Kampuni ya Simon Group imechangia kiasi cha Shilingi
Milioni 25 kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu katika mkoa wa Simiyu.
Akikabidhi
hundi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Simon Group, Ndg. Leonard Kitwala amesema
Kampuni hiyo imetoa fedha hizo ili
kuunga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya Sekta ya Elimu na kwa kuwa
Simiyu ni mahali alipozaliwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Simon Kisena
ameona ni vema asaidie maendeleo ya
elimu nyumbani kwao.
Aidha, Kitwala amesema kama kampuni wameamua kuunga mkono
ujenzi wa miundombinu ya Elimu Simiyu kwa kuwa wamependezwa na juhudi za
Viongozi wa Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika
kuwaletea maendeleo wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu.
Akipokea hundi ya shilingi milioni 25 kwa niaba ya Viongozi
na wanafunzi wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa
Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka amesema anaishukuru Kampuni ya Saimon Group ambayo
inaendesha mradi wa Usafrishaji wa Mabasi Dar es Salaam(UDA) kwa kuamua
kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu mkoani humo.
“Nawashukuru sana SAIMON GROUP kwa kuamua kusaidia ujenzi
wa miundombinu ya elimu Simiyu, shilingi milioni 25 ni fedha nyingi sana kwenye
kufanikisha ujenzi wa mundombinu ya elimu hasa kwa mkoa kama wa kwetu ambao shughuli
nyingi za ujenzi tunatumia “Force Account” , tunatumia nguvu za wananchi na Serikali
ina nafasi yake katika ujenzi wa miradi
hiyo” alisema
“ Zaidi sana namshukuru Mkurugenzi wa SIMON GROUP ndugu
Robert Kisena ambaye ni mzaliwa wa Mkoa huu kwa kuona arudishe sehemu ya
faida ya biashara zake nyumbani, kwa niaba ya viongozi wenzangu ninamkikishia
kwamba mchango huu utaenda kwenye matokeo yanayoonekana, hata wakati wa
uzinduzi wa madarasa yatakayojengwa tutaipa nafasi Kampuni ya SIMON GROUP kuja kuona alama
waliyoweka katika mkoa wetu” alisisitiza Mtaka.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi,
Mhe.Robert Lweyo amesema mchango huo wa SIMON GROUP umekuja katika muda muafaka
ambao mkoa huo una uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa hivyo alimshukuru
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg. Robert Kisena na kuahidi pia kuwa fedha hizo
zitafanya kazi iliyokusudiwa..
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto)
akipokea hundi ya shilingi milioni 25 iliyotolewa na Kampuni ya SIMON GROUP kwa
ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu kutoka kwa Ndg.Leonald Kitwala ambaye
aliyekabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampun hiyo Ndg.Robert Kisena.
Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, Mhe.Robert Lweyo akitoa shukrani kwa Kampuni ya SIMON GROUP
kupitia kwa Ndg.Leonald Kitwala
aliyekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 25 kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (hayupo picha) kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg.Robert
Kisena, kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu ya Elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto)
akipokea hundi ya shilingi milioni 25 iliyotolewa na Kampuni ya SIMON GROUP kwa
ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu kutoka kwa Ndg.Leonald Kitwala ambaye
aliyekabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampun hiyo Ndg.Robert Kisena
0 comments:
Post a Comment