Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan amekitaka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kuongeza
ubora na kupanua wigo wa udahili wa wanafunzi kwenye programu za sasa ili
kuendana na Sera Tanzania ya viwanda na kufikia Uchumi wa kati ifikapo 2025.
Ushauri huo ameutoa katika mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu
Huria cha TANZANIA yaliyofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi Mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais amesema kuwa ili kuweza kufikia
TANZANIA ya viwanda na kufikia uchumi wa kati 2025 lazima udahili wa wanafunzi
katika vyuo vikuu ufikie kiwango cha angalau asilimia 23.
“Naungana na Mhe.Rais kuwaomba muisaidie nchi yetu
kuongeza kiwango cha udahili wa wananchi wake kwa haraka na kwa kasi
itakayotuwezesha kufikia lengo la kuwa nchi ya Uchumi wa kati ifikapo 2025”
alisema
“Kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia kiwango kidogo cha
udahili katika elimu ya juu ni sifa ya msingi ya Uchumi wa chini na wa
kimaskini, Uchumi wa kati na wa Viwanda hauwezi kufikiwa na kuwa endelevu
pasipokuwa na kiwango cha udahili katika elimu ya juu cha angalau asilimia 23” alisema Makamu wa
Rais.
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.William
Ole Nasha amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania katika maendeleo ya sekta ya elimu nchini kwa kuwa kimekuwa
mtekelezaji mkuu wa malengo na mikakati ya Serikali kwa upande wa ujifunzaji kwa
njia za masafa.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa
Elifas Bisanda amesema tangu Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kianzishwe idadi ya
wahitimu imefikia 38, 993 baada ya mahafali ya 34 idadi hiyo imeongezeka
kufikia 39,934, jambo ambalo limechangia kukuza rasilimali watu hapa nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema kufanyika
kwa mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria
cha Tanzania mkoani humo kutakuwa chachu na kutaleta mwamko mpya wa elimu kwa
wananchi Mkoani humo.
“Tuliona tuwaalike wanafunzi ili kujenga hamasa kwao,
tulialika kamati zetu za shule, madiwani, walimu na wananchi wote wa Simiyu ili
washuhudie tukio hili tukiamini kuwa kwa kuona tukio hili kila mmoja atatamani
kuwa hivyo kesho, kama siyo yeye basi
awe mwanaye au ndugu yake” alisema
Mtaka.
Jumla ya wahitimu 941 kutoka Tanzania bara na Zanzibar na
nchi jirani walihudhurishwa mbele ya Mkuu wa Chuo Kikuu Huria
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na kutunukiwa Astashaha, stashahada, shahada, shahada za
uzamili , ambapo miongoni mwa hao 941 wahitimu saba walitunukiwa shahada ya uzamivu(PhD).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki matembezi ya mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania pamoja na Mkuu wa chuo hicho Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (kulia) kuelekea Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwenye sherehe za mahafali hayo zilizofanyika Mjini Bariadi Mkoa wa Simiyu.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria Tanzania Profesa Rwekaza Mukandala
wakati wa mahafali ya 34 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu. .(Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais)
Baadhi ya Wahitimu waliohitimu
katika Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. .(Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Baadhi ya Wahitimu waliohitimu
katika Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. .(Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na wananchi wa Mkoa wa Simiyu katika Mahafali
ya 34 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa
Bariadi Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
na wananchi wa Mkoa huo katika Mahafali ya 34 ya Chuo hicho yaliyofanyika
katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani humo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof.Elifas
Bisanda akizungumza na Wahitimu wa Chuo hicho na wananchi wa Mkoa wa Simiyu katika
Mahafali ya 34 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji
wa Bariadi Mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan(kulia), Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof.Elifas Bisanda(kushoto) Mkuu wa chuo hicho
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda (katikati) wakishangilia jambo katika
Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan( wa nne kulia), akiwa
katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania na Viongozi
wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya Mahafali ya 34 ya Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania, yaliyofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani
Simiyu(kulia) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
0 comments:
Post a Comment