Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amezindua rasmi leo zoezi la chanjo ya Saratani ya Mlango wa
Kizazi ambayo inatarajiwa kutolewa kwa watoto wa kike takribani 37,141 wenye
umri wa miaka 14 kwa mkoa mzima wa Simiyu.
Uzinduzi huo umefanyika katika
Uwanja wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B na kushirikisha watoto wenye umri wa
miaka 14 kutoka katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari za Halmashauri ya
Mji wa Bariadi.
Akizungumza
na wanafunzi walioshiriki katika uzinduzi wa chanjo hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa
amewataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wa kuwahamasisha wenzao kwenda kupata
chanjo na kuwahamasisha wazazi kuwahimiza watoto wa kike wote wenye umri wa
miaka 14 kwenda kupata chanjo hiyo.
Mratibu
wa Chanjo Mkoa wa Simiyu Bibi.Beatrice Kapufi ametoa wito kwa wazazi na walezi
kuhakikisha watoto wenye umri wa miaka 14, wanapata haki yao ya kupata chanjo ya Saratani
ya Mlango wa Kizazi ambayo itatolewa bila malipo katika vituo vya kutolea
huduma za afya, shule za Msingi na Sekondari.
Aidha,
amesema Mkoa kupitia Kitengo cha Huduma za Chanjo wameshatoa mafunzo kwa
watendaji, watoa huduma wote wa vituo vinavyotoa huduma ya chanjo na walimu
wanaojishughulisha na huduma za Afya katika Shule za Msingi na Sekondari zote
mkoani Simiyu.
“Nitoe
wito kwa wazazi wote kuhakikisha watoto wa kike wote wenye miaka 14 wanapata
haki yao msingi kupata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi, chanjo hii inatolewa
bure na itatolewa mara mbili, mtoto akishapata kwa mara ya kwanza atatakiwa
kwenda kupata chanjo ya pili baada ya miezi sita” alisema Kapufi.
Nao
wanafunzi waliopata chanjo wameishukuru Serikali kwa kuwaletea chanjo hiyo
ambayo wamesema itawasaidia kujikinga na maambukizi ya Saratani ya Mlango wa
Kizazi.
Muuguzi Neema Mlay akitoa
chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa mwanafunzi Happiness Robert wa Shule
ya Sekondari Simiyu wakati wa Uzinduzi wa chanjo hiyo Mkoa wa Simiyu katika Uwanja
wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B Mjini Bariadi, (kulia) Mkuu wa Mkoa huo,
Mhe.Anthony Mtaka akishuhudia zoezi hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wanafunzi wa baadhi ya Shule za Msingi na
Sekondari za Mjini Bariadi wakati wa uzinduzi wa Utoaji wa chanjo ya Saratani
ya mlango wa Kizazi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B Mjini
Bariadi.
Flora Masunga mwanafunzi
wa Shule ya Msingi Sima B akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani)
baada ya kupata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi mara baada ya uzinduzi
wa Utoaji wa chanjo hiyo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B
Mjini Bariadi.
Mratibu
wa Chanjo Mkoa wa Simiyu, Baetrice Kapufi akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) baada ya Uzinduzi wa zoezi la chanjo ya Saratani ya Mlango wa
Kizazi uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Sima A na Sima B Mjini
Bariadi.
0 comments:
Post a Comment