Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndg. Jumanne Sagini amewataka
viongozi wa dini kwenda kuwa chachu ya kuibadilisha jamii ,
kuhusu matumizi ya nishati na maji ,na namna ya kutoa taarifa wanapouziwa
bidhaa isiyo na kiwango .
Sagini ametoa ushauri huo alipokutana
na viongozi hao mjini bariadi ,ikiwa ni mwendelezo wa Baraza la Ushauri
watumiaji Nishati na Maji kuyafikia makundi mbalimbali kueleza umuhimu wa
chombo hicho. .
Sagini amesema viongoni wa dini ni
watu muhimu katika jamii ,hivyo ni vema elimu waliyoipata wakaitumie katika
kupunguza changamoto za nishati na maji kwa kutumia ujumbe mbalimbali.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Mtendaji
wa Baraza la Ushauri la watumiaji Nishati na Maji Getruda Mbilinyi amesema kuwa
kukutana na kundi la viongozi wa dini ambao wanaushawishi mkubwa katika jamii
itasaidia wananchi wengi kuzijua haki zao ,pale wanapopata huduma
zisizoridhisha
Baadhi ya viongozi wa dini wamesema
kuwa mafunzo hayo waliyoyapata watayatumia kuwaelimisha waumini wao kupitia
mahubiri faida za utumiaji nishati hiyo.
Mafunzo kwa viongozi wa dini
yaliyokuwa ya siku moja yaliandaliwa na Baraza la Ushauri , Watumiaji wa
huduma za Nishati na Maji baina ya viongozi themanini na mbili wa dini na
Kamati ya watumiaji wa huduma ya nishati na maji ,halmashauri ya mji wa bariadi
,lengo likiwa utoaji elimu kuhusiana na upatikanaji wa huduma bora kwa wateja.
0 comments:
Post a Comment