Shirika
la Mendeleo la Uingereza (DFID) kupitia Mpango wa Kuboresha Elimu
Tanzania(EQUIP-T) limetoa jumla ya shilingi bilioni 1.7 kwa ajili ya ujenzi wa Miundombinu ya Elimu
katika Halmashauri zote za mkoa wa Simiyu.
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka wakati wa hafla fupi
ya makabidhiano na vyerehani 50 kutoka Ubalozi wa China, kusaini hati ya
makubaliano ya ujenzi wa Bweni la Wasichana Shule ya Sekondari Nkoma Itilima, Makabidhiano ya. Hundi ya Shilingi Milioni 178 kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo zilizotolewa na Balozi wa China, na
uwasilishwaji wa Taarifa za mashirika wadau wa Maendeleo mkoani Simiyu(DFID,
AMREF na UNFPA), ambayo ilishuhudiwa na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia
Suluhu Hassan.
Mtaka
amesema fedha hizo zimeshapokelewa katika Akaunti za Halmashauri zote za Mkoa
huo na wiki ya kuanzia tarehe 26/02/2018 Halmashauri hizo zinaanza kujenga
miundombinu ya Elimu.
Mtaka
ametoa shukrani zake kwa Shirika hilo ambalo amesema limechangia kwa kiasi
kikubwa mabadiliko katika Elimu na kuufanya mkoa wa Simiyu kutoka kwenye nafasi
za mwisho kwenye ufaulu mpaka kufikia nafasi ya 11 kwa mwaka 2017.
“
Tunawashukuru sana DFID kwa namna wanavyotusaidia katika Sekta ya Elimu kwenye
mkoa wetu, DFID kupitia EQUIP wametoa
IPAD(Vishikwambi) kwa kila Mkuu wa Shule ndani ya mkoa Simiyu, Kila Mratibu wa
Elimu wa Elimu Kata amepewa pikipiki na
anapewa posho ya shilingi 206,000/= kila
mwezi kwa ajili ya kununua mafuta ya kuwawezesha kutembelea
shule zao, sisi kama mkoa
tunawashukuru sana” alisema Mtaka.
Akitoa
taarifa ya utendaji kazi wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) Bi.
Elizabeth Arthy amesema Shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi za
Serikali na kuhakikisha wanashiriki
katika kuinua ubora wa elimu kwa watoto wa Mkoa wa Simiyu.
Naye
Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke aliyekabidhi vyerehani 50 kwa ajili ya
Kikundi cha Wanawake Mjini Bariadi
amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka kwa jinsi
anavyojishughulisha katika kuwaletea wananchi wa Mkoa wa Simiyu maendeleo na akaahidi
kuendelea kushirikiana na mkoa huo katika nyanja mbalimbali.
Kwa
upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika lilaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA),
Bi. Jacqueline Mahon amewapongeza viongozi wa mkoa wa Simiyu wakiongozwa na
Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na akaahidi kuendelea kuunga mkono juhudi
za maendeleo mkoani humo kupitia huduma za afya ya uzazi kwa wananwake na
vijana.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mhe.Andrew Chenge,
aliyashukuru mashirika hayo na Balozi wa China ambao ni wadau wakubwa wa
maendeleo mkoani humo katika Sekta ya elimu, afya na viwanda na kubainisha kuwa
mkoa huo una kiu ya maendeleo ni hivyo umejipanga kwenda kwa kukimbia wakati
wengine wanatembea.
MWISHO
|
Kutoka kushoto (wanaoandika) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakisaini hati ya
makubaliano ya Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Nkoma
wilayani Itilima, fedha ambazo zimetolewa na Balozi wa China hapa nchini,
Mhe.Wang Ke., zoezi ambalo lilishuhudiwa pia na Makamu wa Rais wa Tanzania,
Mhe.Samia Suluhu Hassan Jana Mjini Bariadi..
Mwakilishi wa Shirika laUingereza la ( DFID) Bi. Elizabeth Arthy akiwasilisha
taarifa ya namna Shirika hilo linavyofanya kazi na mkoa wa Simiyu mbele ya
viongozi wa Kitaifa na Mkoa wa Simiyu, katika hafla iliyofanyika jana Viwanja
vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Itilima(mwenye miwani) na Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Wang Ke wakisaini
hati ya makubaliano ya ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari
Nkoma wilayani Itilima, fedha ambazo zimetolewa na Balozi huyo , zoezi ambalo
lilishuhudiwa pia na Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan, Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka na viongozi wengine wa Kitaifa na Mkoa
mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akimshukuru Balozi wa China hapa Nchini, Mhe.Wang Ke mara
baada ya kusaini hati ya makubaliano ya ujenzi
wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Nkoma wilayani Itilima, fedha
ambazo zimetolewa na Balozi huyo , zoezi ambalo lilishuhudiwa pia na Makamu wa
Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan(katikati) na viongozi wengine wa
Kitaifa mjini Bariadi.
Balozi wa China hapa Nchini,
Mhe.Wang Ke akimkabidhi Makamu wa Rais
wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan Hundi ya Shilingi milioni 178 kwa ajili ya
ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Nkoma wilayani Itilima,
fedha ambazo zimetolewa na Balozi huyo kwa Serikali mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akionesha Hundi ya Shilingi
milioni 178 iliyotolewa na Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Wang Ke kwa ajili
ya ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Nkoma wilayani
Itilima zoezi lililofanyika jana Mjini Bariadi.
Balozi wa China hapa nchini, Mhe.Wang Ke akitoa
maelezo kwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan(wa pili
kulia) kabla ya kumkabidhi vyerehani 50 kwa ajili ya kikundi cha wanawake wa Mjini
Bariadi zoezi lililofanyika jana Mjini Bariadi.
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan
na viongozi wa Mkoa wa Simiyu pamoja na Halmashauri ya Mji wa Bariadi wakipokea cherehani
kama ishara ya makabidhiano ya vyerehani 50 kutoka kwa Balozi wa China hapa
nchini, Mhe.Wang Ke, zoezi lililofanyika jana mjini Bariadi.
Mwakilishi Mkaazi wa Shilika la umoja wa Mataifa
linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UFPA) Bi. Jacqueline Mahon akiwasilisha taarifa ya namna Shirika hilo
linavyofanya kazi na Mkoa wa Simiyu katika kikao kilichofanyika jana Mjini
Bariadi.
Kiongozi wa AMREF Tanzania, Bi. Florence Temu akiwasilisha taarifa ya namna
Shirika hilo linavyofanya kazi na Mkoa wa Simiyu kwa Viongozi wa Kitaifa na
Mkoa katika Hafla iliyofanyika jana
Mjini Bariadi.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi, akitoa shukrani kwa
wadau wote wanaounga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea maendeleo wakati
wa uwasilishwaji wa taarifa za wadau hao kwa viongozi wa Kitafa na Mkoa katika
hafla iliyofanyika jana Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akiteta jambo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 178 za ujenzi wa Bweni Itilima, Vyerehani
50 viliyotolewa na Balozi wa China hapa nchini Mhe.Wang Ke kwa kikundi cha wanawake Bariadi Mjini na
uwasilishwaji wa taarifa za mashirika wadau wa maendeleo mkoa wa Simiyu jana
jioni.
|
0 comments:
Post a Comment