufungua Mkoa huo kibiashara.
Naye Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ameshukuru juhudi zinazofanywa na
Serikali kwa mkoa huo kwa kuwa ulipoanzaishwa mwaka 2012 barabara zilikuwa
zinapitika kwa shida, lakini sasa
wananchi wanatumia muda mfupi kwenda maeneo mbalimbali, hivyo amesema barabara
hiyo itakapokamilika nayo itachangia kurahisisha usafirishaji.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti wananchi wa Kijiji cha Banya wilayani Itilima mahali inapojengwa
Kambi ya Mkandarasi CHICCO wamelalamikia suala la mkandarasi kuchukua vibarua
wa kufanya kazi za mradi nje ya Mkoa pamoja na malipo yasiyoridhisha kwa wale waliopata nafasi ya kufanya kazi
katika mradi huo.
“Mhe. Waziri hivi ni
sahihi kweli barabara ijengwe hapa kwetu halafu vibarua watoke mikoa mingine , mimi naona siyo sawa tunaomba
Serikali itusaidie na sisi wananchi wa hapa tupate kazi; pia hata hawa
wanaofanya kazi hapa malipo ni kidogo elfu tano kwa siku haitoshi” alisema
Samweli Jisena.
Waziri Mbarawa
amemuagiza Meneja wa TANROADS Mkoa wa Simiyu, Mhandisi.Albert Kent kuhakikisha
kuwa anasimamia suala la wananchi wa eneo la mradi kupewa kazi na mkandarasi na
upande malipo amewataka wafanyakazi kukubaliana na mkandarasi juu ya malipo
yao.
Ujenzi wa
Barabara ya Bariadi-Maswa ni ahadi ya Rais wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli aliyoitoa Januari 11, 2017 akiwa katika ziara yake ya siku mbili
mkoani Simiyu mara baada ya kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi yenye urefu wa
Kilomita 71.8 mjini Bariadi.
Meneja wa TANROADS Mkoa
wa Simiyu, Mhandisi.Albert Kent akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(wa pili kushoto, alipotembelea eneo la ujenzi wa Kambi ya Mkandarasi
CHICCO anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi- Maswa wakati wa
ziara yake Mkoani Simiyu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi
CHICCO anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi- Maswa wakati wa
ziara yake Mkoani Simiyu.
Mjumbe wa Halmashuri
Kuu ya CCM (NEC), Gungu Silanga akieleza juu Ujenzi wa mradi wa barabara ya
Bariadi-Maswa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa wakati wa ziara yake katika eneo
la ujenzi wa Kambi ya Mkandarasi CHICCO anayetekeleza mradi huo Mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe.Enock Yakobo(kulia)akieleza juu ya Ujenzi wa mradi wa barabara ya
Bariadi-Maswa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa wakati wa ziara yake katika eneo
la ujenzi wa Kambi ya Mkandarasi CHICCO anayetekeleza mradi huo Mkoani Simiyu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza Samweli Jisena mwananchi kutoka Kata ya Luguru akitoa malalamiko yake, wakati alipotembelea
eneo la ujenzi wa Kambi ya Mkandarasi CHICCO
anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi- Maswa Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe.Benson Kilangi (kushoto) akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika eneo la ujenzi wa Kambi ya Mkandarasi CHICCO
anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bariadi- Maswa Mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment