Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa
wito kwa walimu wote wa kike mkoani humo kuwasaidia wanafunzi wa kike katika
elimu ya kujitambua ili iwasaidie kuepukana na vishawishi vinavyoweza kupekelekea
mimba za utotoni.
Mtaka
ameyasema hayo jana katika Kongamano la Elimu ya Masuala ya Jinsia kwa Walimu
na Wanafunzi wa Kike wa baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Makao Makuu, kilichofanyika
katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi.
Amesema si masuala yote ya
yanayohusu maisha yamewekwa katika mitaala, hivyo walimu wanapaswa kusimama
katika nafasi zao kama wazazi ili kile wanachotamani kuwafundisha watoto wao au
ndugu zao kwa lengo la kuwalinda na tabia zisizofaa, wakifanye pia kwa
wanafunzi wao wa kike ili wawasaidie wasiharibike.
Ameongeza kuwa Viongozi na Watendaji mbalimbali wa Serikali Mkoani
humo wanatamani wanafunzi wote wa kike wanaoanza darasa la kwanza na kidato cha
kwanza wamalize masomo na kufikia ndoto zao pasipo vikwazo vyovyote ikiwemo
mimba za utotoni.
“Tungehitaji kuona wanafunzi wa
kike wa mkoa wetu wanajitambua, tusingehitaji kuwa na wanafunzi wa kike
wanaopata mimba wakakatisha masomo yao na ndoto zao, natamani watoto wa kike wa
Simiyu suala la elimu liwe Kipaumbele chao cha kwanza” alisema Mtaka
“Msaada wa kwanza wa watoto wetu
wa kike ni walimu wetu wa kike, mwalimu anayewasimamia vizuri watoto wa
kike na kuwasaidia wasiharibike hata
watoto wake nyumbani hawawezi kuharibika, ‘uki-ignore’ (ukipuuza) kwamba
mwanafunzi hakuhusu kesho utakuta mwanao ndiye anayeharibikiwa” alisisitiza.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa
amesema ipo haja na hoja kujenga mabweni ya wanafunzi wa kike kwa shule zote za
Sekondari za Kata ili watoto wa kike wasipange wala kutembea mwendo mrefu.
Kwa upande wake Hakimu Mfawidhi
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Mary Mrio amesema walimu wa kike wakiwasaidia na kuwa
marafiki kwa watoto wa kike ni rahisi watoto kuwaeleza matatizo yanayowakabili
na akawataka wanafunzi kuwa wawazi kwa walimu wao wa kike ili wasaidiwe.
Naye Mtaalamu wa Masuala ya
Jinsia kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la AMREF kupitia Mradi wa UZAZI
UZIMA ametoa wito kwa watoto wa kike mkoani Simiyu kutokubali kutumiwa kama
mitaji na wazazi wao kwa kukatishwa masomo na kuozeshwa mapema, ili kukabiliana na changamoto ya mimba za utotoni katika kufikia ndoto zao.
Katika hatua nyingine wanafunzi
wa kike wameiomba Serikali kuona namna ya kuwashirikisha wazazi na walezi wao katika
makongamano ambayo yanatumika kutoa elimu ya masuala ya jinsia ili nao wawe na
uelewa juu ya masuala hayo na kujua namna ya kuwasaidia watoto wao.
“Kwenye makongamano kama haya
ingekuwa vizuri tukiwahusisha baadhi ya wazazi ili nao wapate elimu kama hii
tunayopata sisi, maana sisi watoto wa kike kuna wakati unaweza ukawa unaumwa
ila ukimweleza mzazi anasema hutaki kufanya kazi” Florencia Ndakama
mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Shule ya Sekondari Bariadi
Akitoa
taarifa juu ya ushiriki wa wanafunzi na walimu wa kike katika kongamano hilo,
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory amesema jumla ya walimu 228
na wanafunzi 1506 kutoka katika baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mjini
Bariadi wameshiriki.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na walimu na wanafunzi wa kike kutoka katika
baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Mjini Bariadi katika Kongamano la Elimu
ya Masuala ya Jinsia lililofanyika jana katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini Bariadi.
Mwanafunzi
kutoka Shule ya Sekondari kidinda akichangia jambo katika Kongamano la Elimu ya
Masuala ya Kijinsia kwa walimu na wanafunzi wa kike kutoka katika baadhi ya
Shule za Msingi na Sekondari za Mjini Bariadi, lililofanyika jana katika Shule
ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini
Bariadi, (kulia) Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kutoka shirika lisilo la Kiserikali la AMREF.
Mwanafunzi
kutoka Shule ya Sekondari kidinda akichangia jambo katika Kongamano la Elimu ya
Masuala ya Jinsia kwa walimu na wanafunzi wa kike kutoka katika baadhi ya
Shule za Msingi na Sekondari za Mjini Bariadi, lililofanyika jana katika Shule
ya Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini
Bariadi.
Mwandishi
wa Habari wa Gazeti la Nipashe, Bibi.Happy Severine akitoa mada katika Kongamano
la Elimu ya Masuala ya Jinsia kwa walimu na wanafunzi wa kike kutoka katika
baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Mjini Bariadi, lililofanyika jana
katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa
Memorial Mjini Bariadi
Hakimu Mfawidhi wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe.Mary Mrio akitoa mada katika Kongamano la Elimu ya Masuala
ya Jinsia kwa walimu na wanafunzi wa kike kutoka katika baadhi ya Shule za
Msingi na Sekondari za Mjini Bariadi, lililofanyika jana katika Shule ya
Sekondari ya Kusekwa Memorial Mjini
Bariadi.
Afisa Vijana wa
Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Bibi.Zena Mchujuko akitoa mada katika Kongamano
la Elimu ya Masuala ya Jinsia kwa walimu na wanafunzi wa kike kutoka katika
baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Mjini Bariadi, lililofanyika jana
katika Shule ya Sekondari ya Kusekwa
Memorial Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment