Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo ameishauri
Serikali kutoa kipaumbele kwa wilaya mpya za Busega na Itilima mkoani humo, katika Ujenzi wa Ofisi na Nyumba za Watumishi
ili watumishi waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri.
Mhe. Yakobo ameyasema hayo Aprili 10, alipotembelea na
kuona Ujenzi wa Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Busega ambalo mpaka
kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 4.6 , wakati wa Ziara ya Kamati
ya Siasa ya CCM Mkoa ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
“Ingekuwa
vizuri Ofisi na nyumba za watumishi zipatikane maana Busega imeshajitegemea,
kama mkoa tuwe na kaulimbiu hiyo kuwa wilaya hizi mpya ziangaliwe; eneo hili ni
changa linapaswa kuendelezwa ili watumishi wa hapa nao wafurahie utumishi
wao”alisema Mhe.Yakobo
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana
na Wakurugenzi wa Halmashauri waliwasilisha suala hilo kwa Kamati ya Bunge na
kuomba mkoa wa Simiyu kwa kuwa ni mpya uangaliwe sana kwenye mahitaji muhimu
hususani yanayowagusa watumishi ikiwemo makazi.
“Ningependa
kuwaomba Mwenyekiti wa CCM mkoa na Mjumbe wa NEC mlibebe jambo hili kama agenda
ya Mkoa, sisi kama Serikali tulienda pamoja na Wakurugenzi kwenye Kamati ya
Bunge, tukaomba kama Mkoa mpya waangalie mahitaji ya msingi hasa kwa watumishi,
majengo yote haya tumeyaombea fedha na majengo ya Mkoa pia tumeyaombea fedha”
alisema Mtaka.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema Serikali imeshajenga nyumba
nne (04) kwa ajili ya watumishi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Busega na mpango wa
kuendelea kupata fedha kwa ajili ya kujenga nyumba zilizobaki unaendelea.
Aidha,
Sagini amesema Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha jengo la Halmashauri
ya Wilaya ya Busega, Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega pamoja makazi
yake.
Katika
hatua nyingine Sagini amewataarifu wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa
Simiyu kuwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo na kukamilisha ujenzi wa Nyumba za Viongozi wa
Mkoa zimetengwa.
Kamati
ya Siasa ya CCM Mkoa ikiongozwa na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe.Enock Yakobo pamoja na kukagua jengo la Halmashauri
wilayani Busega ilikagua Miradi mingine ya maendeleo katika Sekta ya Maji, Elimu
na Afya.
MWISHO
Baadhi ya Viongozi wa
Serikali mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega wakiwa na Wajumbe wa Kamati ya
Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu, ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mhe.Enock
Yakobo wakati walipotembelea mradi wa maji wa Lamadi katika ziara yao ya
kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Ndg.Anderson Njiginya (katikati kushoto)
akitoa maelezo kuhusu Jengo la Halmashauri hiyo kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa
ya CCM Mkoa wa Simiyu, ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mhe.Enock Yakobo
wakati walipotembelea mradi huo katika ziara yao ya kukagua utekelezaji wa
Ilani ya CCM wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa,
Mhe.Enock Yakobo(kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Busega, Ndg.Anderson Njiginya (kulia) akitoa maelezo juu ya ujenzi wa vyumba viwili
vya maabara, katika Shule inayojengwa
Kijiji cha Lukungu ambayo wananchi wanakusudia
kuipa jina na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka itakapokamilika, katika ziara Kamati ya Siasa ya CCM Mkoawilayani
Busega.
Baadhi ya Viongozi wa
Serikali mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Busega wakiwa na Wajumbe wa Kamati ya
Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu, ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Mhe.Enock
Yakobo wakiingia katika moja ya Bweni lililojengwa Shule ya Sekondari Mkula kwa
fedha za Mradi wa Lipa kulingana na Matokeo(P4R) katika ziara yao ya kukagua utekelezaji wa
Ilani ya CCM wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment