Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Awamu ya tatu
umeendelea kunufaisha wananchi wakiwemo wakazi wa kijiji
cha Nkoma wilaya ya Itilima na Nyakabindi
wilaya ya Bariadi mkoaniSimiyu.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini katika Kijiji cha Nkoma wilayani Itilima, Mtaa wa Nyakabindi na Mtaa wa Old Maswa wilayani Bariadi wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini katika Kijiji cha Nkoma wilayani Itilima, Mtaa wa Nyakabindi na Mtaa wa Old Maswa wilayani Bariadi wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Mmoja wa wanufaika wa Mpango
huo, Bibi. Rebecca Masunga kutoka Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi, amesema TASAF
imemsaidia kutoka katika umaskini sasa anapata kipato kinachomwezesha kujikimu,
kwa kuwa amelima ekari tatu za pamba, ekari moja ya mahindi, ana ng’ombe 14 na
mbuzi wanne na amenunua plau kwa ajili ya kulimia.
“Nilikuwa maskini wa
kutupwa , nilipoingia TASAF na kuanza kupokea zile elfu 36 nilikopa fedha
nikalima nyanya ekari moja nikauza, nilipata shilingi laki sita nikanunua
ng’ombe watatu wakakua; baadaye nikawauza
nikapata milioni moja na laki tano nilinunua ng’ombe 14 ndiyo hao mnaowaona
tunawachunga sasa” alisema Rebecca Masunga.
“Tuna kikundi chetu
ambacho tunaweka fedha zetu baadaye tunagawana, tukisha gawana tunaenda
kuzalisha, tunalima nyanya, kabeji, pamba halafu tunauza; mpango wangu wa
baadaye niwe na mtaji mkubwa na nijenge nyumba bora ” alisisitiza Bibi.Masunga.
Nae Bibi. Stella
Masamaki mkazi wa Old Maswa wilayani amesema kupitia mpango wa Kunusuru kaya
maskini aliweza kukodi mashamba nakulima pamba, baada ya kuuza pamba akajenga
nyumba bora ya vyumba vitatu na akatoka kwenye nyumba ya udongo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo amewapongeza wanufaika wa TASAF ambao wamezitumia
fedha hizo kwa manufaa na akawashauri kuanzisha miradi midogo midogo na
kuwatumia wataalamu wa kilimo pamoja na mifugo kuwasaidia katika uendelezaji wa
miradi yao ya kilimo na mifugo.
Katika hatua nyingine
Mratibu wa TASAF Wilaya Itilima Bw. John
Rajabu amesema wanufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini wameibua mradi wa
maji ambao pia utawanufaisha na wananchi wengine, ambapo mpaka kukamilika kwake
utatumia takribani milioni 15.
Wakati huo huo Wajumbe
wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wamefanya ziara katika Wilaya ya
Meatu, Itilima na Maswa na kukagua miradi ya Maji, Afya na Elimu nakuwataka
viongozi na watendaji katika maeneo husika kutimiza wajibu wao na kuhakikisha
kuwa miradi yote inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati ili wananchi waweze
kupata huduma wanazostahili.
Sanjali na hilo wajumbe
hao wamewataka viongozi kutambua fedha zinazochangwa na wananchi na kusimamia
vizuri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ili zitumike kama ilivyokusudiwa.
Baadhi ya Viongozi wa
Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakikagua shamba la pamba la
mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga(mwenye kitambaa cheupe) wa
Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Baadhi ya Viongozi wa
Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu wakiangalia mifugo ya mnufaika wa
Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa
Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akimpongeza mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya
Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi
kwa kununua jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) kwa ajili ya kulimia, wakati
wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa
wa Simiyu kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Baadhi
ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu walipotembelea na kuona nyumba ya
mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Stella Masamaki wa Mtaa wa Old Maswa wilayani Bariadi, wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akitoa maelezo ya awali juu wanafaika wa TASAF III
wilayani humo wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM
wilayani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi
akitoa maelezo ya awali juu mradi wa Maji ulioibuliwa na wanafaika wa
TASAF III katika Kijiji cha Nkoma wilayani humo wakati wa Ziara ya Kamati ya
Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Itilima, Mhe.Benson Kilangi akitoa
maelezo ya awali juu mradi wa Maji ulioibuliwa na wanafaika wa TASAF III katika
Kijiji cha Nkoma wilayani humo wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM
wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg..Fabian Manoza akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Serikali kuhusu Jengo la Wodi ya Wazazi linalojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Meatu, wakati wa ziara ya viongozi hao ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya
Maswa, Mhe.Dkt. Seif Shekalaghe akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa
ya CCM Mkoa wa Simiyu na baadhi ya viongozi wa Serikali kuhusu Jengo la Zahanati ya
Kijiji cha Mwandete inayojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wananchi, wakati
wa ziara ya viongozi hao ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
0 comments:
Post a Comment