Wadau mbalimbali
wa maendeleo wa Mkoa wa Simiyu wametoa shilingi Milioni 10 na Kilo 1200 za
mchele, mafuta ya kula, sabuni , sukari na mahitaji mengine kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi wa kidato cha Sita walioweka Kambi ya kitaaluma
wilayani Maswa kwa ajili ya kujiandaa na Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi
Mei.
Akizungumza wakati
wa makabidhiano katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa, Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amewataja wadau hao kuwa ni Ofisi yake iliyotoa
shilingi milioni 10 kwa ajili ya kuongezea posho ya walimu mahiri 40
wanaowafundisha wanafunzi hao pamoja na kununua mahitaji maalumu kwa ajili ya
wanafunzi wa kike.
Amesema
wadau wengine ni Mbunge wa Itilima Mhe.Njalu Silanga aliyetoa kilo 500 za
mchele, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kilo 300, Mkurugenzi wa
Itilima kilo 100 za mchele, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi kilo
100 za mchele, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bariadi kilo 100 za mchele na
Mkurugenzi Busega kilo 100 za mchele.
Aidha,
amesema Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imeahidi kuchangia ng’ombe wawili na
Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu imeahidi kuchangia kilo 100 za
mchele.
Mtaka
amewashukuru wadau wote walioguswa kuwachangia wanafunzi hao wa kidato cha sita
na akatoa wito kwa wazazi, viongozi na
watu kutoka makundi mbalimbali kujitokeza kuunga mkono juhudi zinazofanywa na
Idara ya Elimu katika kuwasaidia wanafunzi hao, ili waweze kujiandaa na kufanya
vizuri katika Mtihani wa Taifa mwezi Mei.
“Lengo
letu ni kuhakikisha kuwa mwaka huu mkoa wetu unaingia kwenye mikoa itakayofanya
vizuri zaidi Kitaifa, niendelee kuwaomba wanafunzi mliopo hapa mzingatie masomo
siku 10 mtakazokaa hapa ziwe na manufaa kwenu na ninyi walimu 40 wafundisheni
watoto kwa vipaji vyote mlivyojaliwa na Mwenyezi Mungu ili wafanye vizuri
kwenye mtihani wao wa mwisho” alisema Mtaka.
Wakati
huo huo Mkuu huyo wa Mkoa amesema baada ya kambi hiyo ya kitaaluma kumalizika
ndani ya hizo siku10 ufanyike mtihani ili kuwapima wanafunzi na akaahidi kutoa
zawadi ya shilingi milioni tano kwa walimu wataotunga maswali yatakayofanana na
yale yatakayokuwepo katika Mtihani wa Taifa kwenye masomo yao.
Akizungumza
kwa niaba ya walimu mahiri 40 wanaowafundisha wanafunzi kambini hapo Mwalimu
Makame S. Makame kutoka Shule ya Sekondari Bariadi, amesema kwa namna walivyojitolea kuwafundisha
wanafunzi hao wana imani kubwa kuwa mwaka 2018 utakuwa mwaka matokeo
mazuri(Kidato cha Sita) ya kihistoria
kwa Mkoa wa Simiyu.
Mwanafunzi
Martina Simba kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa amemshukuru Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu na wadau wengine wote kwa misaada waliyoitoa na kusisitiza kuwa,
kukaa kwao kambini hapo siku kumi hakutakuwa bure bali ni mwanzo mzuri wa
safari yao ya mafanikio ya kuwafikisha katika mikoa itakayofanya vizuri zaidi
katika Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2018.
Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha
Sita Mkoani Simiyu ilifunguliwa rasmi Aprili 3 ikiwa na jumla ya wanafunzi1003
kutoka shule 11 na walimu mahiri 40 kwa ajili ya kuwafundisha na inatarajiwa
kufungwa Aprili 13, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza na wanafunzi wa Kidato
cha Sita kutoka katika Shule 11 mkoani humo walioweka kambi ya kitaaluma kwa
ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa utakaofanyika Mwezi Mei, mara baada ya
kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na wadau kwa ajili ya wanafunzi
hao.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony akikata utepe kabla ya kakabidhi msaada wa vitu mbalimbali viliyotolewa
na wadau kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka katika Shule 11 mkoani humo,
walioweka kambi ya kitaaluma kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa
utakaofanyika Mwezi Mei 2018.
Afisa
Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka katika Shule 11
mkoani humo walioweka kambi ya kitaaluma kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa
Taifa utakaofanyika Mwezi Mei mwaka huu.
Baadhi
ya Walimu Mahiri wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo
pichani) wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka
katika Shule 11 mkoani humo walioweka kambi ya kitaaluma kwa ajili ya
maandalizi ya Mtihani wa Taifa utakaofanyika Mwezi Mei mwaka huu.
Mwanafunzi
Martina Simba kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa akitoa shukrani kwa
Viongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa msaada wa chakula na mahitaji mengine uliotolewa
kwa wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka katika Shule 11 mkoani humo walioweka
kambi ya kitaaluma,kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa utakaofanyika
Mwezi Mei mwaka huu.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu walioweka
kambi ya kitaaluma kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa utakaofanyika
Mwezi Mei mwaka huu, wakimsikiliza Mkuu
wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao
leo katika Ukumbi wa Shule ya Wasichana Maswa wilayani Maswa.
Majaliwa
Chibona mmoja wa walimu 40 mahiri wanaowafundisha wanafunzi wa kidato cha sita kutokashule
11 mkoani Simiyu, ambao wameweka kambi ya Kitaaluma kwa ajili ya maandalizi ya
Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Mei 2018, akitoa shukrani kwa viongozi
waliotoa misaada mbalimbali kwa wanafunzi na walimu ili kuwezesha kambi hiyo
kufanikiwa.
Baadhi
ya wanafunzi wasichana wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 mkoani Simiyu wakifurahia
jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Maswa,
Mhe.Dkt.Seif Shekalaghe(mwenye miwani) mara baada ya kukabidhiwa msaada wa
chakula na mahitaji mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment