Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka
Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt.Joseph Chilongani pamoja na wataalam wa Halmashauri
ya Meatu kutunga sheria ndogo zitakazosaidia kulinda na kutunza bwawa la maji
la Mwanjoro.
Mhe.
Makamu wa Rais amesema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya
Mwanjoro mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa bwawa la maji la Mwanjoro
lililopo kata ya Mwanjoro Wilayani humo.
Mhe.Makamu wa Rais
amesema Serikali inatambua uwepo wa
tatizo la maji na ukame uliopo Wilayani humo ndiyo maana imeamua kujenga bwawa
hilo litakalogharimu shilingi bilioni1.3 kwa awamu ya kwanza, hivyo ni lazima kuwepo na sheria ndogo zitasaidia
kufanya bwawa hilo lidumu na kutoa huduma endelevu kwa wananchi
“Hili bwawa halitaki
mifugo isogezwe huku wala shughuli za binadamu zije huku, nimemtaka Mkuu wa
Wilaya na wataalam waweke sheria ndogo za kulinda bwawa na eneo linalozunguka
bwawa, sheria zitakapo tungwa mzifuate, mkiliharibu mtakosa maji na mtarudi
kule kule mlikotoka” alisisitiza Makamu wa Rais.
Ameongeza kuwa pamoja
na Serikali kujenga Bwawa hilo kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo,
kutokana na hali ya ukame ya wilaya hiyo Serikali imejipanga kujenga bwawa
lingine litakalotumika kwa ajili ya shughuli za Kilimo cha Umwagiliaji.
Akitoa maelezo juu ya
mradi huo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Sera
ya Serikali ni kuwapunguzia wananchi adha ya kufuata maji umbali mrefu, hivyo
kupitia mradi wa Mwanjoro wananchi wa Vijiji vya Mwanjoro, Mbushi na Jinamo watasogezewa
huduma za maji karibu ili wasiende zaidi ya mita 400.
Aidha, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza kuwasilisha orodha ya mahitaji ya visima vya
maji katika wilaya hiyo, ili viwekwe
katika bajeti ya mwaka 2018/2019 , lengo likiwa ni kuongeza kiwango cha utoaji
wa huduma za maji kwa wananchi wilayani humo.
Akizungumza kwa niaba
ya wananchi wa Mbunge wa jimbo la Meatu Salum Khamis ameishukuru serikali kwa
jitihada zote zinazofanyika katika kuondoa tatizo la maji na akaahidi
kushirikiana na Wabunge pamoja na Wizara ya Maji kuhakikisha wananchi wa Meatu
wanapata maji safi na salama.
Naye Mbunge wa Jimbo la
Kisesa ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Luhaga Mpina akizungumza
kwa niaba ya wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata ya
Mwandoya ameomba Wizara ya Maji isaidie upatikanaji wa maji katika kata zote za
Jimbo la Kisesa.
Makamu wa Rais
anaendelea na ziara yake ya siku nne Mkoani Simiyu ambapo leo akiwa wilayani
Meatu ameweka Jiwe la msingi mradi wa Maji wa Bwawa la Mwanjoro, amesalimia wananchi
wa Kata ya mwanjoro, Mwanhuzi na kufanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Mwandoya.
MWISHO
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akikata
utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Mradi wa Maji wa Bwawa la
Mwanjolo wilayani Meatu wakati wa Ziara yake Mkoani Simiyuc(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi ujenzi wa Mradi wa Maji wa
Bwawa la Mwanjolo wilayani Meatu wakati wa Ziara yake Mkoani Simiyu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan , Viongozi
wa Kitaifa na Mkoa wa Simiyu wakishangilia mara baada ya kuwekwa kwa jiwe la
msingi la ujenzi wa Mradi wa Maji wa Bwawa la Mwanjolo wilayani Meatu wakati wa
Ziara yake Mkoani Simiyu, (wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka
.(Picha Na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhe.Isack Kamwelwe akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kuhusu Mradi wa Maji
wa Bwawa la Mwanjoro unaotekelezwa wilayani Meatu mkoa wa Simiyu. (Picha Na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasalimia
wananchi wa Mji wa Mwanhuzi wilayani Meatu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa wilayani Meatu,
Mhe.Luhaga Mpina, akizungumza na
wananchi wa Kata ya Mwandoya(hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Mwandoya, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe.Salum Khamis, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwanjoro (hawapo
pichani), mara baada ya Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kuweka jiwe la
msingi la msingi mradi wa Bwawa la maji la Mwanjoro wilayani humo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasalimia
wananchi wa Kata ya Mwanjoro wilayani
Meatu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment