Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan
amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kuunga mkono jitihada za Serikali hususani katika utekelezaji wa Sera ya Tanzania
ya Viwanda.
Mhe.Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Wananchi wa Mji
wa Bariadi kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa CCM Mkoa wa Simiyu.
Amesema amepokea taarifa kuwa Mkoa wa Simiyu una jumla ya viwanda 14 vya
kuchakata pamba na viwanda vidogo vya kuongeza thamani ya mazao 1035, jambo ambalo ni maendeleo makubwa kwa wananchi
na akatoa wito kwa wananchi wa Simiyu kuendelea kuwekeza katika maeneo
mbalimbali na kuwataka kuwapokea wawekezaji kutoka maeneo mengine ndani na nje
ya nchi.
Aidha, amepongeza utekelezaji wa mkakati wa “Wilaya Moja Bidhaa Moja” ambao
amesema ni mkakati mzuri unaoupambambanua Mkoa wa Simiyu katika Sekta ya Viwanda.
“Nimeelezwa hapa na Mkuu wa Mkoa kuwa mmeanza kwa kila wilaya moja kuwa na
bidhaa moja(kiwanda kimoja) lakini haikatazwi wilaya hiyo kuwa na viwanda
vidogo, nimeelezwa kuwa Meatu mmeamua kusindika maziwa na Maswa kiwanda cha
chaki, Bariadi kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba na hiki ni
kiwanda changu ninacho kisimamia” alisema
“Nataka kuahidi kuwa kiwanda hiki kitajengwa na kitazalisha bidhaa za sekta
ya Afya, Busega pia kitajengwa kiwanda cha maji tunayotundikiwa hospitali(IV
Infussion/drip), Itilima nimeambiwa ni masuala ya asali na alizeti, lakini pia
nimeambiwa kuna viwanda vya bidhaa za ngozi maeneo tofauti nawapongeza sana kwa
mwamko mkubwa huu” alisisitiza Makamu wa Rais.
Wakati huo huo Mhe.Makamu wa Rais amewapongeza viongozi wa Mkoa na
Halmashauri ya Mji Bariadi kwa kusimamia na kuhakikisha barabara za Mjini
Bariadi zinajengwa kwa kiwango kinachoridhisha, hivyo amesisitiza usafi uimarishwe katika barabara hizo hususani
barabara iliyopewa jina lake ili
kupendezesha Mji.
Katika hatua nyingine Mhe.Makamu wa Rais amewahakikishia wananchi wa Mkoa
wa Simiyu upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2019/2020, kupitia
Mradi mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria ambao unatekelezwa na Wizara iliyo
chini ya Ofisi yake kwa kushrikiana na Wizara ya Maji.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema tarehe
21/02/2017Mhe. Makamu wa Rais atakutana na timu ya wataalam wanaofanya upembuzi
yakinifu wa ujenzi wa Kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba mkoani
humo, ambapo alibainisha kuwa mkoa umejipambanua
kwenye sekta ya viwanda hasa katika kutekeleza maono na mtazamo wa Viongozi wakuu
wa Kitaifa.
Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge akawasilisha changamoto za wananchi kwa Makamu
wa Rais amesema wananchi Bariadi wanakabiliwa
na uvamizi wa tembo katika mashamba yao , hivyo ni vema ikawekwa mipaka na zikatafutwa njia
ya kuwazuia, jambo ambalo Mhe. Makamu alilitolea ufafanuzi kuwa Serikali
italifanyia kazi kuhakikisha wanyama hao hawawadhuru watu na kuharibu mazao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Samia Suluhu Hassan
akiwa katika ziara yake wilayani Bariadi ameweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa
Nyumba za Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, amekagua ujenzi wa barabara za Bariadi
Mjini na kufungua barabara moja iliyopewa jina lake”BARABARA YA SAMIA SULUHU”.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mhe.Samia Suluhu Hassan akifungua moja ya barabara za Mji wa Bariadi iliyopewa jina lake “SAMIA SULUHU AVENUE” wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa
kumbukumbu katika barabara iliyopewa jina lake “BARABARA YA SAMIA SULUHU” Mjini
Bariadi, wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan (katikati)
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka(mwenye suti kulia) wakifurahia
jambo na baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia akifungua barabara iliyopewa
jina lake “BARABARA YA SAMIA SULUHU” Mjini Bariadi wakati wa ziara yake katika
Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.
Mbunge
wa Jimbo la Bariadi, Mhe.Andrew Chenge
akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Bariadi katika Mkutano wa Hadhara
uliofanyika Uwanja wa CCM Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan mkoani humo.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na
wananchi wa Bariadi (hawapo pichani) katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Mkoa wa
Simiyu, wakati wa ziara yake mkoani humo.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwaaga wananchi wa
Bariadi Mjini mara baada ya kumaliza Mkutano wa Hadhara uliofanyika Uwanja wa
CCM Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara yake mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akipanda mti wa kumbukumbu katika ya “BARABARA YA SAMIA SULUHU” Mjini Bariadi,
ambayo imefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe.Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Bariadi Mkoani
Simiyu.
Wabunge wa Viti Maalum
kupitia CCM Mhe. Esther Midimu(wa sita
kulia) na Leah Komanya (anayefuata) wakicheza pamoja na Kwaya ya Walimu Bariadi katika Mkutano wa
Hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara ya Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan mkoani humo.
Kwaya ya AICT Bariadi ikitoa
burudani ya wimbo kwa wananchi na viongozi kabla ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan kuzungumza na wananchi katika
Mkutano wa Hadhara uliofanyika Uwanja wa CCM Mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara
yake mkoani humo
0 comments:
Post a Comment