Kaya 6120 sawa na asilimia 52
ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu
zimewezeshwa kulima pamba ekari 8712 katika Msimu wa mwaka 2017/2018 kwa
kutumia fedha za uhawilishaji.
Hayo yalibainishwa na
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Simiyu Bw. Nyasilu Ndulu wakati
wa kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi juu ya
mpango huo kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Nyasilu amesema pamoja na kulima pamba walengwa wa
mpango huo katika Wilaya ya Bariadi na wilaya nyingine Mkoani Simiyu kupitia
fedha za uhawilishaji (wanazopewa) wamefanikiwa kujenga nyumba, kufuga,
kuanzisha biashara ndogo ndogo na kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF).
Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa zoezi la
uhawilishaji chini ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini awamu ya tatu mwaka 2015
hadi sasa, tayari awamu 17 za
malipo zimekwisha fanyika kwa walengwa 37, 533 na jumla ya shilingi bilioni
28.9 zimelipwa kwa wahusika.
Amesema fedha hizo
zimejumuisha ruzuku za aina mbili ikiwa ni ruzuku ya msingi na ile itokanayo na
utimizaji wa mashati ya Afya na Elimu ambapo watoto 39,068 sawa na asilimia
90.3 wameweza kupata mahitaji muhimu ya shule na kukuhudhuria shuleni na watoto
51, 280 sawa na asilimia 93.1 wamepata mahitaji ya kliniki na kupelekwa kliniki.
“Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini umeweza
kuwasaidia walengwa kujikwamua kutoka kwenye umaskini, wapo walioanzisha
biashara, wanaolima, wanaofuga, waliojenga nyumba bora; kwa kutumia fedha hizi wanazopewa
wapo ambao watoto walikuwa hawahudhurii shuleni na kliniki lakini sasa hivi mahudhurio
mazuri” Alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka awali akifungua kikao amesema pamoja na mafanikio waliyoyapata walengwa, wanufaika
wote waliofanya mambo ya maendeleo ni vema wakawa mfano kwa wenzao
huku akiwataka wale walioshindwa kuondolewa kwenye mpango huo.
Aidha, Mtaka aliwataka walengwa
wote wa mpango kuendana na malengo ya nchi ya kuelekea kwenye Uchumi wa Kati
ifikapo mwaka 2025 badala ya kuwaza kuendelea kubaki katika mpango huo.
“Mtazamo wangu mimi ni vizuri wanufaika wa
TASAF waendane na Mpango wa Nchi, tunaposema tunataka kwenda kwenye Uchumi wa
Kati kufikia mwaka 2025 wanufaika wa TASAF wanapaswa kujindaa kwenda kwenye
uchumi wa kati, ili badala ya watu kutaka tu kuingia kwenye mpango, tupate watu wanaotaka kutoka baada ya kupiga
hatua na kutoka kwenye umaskini waliokuwa nao mwanzo” alifafanua Mtaka
Nae Bw. Fariji Mishael mtaalamu wa
ufuatiliaji wa tathmini kutoka Ofisi ya TASAF Makao makuu aliupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza
mpango huo vizuri na kuomba wataalamu kuwasaidia walengwa walio kwenye maeneo
yao katika kuwashauri namna bora ya kuendesha
miradi waliyoianzisha ili iwe endelevu na iweze kuwasaidia kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na viongozi wa mkoa
huo wakati alipofungua kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa
huo juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT
mjini Bariadi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na viongozi
wa mkoa huo katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo
juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT
mjini Bariadi.
Bw. Fariji Mishael mtaalamu wa ufuatiliaji wa tathmini kutoka Ofisi ya
TASAF Makao makuu akizungumza na
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, katika kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa
viongozi hao juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika
ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo,
Mhe.Anthony Mtaka katika cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo
juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT
mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Benson Kilangi akichangia jambo katika kikao
cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu juu ya Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Katibu wa CCM Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donald Magesa akichangia jambo, katika
kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa mkoa huo juu ya Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani akichangia jambo katika
kikao cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa mkoa wa Simiyu juu ya Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo,
Mhe.Anthony Mtaka katika cha kujenga uelewa wa pamoja kwa viongozi wa Mkoa huo
juu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kilichofanyika katika ukumbi wa KKKT
mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment