Wanafunzi
7,361 wa kidato cha nne kutoka katika shule za sekondari Mkoani SIMIYU
wanatarajia kuweka kambi maalum ya kitaaluma ili kujiandaa na Mtihani wa Taifa
na kuweza kuinua kiwango cha ufaulu mkoani humo.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipokuwa
akifunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi 1005 wa Kidato cha Sita kutoka shule
11 Mkoani humo, waliokuwa chini ya Wakuu wa Shule 11 na walimu mahiri 40,
wilayani Maswa.
Lengo la kambi hii lilikuwa ni kutekeleza sehemu ya mkakati
wa Mkoa huo wa kufuta daraja la nne na sifuri kwa kuwaandaa wanafunzi wa Kidato
cha Sita Mkoani humo na Mtihani wa Taifa unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa
mwezi Mei.
Mtaka anasema baada ya kumalizika kambi hiyo ni
matumaini ya Mkoa wa Simiyu kuona wanafunzi wanafaulu kwa kiwango cha daraja la
kwanza na kufuta sifuri huku akitangaza kuanza kwa kambi ya wanafunzi wa
kidato cha nne.
“Tumemaliza kambi ya Kidato cha Sita, natangaza rasmi
leo kuwa tutakuwa na Kambi ya Kidato cha
Nne na Darasa la Saba mwezi Juni Mwaka huu, wanafunzi 7361 wa kidato cha nne
watakaa kwenye kambi siku 21, kila wilaya itakaa na wanafunzi wake na mimi kama
Mkuu wa Mkoa nitayafungua makambi hayo” alisema
“Baada ya kambi hiyo tutachukua wanafunzi bora watano katika
kila shule baada ya mtihani wa Mkoa kufanyika ambao watatengeneza kambi kiwilaya
pia, ili tuchakate na kupata wanafunzi
bora watakaotengeneza daraja la kwanza kwenye mkoa” alisisitiza
Aidha, Mtaka amesema anashauriana na Maafisa Elimu
kuona uwezekano wa kutengeneza kambi kwa
ajili ya wanafunzi 10 ambao wanafanya vibaya kwa kila shule ili waweze
kusaidiwa na baaaye Mkoa uweze
kuondokana kabisa na sifuri.
Ameongeza kuwa pia mwezi Juni wanafunzi 36,156 wa darasa
la saba wataweka kambi na kambi zote mbili zitafunguliwa kwa pamoja, hivyo
akatoa taarifa kuwa wadau wote wa elimu na watu wenye mapenzi mema
watakapoombwa kuchangia ili kuwezesha kambi hizo wakubali kuunga mkono suala
hilo.
Afisa Elimu wa Mkoa wa SIMIYU, Julius Nestory ameahidi
kuwa kufikia mwaka 2020 kutakuwa na Mapinduzi makubwa ya Sekta ya Elimu katika
Mkoa huo.
Wanafunzi wa kidato cha sita waliomaliza kambi iliyochukua
takribani siku kumi wamesema kukutanishwa pamoja kumewasaidia hasa kwenye mada
na maswali yalikuwa yanawasumbua, hivyo kwa sasa wamejiandaa vizuri na
watafanya vizuri katika Mtihani wao wa mwisho.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU amesema
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itatoa Shilingi Milioni Mbili kwa mwanafunzi atakayeingia
katika kumi bora Kitaifa, Shilingi Milioni Tano kwa shule itakayokuwa miongoni
mwa shule kumi bora na mwalimu mahiri atakayewezesha Alama A atapata Shilingi Laki mbili.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 Mkoani
humo wakati wa kufunga Kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi hao 1005 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya
Maswa.
Afisa Elimu wa Mkoa wa
Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka
shule 11 Mkoan humo wakati wa kufunga Kambi
ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao 1005 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya
Maswa.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha
Sita kutoka shule 11 Mkoani humo wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao 1005 katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoa Shule 11 Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu
wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika zoezi la kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi
hao 1005 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na baaadhi ya viongozi wa Chama na Serikali, Maafisa Elimu na wanafunzi
baada ya kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha
Sita 1005 Mkoani humo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na baaadhi ya viongozi wa Chama na Serikali, Wakuu wa Shule na wanafunzi
baada ya kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha
Sita 1005 Mkoani humo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na baaadhi ya viongozi wa Chama na Serikali, Walimu mahiri na wanafunzi
baada ya kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa Kidato cha
Sita 1005 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa
0 comments:
Post a Comment