Mkoa
wa Simiyu umejipanga kimkakati katika
kuhakikisha unaongeza ufaulu kwenye Elimu na kuwa miongoni mwa mikoa
inayofanya vizuri Kitaifa kutoka mahali ulipo sasa, kwenda kwenye nafasi ya tarakimu moja(single
digit) yaani nafasi ya kwanza hadi ya tisa.
Hayo
yalibainishwa katika kikao maalum kilichofanyika jana Mjini Bariadi kati ya Viongozi
na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri)
ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa
mwaka 2017, kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini amewataka walimu pamoja na watendaji
wengine wa idara ya Elimu kuongeza bidii katika maeneo yao ili waweze
kuufikisha mkoa katika nafasi ya tarakimu moja (single digit) kwa kuwa sababu,
uwezo na nia ya kufika hapo ipo.
“Watu
wa Sekta ya elimu Ombi langu kwenu wakati tukiwa tunajipongeza kuwa wa 14
katika mtihani wa kidato cha nne mwaka 2017 tudhamirie kuongeza bidii ili
tuingia kwenye ‘single digit’, sababu za kuingia kwenye ‘single digit’ zipo,
uwezo upo kwa kuwa ninyi mpo na nia ya Simiyu kuonekana juu tunayo” alisema
Sagini.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema miongoni mwa mambo yatakayofanya mkoa huo
kuendelea kufanya vizuri ni pamoja na kuendeleza makambi kwa wanafunzi wa
madarasa ya mitihani ambayo yatasaidia kuwaandaa vema na Mitihani ya Taifa.
Aidha,
Mtaka amesema mkoa huo umeandaa Mpango Mkakati wa TEHAMA ambayo katika sekta ya
elimu itasaidia kutekeleza mpango wa madarasa ya mitihani kusoma kwa kupitia
mitandao na tayari umepokea kompyuta 60 kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi ambazo zitaweka katika shule zenye mifumo ya
TEHAMA ili kuwezesha mpango huo.
Wakati
huo huo Mtaka amesisitiza juu ya eneo la umuhimu wa chakula kwa wanafunzi ambapo
amemuagiza Afisa Elimu Mkoa kuitisha kikao cha Wenyeviti wa Kamati za Shule, waweze
kuzungumza namna ya nzuri ya kuwawezesha wanafunzi kula chakula wawapo shuleni,
ili wasome vizuri baadaye waweze kufanya vizuri katika masomo yao..
“
Kama tunataka kuwa mkoa bora na kushindana kwenye elimu wazazi wakubali
kuchangia chakula ili watoto wale shuleni, nitakaa na wazazi niwaambie ukweli
watoe sehemu ya chakula cha nyumbani kije shuleni na waweke utaratibu wa kuwapikia watoto ili
wale shuleni” alisema Mtaka.
Kwa
upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory alisema uwezo wa
mkoa huo kufikia nafasi ya tarakimu
moja(single digit) upo kwa kuwa, tangu mkoa huo ulipoanzishwa mwaka 2012
umekuwa ukifanya vizuri hususani katika Mtihani wa Kidato cha Nne, ambapo
ulitoka katika nafasi ya 17, nafasi ya 14
miaka miwili mfululizo na kufikia nafasi ya 11 mwaka 2017.
Nao
baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa shule walisema ili kufikia azma ya Mkoa huo
kushika nafasi ya tarakimu moja yaani nafasi ya kwanza hadi ya tisa(single
digit) wamejipanga katika kusimamia mipango mkakati ya shule zao, kuendeleza mazoezi
ya mara kwa mara, kuongeza ushirikiano na wazazi, kufautilia ratiba na
kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
“Kilichonisaidia
mpaka shule yangu ikawa ya pili kimkoa katika mtihani wa darasa la nne ni
ushirikiano na wazazi, mitihani ya ujirani mwema, watoto kula chakula cha mchana
shuleni pamoja na kuhakikisha walimu wanafuata ratiba ya masomo” alisema Joseph
Kasoka Mwalimu Mkuu Shule ya msingi Halawa wilayani Bariadi.
Kikao
cha watendaji wa Idara ya Elimu kiliwahusisha Maafisa Elimu wa Wilaya, Wadhiti
Ubora wa Elimu, Waratibu wa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu na baadhi
ya Walimu waliofanya vizuri katika masomo yao kwenye Mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, lengo likiwa
nikutambua juhudi zilizofanyika kwa mwaka 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya,
Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye
Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao kilichofanyika jana Mjini
Bariadi.
Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya
Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika
masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao
kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Afisa
Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na Watendaji wa Idara
ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na baadhi ya walimu (mahiri) ambao
walifanya vizuri katika masomo yako kwenye Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka
2017, katika kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi..
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Mwasubuya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambayo
ilikuwa ya kwanza Kimkoa katika Mtihani wa Darasa la Nne 2017 akieleza uzoefu
wake mbele ya walimu wenzake na viongozi wa idara ya elimu, katika kikao
kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Ndg.Abdallah Malela akizungumza
na Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na
baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye
Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, katika kikao kilichofanyika jana
Mjini Bariadi.
Mwalimu
Aron Kiunsi wa Shule ya Sekondari Bariadi akipokea Cheti kutoka kwa Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka kama mwalimu mahiri wa somo la Kiingereza
katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2017, katika kikao cha viongozi
na watendaji wa Elimu kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na walimu mahiri kwenye masomo mbalimbali katika Mitihani ya Kitaifa
mwaka 2017 mara baada ya kikao cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu
ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na walimu hao, kumalizika jana mjini Bariadi.
Baadhi
ya Viongozi na Watendaji wa Idara ya Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na
baadhi ya walimu (mahiri) ambao walifanya vizuri katika masomo yako kwenye
Matokeo ya mitihani ya Kitaifa mwaka 2017, wakifuatilia masuala mbalimbali
katika kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini(wa nne kushoto mbele) akiwa katika
picha ya pamoja na walimu mahiri kwenye masomo mbalimbali katika Mitihani ya
Kitaifa mwaka 2017 mara baada ya kikao cha Viongozi na Watendaji wa Idara ya
Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata na walimu hao, kumalizika jana mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment