Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi
mkoani Simiyu kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu ili kuunga mkono
jitihada za Serikali katika maendeleo ya Sekta ya Elimu.
Mhe.Makamu wa Rais
ameyasema hayo wakati akizungumza na
Wananchi wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa
Nguzo Nane wakati wa ziara yake mkoani humo.
Amesema
Serikali imeamua kutoa elimu bila malipo na kuwapunguzia wazazi mzigo wa
kulipia gharama za karo na michango mbalimbali ya uendeshaji wa shule lakini
suala la kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu wananchi wanapaswa kuunga
kuchangia ili kuunga mkono juhudi hizo.
“
Tunapeleka fedha katika shule zote za Msingi na Sekondari ili wanafunzi waweze
kusoma vizuri lakini kwenye suala la ujenzi wa matundu ya vyoo, madarasa, maabara
pamoja na kwamba Serikali ina wajibu wa kufanya hayo na ninyi wananchi mnao
wajibu wa kusaidia kufanya hayo” alisema Mhe. Makamu wa Rais.
Wakati
huo huo Mhe.Makamu wa Rais ameipongeza Wilaya ya Maswa kwa kuongeza ufaulu
kutoka asilimia 45 hadi asilimia 75 kwa mwaka 2017 na akakemea vikali tabia ya
wanaume wanaoua ndoto za watoto wa kike kwa kuwapa mimba , ambapo amesema jicho
la Serikali liko kwa watoto wa kike na itawachukulia hatua kali wote
watakaobainika kufanya hivyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt.Seif Shekalaghe amesema watoto wa kike
28 wameripotiwa kuwa na mimba katika kipindi cha mwezi Desemba 2017 hadi sasa na
Serikali ya Wilaya kupitia Operesheni tokomeza Mimba imefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa 15 na kati ya hao wawili wamehukumiwa miaka 30 jela kila mmoja.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Madini , Mhe.Stanslaus Nyogo amewashukuru viongozi wa Wilaya kuleta
mafanikio katika elimu ikiwa ni pamoja na ongezeko la ufaulu.
Katika
hatua nyingine Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia
Suluhu Hassan mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Upasuaji Hospitali ya
Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING
THEATER” amewataka Watumishi wa Afya kufanya kazi kwa bidii
Aidha,
amesema Serikali itahakikisha inaboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na
ujenzi wa vituo vya Afya katika kila kata na kuboresha huduma za Afya ya Mama
na Mtoto ili kupunguza Vifo vya mama na mtoto.
Naye
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Josephat Kandege amesema Serikali
imekusudia kujenga vituo vya Afya 286 kufikia mwisho mwa mwaka 2017/2018 lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa huduma za
afya kwa kupunguza mrundikano wa wagonjwa katika Hospitali za Wilaya.
Mbunge
wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mhe.Mashimba Ndaki amesema pamoja na kuendelea
kuboresha sekta ya Afya kwa kujenga miundombinu, ni vema Serikali ikaajiri
watumishi wa Idara ya Afya kukabiliana na upungufu uliopo.
Mhe.Makamu
wa Rais amemaliza Ziara yake Wilayani Maswa ambapo amefungua Jengo la Upasuaji
la Upasuaji Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA
SULUHU HASSAN OPERATING THEATER” na kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa
Nguzo Nane.
MWISHO
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akimwagilia mti wa
mwembe alioupanda mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Hospitali ya
Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING
THEATER” wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na
wananchi wa Wilaya ya Maswa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja
wa Nguzo nane Mjini Maswa, wakati wa ziara yake wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la
Maswa Mashariki, Mhe.Stanslaus Nyogo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini
akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia
Suluhu Hassan wakati alipokuwa akikagua Jengo la Upasuaji la Hospitali ya
Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING
THEATER” mara baada ya kulifungua wilayani humo.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akikagua Hospitali ya
Wilaya ya Maswa mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Hospitali ya Wilaya
ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING THEATER”
wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, (kulia mwenye miwani) Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Dkt.Seif Shekalaghe akimuongoza.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan(katikati) akia katika
picha ya pamoja na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya maswa na Mkoa wa
Simiyu mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Hospitali ya Wilaya ya Maswa
ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING THEATER” wakati wa
ziara yake wilayani Maswa.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiagana na wananchi
wa Wilaya ya Maswa mara baada ya mkutano wa Hadhara uliofanyika Uwanja wa Nguzo
Nane mjini Maswa.
Mbunge wa Jimbo la
Maswa Mashariki ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini , Mhe.Stanslaus Nyogo, akizungumza
na wananchi wa Wilaya ya Maswa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika katika
uwanja wa Nguzo nane Mjini Maswa, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan wilayani humo
Mbunge
wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mhe.Mashimba Ndaki, akizungumza na
wananchi wa Wilaya ya Maswa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja
wa Nguzo nane Mjini Maswa, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment